NDUGU MZAZI; barua ya wazi kwa wazazi na walezi wote


Ndugu mzazi: barua ya wazi kwa wazazi na walezi wote

Unaweza kumpenda mtoto anayepata A darasani na kumchukia anayepata C au F. Lakini anayepata A darasani inawezekana asipate A maishani.
Tujifunze kupenda watoto wote na kuwajali watoto wote kwa usawa.
Ndugu wazazi A ya darasani haimaanishi maisha yatakuwa mazuri. Na maisha mtaani yalivyo hayapimwi kwa viwango vya A za darasani.
Mwanao akienda benki hataulizwa kuonesha alipata A ngapi darasani. Benki wanachohitaji kuona ni je, ana pesa mkononi?
Ndugu mzazi, mwanao akianzisha biashara au kufungua kampuni, hatatakiwa kuonesha A za darasani.
Na hata akienda kukata tiketi ya ndege hawaulizi “tuoneshe A ya darasani ili tukukatie tiketi”. Wanachojali na WANACHOTAKA kuona ni Je mfuko unasoma?
Ndugu mzazi kama kuna kitu cha muhimu unapaswa kumfundisha mtoto wako basi mfundishe umuhimu fedha. Mfundishe namna ya kutafuta fedha na namna ya kuzitumia.
Mfundishe namna ya kuwekeza akiwa bado mdogo ni hazina kubwa ambayo ukimpa hatakusahau.
Ndugu mzazi, sio kwamba nimesema usimpeleke mtoto wako shuleni. Na wala sijasema mtoto wako asisome ila napenda ufahamu kwamba maisha ni zaidi ya A za shuleni.
Napenda ufahamu kwamba shuleni unafundishwa kusoma na kuandika. Ila maisha yanahitaji usome kweli na kuandika kweli kweli.

……………………………………………………………..Ndugu mzazi, usibaki tu kumwambia mtoto wako kwamba Kuna shetani. Ukiishia kusema hivyo utakuwa unalea kilaza. Mwambie kabisa kwamba anapokuwa amepanga kufanya majukumu yake ya siku na akawa hayajayafanya huyo ndiyo SHETANI mwenyewe.
Mwambie akipokea elfu kumi na akaitumia yote ikaisha huyo ndiye SHETANI mwenyewe
Mwambie akiishi maisha bila ya kuwa ndoto, kusudi wala malengo shetani anakuwa amemtawala.
Mwambie akiamini kila kitu anachoambiwa bila kufikiri na kufikia uamuzi wake mwenyewe na huyo ni shetani pia.
Mwambie akiishi chini ya viwango vyake huyo pia ni shetani anakuwa amemtawala.
Mwambie akianza kitu na akaishia njiani huyo ndiye shetani mwenyewe.
………………………………………………………………Ndugu mzazi, kama umeajiri wafanyakazi wa ndani basi mwanao asibweteke tu na kukaa bila kufanya kazi. Itakuwa ni Jambo la ajabu mfanyakazi wa ndani akawa anafanya usafi wa ndani na mwanao yupo tu kwenye kochi ananyanyua miguu ili mfanyakazi afanye usafi.
MAKALA ni ni sehemu ndogo sana ya kitabu. Kupata kitabu hiki hapa utalipia kiasi cha shinfi elfu mbilil tu. ukilipia elfu 2 utaunganisha na kundi la think big for Africa ikiwa ni pamoja na kupata kitabu hiki hapa cha kipekee sana.
Lipia kwa namba 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Karibus sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X