UKIAMBATANA NA MASIKINI WATANO, WEWE NI MASIKINI WA SITA


UKIAMBATANA NA MASIKINI WATANO, WEWE NI MASIKINI WA SITA



Ukiambatana na masikini watano, wewe ni masikini wa sita. Ukiambatana na matajiri watano, wewe ni tajiri wa sita.  Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu waliokuzunguka wanakuwa na mchango mkubwa kwa kile unachokuwa.

Jim Rohn aliwahi kusema kuwa wale watu waliokuzunguka  wanakuwa na mchango mkubwa sana kwa kile ambacho unakuwa. Ukitafuta wastani wa kipato cha watu watano waliokuzunguka utagundua kwamba hamjazidiana  sana.
Ukifuatilia mahusiano ya wale watu ambao wamekuzunguka, utagundua kuwa hamjatofautiana sana kimahusiano. Yaani nyote mna mahusiano yanayoendana endana.
Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa unakuwa na timu nzuri ya marafiki wako watano wa karibu sana. Maana Hawa Wana mchango mkubwa sana kwa kile kitu ambacho unakuwa maishani mwako.
Kama maishani mwako utaamua kufanya uamuzi wa maana sana. Basi hakikisha kwamba unafanya uamuzi wa marafiki wachache wa kuambatana nao. Hawa wanapaswa kuwa wale ambao wanakupa nguvu, sio wale ambao muda wote wanakuambia mkapige stori.
Hawa wanapaswa kuwa watu wanaofikiri nje ya boksi, sio wale ambao muda wote wanalalamika kwamba maisha mabaya.
Hawa wanapaswa kuwa wale ambao ukikosea wanakuwa tayari kukwambia ukweli, sio wale wanaokwambia wewe Ni jembe wakati wewe hauna lolote la maana.
Hawa wanapaswa kuwa wale ambao ulifanikiwa wanaturahi, sio wale ambao ukipata fedha tu wanaanza kusema siku hizi unajidai.
Hawa wanapaswa kuwa wale wenye kiu ya maarifa na mafanikio. Sio wale ambao wakikuta unasoma wanaanza kusema waliosoma walikuwa wa zamani.
Hawa wanapaswa kuwa wale ambao penye tatizo wanaona fursa, sio kwenye tatizo wanaona tatizo zaidi.
Hawa wanapaswa kuwa wale ambao ukikaa nao unajiona Kama hujui(sio kwamba wanakushusha hadhi ila kwa jinsi wanavyojifunza na kuwa na ufahamu mkubwa) sio wewe unaonekana ni gwiji kwenye kundi lako.
Sasa nikuulize marafiki zako ni wa aina gani?
Tafakari, chukua hatua

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
Unaweza kuwasiliana naye kwa namba hii hapa 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X