Vitabu Vitano Ambavyo Kila Muhitimu Wa Chuo Kikuu Anapaswa Kuanza Kusoma Mara Moja


Siku sio nyingi Sana, NILIANDIKA makala yenye kichwa cha WANAOSHEREHEKEA KUHITIMU CHUO TUWAAMBIE UKWELI? AU TUWAACHE KWANZA WAFUMUE NYWELE ZAO ZA GRADUATION?
Moja kati ya vitu ambavyo nilieleza kwenye makala hii ni wahitimu wa chuo kujenga tabia ya kusoma vitabu na kuwa tayari kujifunza.

Kwenye maisha ya mtaani huwezi kuja na ile hali ya kusema kwamba mimi nilikuwa kipanga shuleni kwa hiyo na huku nitaendelea kuwa kipanga.

SOMA ZAIDI: Kwa Nini Wanafunzi wanaopata A Wanawafanyia Kazi Wanafunzi Wanaopata C Na Kwa Nini Wanafunzi B Wanaifanyia Kazi Serikali

Maisha ya mtaani yanahitaji kujifunza kila siku. Kinachofanya kujifunza muhimu ni
Moja, kutokana na mabadiliko ambayo yanaendelea kutokea kila kukicha.
Pili kwa sababu unahitaji zaidi ya ujuzi mmoja. Yaani unahitaji kujua utunzaji wa hesabu, mauzo, masoko, utengenezaji wa bidhaa, ushawishi, uongozi, uandishi, elimu ya fedha, elimu ya malengo  na mengineyo mengi.

Sasa haya yote hujajifunza darasani  kitu ambacho kinafanya kujifunza kuwe ni lazima. Kiukweli mtaani huwa hakuna kuhitimu.

Kwa sababu hiyo hapa ninaenda kukuelekeza vitabu vitano ambavyo utaanzia maisha. Vitabu ambavyo vitakupa mwongozo na kufanya uanze kuiona dunia kwa jicho la tofauti kabisa.

1. The Leader who had no title. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Robin Sharma. Kikiwa kimeleta kanuni za uongozi katika Zama hizi mpya.

Umetoka shuleni ukiwa umezoea kusukumwa. Yaani mpaka uambiwe kwamba unapaswa kufanya  ya kitu fulani ndio unafanya.
Umezoea kusimawiwa ili kazi zifanyike. Ila sasa hivi msimamizi wako nambari moja ni wewe mwenyewe. Hii ndio kusema kuwa kitu cha kwanza kabisa unachohitaji kujifunza ni uongozi. UNAPASWA KUJIONGOZA MWENYEWE BILA YA KUHITAJI KUWA NA CHEO.

Soma zaidi: Ukisikia Fulani Ni KIONGOZI, Basi Jua Anafanya Hivi

2.  The Richest Man In Babylon
Kitabu hiki kimeandikwa na Clason. Kina masomo makubwa sana kuhusu fedha na kutengeneza utajiri. Ukishajifunza namna ya kuwa KIONGOZI wako mwenyewe. Sasa njoo na hizo mbinu za kiungozi kwenye masuala ya fedha.

Kwenye kitabu hiki utakutana na dhana muhimu kuhusu fedha ambazo hukuwahi kuambiwa sehemu nyingine. Utakutana na dhana ya kujilipa mwenyewe.
Utakutana na dhana ya kuwekeza. Na vingine vingi.

3. THINK AND GROW RICH
Hiki Ni kitabu kingine ambacho kwa mara ya kwanza litabadili fikra zako kabisa. Ngoja nikwambie kitu. Unahitaji kufikiri tofauti ili uanze kupata matokeo ya tofauti.

Hiki nj kitabu ambacho mpaka sasa hivi kumetengeneza mamilionea wengi kuliko kitabu kingine. Kwenye kurasa za kitabu hiki utakutana na masomo 13 ambayo Kama utaanza kuyatumia mara mkja basi yatabadili fikra zako milele na milele.

4. RICH DAD POOR DAD
Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Robert Kiyosaki ambaye pia ameandika vitabu vingine kama Cashflow Quadrant na Before you quit your job.

Kitabu hiki kitakuonesha kuwa Mambo mengi ambayo umekuwa unajifunza kuhusu pesa sio sahihi.

Umekuwa unapokea fedha unakimbikia kununua runinga au kununua simu kubwa na ya kisasa. Lakini Sasa kwenye kitabu hiki utaelekezwa kwamba kitu bora cha kununua. Sio kwamba hujui kununua, bali umekuwa hufanyi manunuzi sahihi.

Kwenye manunuzi unaweza kununua RASILIMALI (ASSETS) au DHIMA (liability).
Rasilimali inakuingisia pesa mfukoni na dhima inatoa pesa mfukoni mwako. Sasa nikuulize. Runinga inakuingizia fedha? Simu je?
Kitabu hiki kinakuhusu sana.

5. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.
Ninajua unahitaji kutengeneza kesho Bora. Tena kuanzia hapo ulipo. Kitabu Cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kina mbinu kanuni za Kukuwezesha kutengeneza kesho Bora kuanzia hapo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kitabu hiki SOMA HAPA

Rafiki yangu kama ambavyo unaona hapo juu. Hivyo ni vitabu muhimu ambavyo kama utaanza kuvisoma sasa hivi vutabadili maisha yak kwa kiwango kikubwa sana.

TAARIFA MUHIMU KWAKO.  kila mara nimekuwa nikishirikisha watu vitabu. Na kila nikifanya hivyo lazima anajitokeza mtu ambaye anakuja kuomba atumiwe vitabu hivyo. Watu wengine wamekuwa wakipoteza vitabu hivi na hivyo kuniomba nitume vitabu hivi mara nyingine na nyingine.

Sasa ili kurahisisha maisha. Nimeamua vitabu vyote ambavyo nitakuwa nashauri watu wavisome, viwekwe kwenye kundi moja la telegram. Kwenye kundi hilo  kutakuwa na uwezo wa kuomba vitabu na ukatumiwa. Lakini pia utakuwa unaruhusiwa kutuma vitabu kwa watu wengine. hivvo  basi kama umesoma hapa na ungependa kupata vitabu ambavyo nimesema hapa, jiunge kwenye kundi hili la telegram HAPA ili uweze kupata vitabu hivi bure kabisa.

Nakutakia kila la kheri rafiki yangu

Godius Rweyongeza
0755848391


3 responses to “Vitabu Vitano Ambavyo Kila Muhitimu Wa Chuo Kikuu Anapaswa Kuanza Kusoma Mara Moja”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X