๐๐๐๐๐
Huwa inatokea mara nyingi maishani kwamba watu wanashabikia na kupenda mabadiliko yatokee maishani Ila wao huwa kusababisha mabadiliko hayo ni vuta nikuvute
Huwa inaonekana vizuri kumshangilia KIONGOZI wa siasa ambaye anahaidi kuwa mara tu baada ya kuingia madarakani atafanya mabadiliko moja, mbili na tatu
Kitabu Cha WHO MOVED MY CHEESE kimezungumzia sana kuhusu mabadiliko ambayo huwa yanatokea kwenye jamii. Kwenye kitabu hiki ninaweza kusema kwamba watu wamewekwa kwenye makundi matatu linapoja suala la mabadiliko.
Kundi la kwanza, Ni lile ambalo linajua kwamba lazima tu mabadiliko yatatokea na hivyo linajiandaa. Linajua tu ikitokea kuna mabadiliko yoyote yametokea basi na lenyewe litabadilika Mara moja na kuchukua hatua. Hili ni kundi la wale ambao wanajua kuwa maisha ni wajibu wao. Linajua kuwa kushinda na kushindwa ni wajibu wao .
Watu walio kwenye kundi hili, kila mara huwa wanaofuatilia kujua Kama mabadiliko ambayo yameshaanza kutokea ili wasije kushangazwa na mabadiliko yoyote ambayo yametokea.
Kundi la pili, ni la wale watu ambao huwa wanastukia mabadiliko yametokea ila hawajui mabadiliko haya yametokeaje. Wanashangaa tu kuona kitu fulani kinaendelea. Japo kundi hili huwa linabadilika baadae, lakini huwa linafanya hivyo kwa kuchelewa sana.
Kundi la mwisho kabisa ni kundi la watu ambao wanaendelea kushikilia mila na na desturi na hawapo tayari kubadilika. Kiafrika afrika hawa ndio wale huwa wanasema mababu walikuwa wanafanya hivi na hivyo hatuwezi kubadili namna walivyokuwa wanafanya. Hawa ndio wale ambao huwa wanasema, haikuwahi kufanyika hivyo kabla. Yaani Hawa huwaambii kitu, wanashikilia kile kitu cha zamani kama msahafu.
Kati ya hizo aina tatu zote, bila shaka kwa haraka unaweza kujua ni aina gani inafurahia sana maisha. Ni aina ya kwanza. Ila sasa kuwa kwenye kundi hili la kwanza ni vigumu sana.
Ni vigumu kwa sababu watu watakusema ukiwa kwenye kundi hili.
Ni Ni vigumu pia kwa sababu ya uoga.
Ni vigumu kwa sababu ya marafiki ambao wanapenda tuendelee kufanya mambo kama yalivyokuwa yakifanyika hapo zamani.
Hivyo inahitaji kujitoa ili uweze kuingia kwenye kundi la kwanza.
Mwandishi Spencer kwenye kitabu chake cha WHO MOVED MY CHEESE? ametuahirikisha hadithi yenye funzo kubwa sana maishani mwetu.
Hadithi hii inaanza kwa kuwakutanisha vijana waliokuwa marafiki wa ukweli chuoni. Sasa nu miaka michache baadae wamekutana kujadili juu ya mabadiliko na mmoja wa wale vijana anatoa hiyo hadithi ya WHO MOVED MY CHEESE? Hadithi hii imejaa mafunzo mwanzo mpaka mwisho Ila kikubwa zaidi kikiwa ni juu ya MABADILIKO.
1. Kitu cha kwanza kutoka kwenye hiyo hadithi ni aina hizo tatu za watu, naomba wewe ujiulize upo kwenye kundi gani?
2. Hivi ni kitu gani ungefanya kama usingekuwa na uwoga? Hili ni swali ambalo mmoja wa wahusika kwenye hadithi alijiuliza mara kwa mara, hasa pale alipokuwa anaogopa na kutaka kurudi nyuma.
Kwa kujiuliza swali hilo aliamua kusongambele bila kuogopa na kufikia kuleta mabadiliko.
3. Ukiogopa kubadilika unazuia majibu ya maswali yakiyojificha mbali kidogo tu.
4. Ukiwa mtu wa kuangalia mabadiliko madogo kunakufanya usije kustuka yametokea mabadiliko makubwa sana. Maana utakuwa unaendana na hayo mabadiliko mabadiliko madogo madogo yanayotokea kila siku.
5. Kuna nyakati utapaswa kujicheka mwenyewe kutokana na makosa ambayo unafanya na kisha uamue kusongambele.
6. Mambo yanapobadilika na wewe badilika mara moja. Usianze kukaa kwenye eneo hilo hilo na kulalamika.
Kwenye hadithi ya kitabu kuna kajamaa kalikataa kubadilika baada ya mabadiliko makubwa kuwa yametokea.
SOMA ZAIDI: ZAMA ZIMEBADILIKA, maisha yamebadilika, ajira hatarini na wewe badilika.
7 Unapaswa kujua jibini zako ni zipi. Kwa mwingine jibini zake Zinaweza kuwa ni nyumva nzuri, kwa mwingine gari, kwa mwingine biasharabyenye mafanikio wakati mwingine ni familia yenye furaha. Je, wewe jibini zako ni zipi?
8. Siku zote Kuna jibini (cheese) mpya huko? Ni wewe tu kuamua kuzitafuta
Kiukweli kitabu hiki cha WHO MOVED MY CHEESE. Kimejaa mafunzo mengi sana ambayo yatakuinua wewe binafsi.
Kitabu hiki hapa kimetolewa kama audiobook jumatatu ya leo kwenye kundi letu la telegram la AUDIOBOOKS TU. Nikukaribishe uianze wiki yako kwa kujipatia kitabu hiki kwa mfumo wa audiobook.
Ndani ya kundi hili hapa tunapata audiobooks mbili kila wiki. Yaani kila jumatatu na alhamisi.
Kujiunga unalipia 3,000 kwa mwezi. Ambayo ni sawa na 18,000 kwa miezi sita. Sawa na 32,000 kwa mwaka. Ila ukilipia kwa mwaka mzima utalipa elfu 30 tu.
Ebu chukua hatua uwe miongoni mwa watu ambao wanaenda kuwa wanajipatia vitabu kwa mfumo huu wa audiobooks na kusikiliza popote pale bila usumbufu.
Unalipia kwa namba 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA Kisha unatuma ujumbe wenye kwa telegram ili kukutaarifu baada ya hapo nitakuunga na utaanza kufurahia vitabu hivi.
WHO MOVED MY CHEESE?? Audio hii si ya kukosa aiseeh!!!
Makala hii imeandaliwa na Godius Rweyongeza.
Unaweza kuwasiliana naye kwa 0755848391
Au tembelea www.songambeleblog.blogspot.com kujifunza zaidi.