(utashangaa kwa nini ulichelewa kujua hiki kitu)
Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Leo hii naenda kukufundisha namna ya kutengeneza bahati maishani mwako.
Na njia hii ya kutengeneza bahati ni kuwasaidia watu zaidi kupata bahati. Ukiwasaidia watu kupata wanachotaka utakuwa umewawezesha kupata bahati. Na kwa kuwa hili utakuwa umefanya jambo jema sana basi watu hao baadae watakuwa tayari kukulipa kwa kile unachofanya.
Wanaweza wasikulipe leo. Ila kadri utakavyokuwa unaendelea kuwasaidia watu wengi zaidi basi ujue kwamba watu hao pia watakuwa tayari kukulipa kwa kazi ambayo utakuwa unafanya
Hivyo kuanzia sasa hivi ninapoongea na wewe, anza kutengeneza bahati kwa kuwasaidia watu zaidi waweze kupata kitu ambacho wanataka. Sasa nikuulize, unaenda kuwasaidiaje watu? Utawapa nini?
Naomba uchukue muda kutafakari. Kama Unaweza kunishirikisha kile ambacho unaenda kuwasaidia watu kwa kutuma ujumbe wako hapa. https://wa.me/255755848391
kama pia hujajua namnanunavyoweza kutengeneza bahati za watu wengine basi na wewe nitumie ujumbe wako hapa
https://wa.me/255755848391
Nikutakie siku njema
Ni mimi Rafiki wako wa Ukweli Godius Rweyongeza