Jiepushe Na Vitu Hivi Viwili Ili Uweze Kupata Matokeo Mazuri Maishani Mwako


Kuna makosa mawili ambayo umekuwa unafanya kwenye maisha yako ya kila siku ambayo kiukweli unapaswa kuyaepuka mara moja. La sivyo kama utaendelea kuyafanya makosa haya yatakufanya upoteze rasilimali hizi mbili muhimu. Utapoteza rasilimali muda lakini pia utapoteza rasilimali nguvu. Ukiyaepuka utaweza kukutumia muda wako vizuri kufanya mambo ya maana, lakini pia uwekeza nguvu hiyo kwenye kufanya mambo ambayo yanakujenga au kukuongezea kipato kwenye maisha yako.
MOJA EPUKA KABISA KULALAMIKA
Moja ya kitu ambacho watu wengi wanapenda kufanya kwenye maisha ni kulalamika. Kitu kidogo tu utakuta kwamba mtu analalamika. Wanailalamikia serikali, wanawalalamikia wazazi au kuwalalamikia watu. Katika maisha na katika hali yoyote ile ambayo wewe utakuwa nayo, huwezi kukosa mtu ambaye unaweza kumlalamikia.
Hata ukijikwaa njiani unatembea peke yako lazima mtu wa kulalamikia tu utampata. Hata ukichelewa kazini lazima tu utapata wa kulalamikia. Unaweza kukuta unamlalamikia mtoto kwamba alichelewa kuamka, au unalalamikia daladala kwamba walichelewa kufikisha gari ulipokuwa umekusudia, au pengine utalalamikia barabara kwamba ni mbovu na hivyo zimekufanya wewe uchelewe. Kwa vyovyote vile mtu wa kulalamikia hajawahi kukosa hata siku moja.
Ila ukifuatilia kwa umakini utagundua kwamba hivi vitu unasababisha wewe mwenyewe. Na ili uweze kugundua hili, wewe kila likitokea tatizo hakikisha kwamba unajiuliza hivi, imeukwaje mimi nikasababisha hili tatizo. Lazima utagundua kwamba kuna sehemu ambayo wewe umechangia kusababisha hilo tatizo.
Kwa mfano tuseme kwamba umechelewa kazini.
Ukijihoji kwa umakini utagundua kwamba wewe hapo kuna namna ambavyo umesababisha kuchelewa kazini . pengine ulichelewa kuamka au ulijizungusha sana nyumbani kiasi umechelewa au hukupangilia siku yako tangu jana hivyo leo umekurupuka tu ukawa unafanya kila kitu. Au umeanza kupiga stori na mshikaji au shoga wako. Kwa vyovyote vile ukifuatilia utagundua kwamba wewe hapo ndiye msababishaji wa hili tatizo na hakuna mtu mwingine ambaye amesababisha tatizo hili hapa.
Kwa  hiyo basi badala ya kuanza kuwalalamikia watu wengine wewe tafuta kujua ni kwa jinsi gani wewe umesababisha hilo tatizo ili uweze kuliepuka hilo tatizo siku nyingine.

KITU CHA PILI NI KUFUATAILIA MAISHA YA WATU WENGINE
Kama umekuwa na tabia hiii hapa unahitaji kuiepuka mara moja. kwenye maisha  mtu pekee ambaye unahitaji kuhakikisha kwamba unamfuatilia kila siku ni wewe mwenyewe. Usihangaiike kumfuatilia mtu mwingine, maana maisha ya mtu mwingine hayawezi kukusaidia kitu chohcote kile. Hivyoo jifuatilie wewe mwenyewe uweze kujijua kiundani zaidi.
Kwa mfano, jifuatilie ujue kwamba kwa siku unaingiza shilingi ngapi. Jifuatilie ujue kwamba unatumia muda gani mtandaoni na huo muda unakuwa unafuatilia vitu gani. Jifuatilie ili ujue kwamba unaongea na watu gani kwenye simu na hao watu mnaongea kitu gani kwa pamoja. Jifuatilie ujue kwamba chakula gani unakula na je, hicho chakula ni chakula bora kwa ajili ya afya yako. Jifuatilie ili uweze kujua kama unafanyia kazi malengo au au bado uko nyuma sana katika kuyafikia.
Kiukweli kama hutajifuatilia wewe mwenywe ujue kwamba utakuwa unajipoteza na mwisho wa siku utabaki nyuma na utahidwa kukamiliha mambo muhimu sana kwenye maisha.

SOMA ZAIDI: Vitu Sita (06) Ambavyo Utapaswa kuvifanya Maishani Mwako
Rafiki yangu hayo ndiyo mambo muhimu ambayo nilipenda uyafahamu ndani ya siku hii ya leo. Hivyo nikutakie kila la kheri kwenye kazi zako na katika utekelezaji wa majukumu yako. Leo kwenye mtandao wa youtube nimekuandalia video nzuri sana. Unaweza kuendelea mbele kuiangalia hapa ili uweze kujifunza zaidi na kuchukua hatua. https://youtu.be/TjMSSwdHWIk
Tafadhali sana naomba usisahau kusbscribe ili uweze kupata video nyingine kwenye mtandao huo wa youtube. https://youtu.be/TjMSSwdHWIk

KUPATA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU BONYEZA HAPA
KUPATA VITABU BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X