Ukiona unavutwa nyuma zaidi basi jua kwamba ukiachiwa ndio utakimbia kam upepo


Changamoto na vikwazo huwa havikosi kujitokez kwenye maisha. Tofauti ni ukubwa wa changamoto ambayo mtu huwa anakutana nayo.  Sasa changamoto yako inapokuwa kubwa usikate tamaa na kuacha kufanya kile kitu ambacho unapasawa kkuwa unafanya. Unapasawa kujua kwamba kadri unavyokutana na changamoto kubwa kwenye maisha yako basi ujue kwamba ukishaitatua hiyo changamoto utasongambele kwa kasi kubwa sana. Na kadri unavyokuwa na changamoto kubwa ndivyo utaweza kusonga mbele zaidi.

Kadri changamoto zinavyokuvuta nyuma zaidi fahamu kwamba ukianza kutoka huko nyuma na kuchomoka. Basi utakimbia kama upepo. Hivyo endelea kushikilia hapo hapo uliposhikilia kila siku. Weka juhudi. Ila fahamu ukitoka huko nyuma, watu wengine watakuona ukivuka ng,ambo.

Zimebaki siku 2 tu ambapo utaweza kupata vitabu vyangu vyote kwa 20,000. Ikiwa ni zawadi yangu kwako ndani ya mwaka huu 2020. Lipia sasa hivi kupitia 0755848391 jina Godius Rweyongeza kisha nitumie ujumbe wenye jina lako.

Kama una kitabu kimoja kati hivyo utalipia elfu 16 tu. kama una zaidi ya kimoja na ungependa kupata vilivyobaki wasiliana namikupitia 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X