Ebu fanya kitu hiki hapa siku ya leo kuongeza mtadao wako


Siku ya leo ningependa iwe siku yako kuongeza mtandao wako wa watu ambao unawafahamu. Na hapa tunaenda kutumia tu mbinu za kawaida ambazo wewe mwenyewe unaweza kuzitumia kukongeza idadi ya mtandao wako.
Siku ya leo nataka umpgie mtu ambaye hujawahi kumpgia maishani mwako.
Anaweza akawa mtu ambaye umekuwa unamfuatilia kwa kazi anazofanya kila siku. Au anaweza kuwa ni mtu ambaye umekuwa ukijifunza kwake kwa namna yoyote ile. Au anaweza kuwa mtu maarufu, anaweza kuwa ni mtu ambaye unaona kwamba huyu kuna siku anaweza kunisaidia kukutana na mtu mwingine au anaweza kunisaidia kufanikisha kitu fulani. Anaweza pia akawa mtu ambaye unajua ana tatizo ila suluhisho la tatizo hilo ni wewe hapo.
Kwa vyovyote vile hakikisha unatafuta jina la mtu mmoja tu ambaye hujawahi kuwasiliana naye maishani  mwako.
Sasa ukishakuwa na jina la huyu mtu anza kujiuliza unaendaje kupata namba ya huyu mtu. Je, utaipata kwa kutumia mzunguko ambao unao sasa hivi. Jiulize ni watu gani kati ya hawa ambao mimi nawafahamu sasa hivi wanaweza kuwa msaaada kwenye kuipata namba ya huyu mtu? Kama hakuna hata mmoja usihofu. Nenda mbele kwa kuitafuta google. Andika google jina la mtu huyo kisha tafuta namba yake.
Kama haipatikani google basi ulizia hata kama unaweza kupata namba ya mtu wa karibu yake ili uanze kuwasiliana na huyo mtu.
Bila shaka kwa njia hizi nina hakika hutakosa namba yake. Kama ulikuwa nayo ila hujawahi kuitumia basi leo ndio leo, asemaye kesho ni mwongo. Baada ya hapo weka vocha kisha piga. 
KUMBUKA: Kama ni mara yako ya kwanza kabisa unawasiliana na mtu usianze kwa kumtumia ujumbe (hii ni kanuni yangu na ninaitumia sana) hasa mtu huyo anapokuwa mkubwa au anapokuwa ni mtu ambaye unapenda kujifunza kwake zaidi. Mimi kwenye hili huwa naendeshwa na falsafa ya kwamba,
Kama ninaweza kuonana na  mtu ana kwa ana basi sipigi. Kama ninaweza kupiga siandiki ujumbe. Hii ndio kusema kwamba kwangu ujumbe mfupi huwa ni jambo la mwisho kabisa baada ya kuona njia zote zimeshidwa.
Ukipiga hakikisha kwamba unazingatia yafuatayo;
KWANZA,   Hakikisha kwamba kabla ya kupiga unamjua huyu mtu nje ndani. Jua anafanya nini, ili unapoanza kuongea naye unaongea naye vitu vinavyoeleweka. Kwa hiyo fanya utafiti wa kutosha kabla ya kupiga simu
PILI, Mpongezea kwa kazi anayofanya. Au mshukuru kwa jinsi kazi zake zilivyoweza kukusaidia wewe.
TATU, Muulize maswali mahsusi ambayo ungependa kujifunza kutoka kwake. Kisha msikilize anavyoyajibu hayo maswali. Muulize tena maswali mengine ili upate majibu zaidi
NNE, Kama kuna tatizo kwenye biashara yake na wewe unaweza kulitatua, basi mwambie kwamba unaweza kulitatua hilo tatizo.
MWISHO, kama kuna kitu ambacho ungependa huyu mtu akusaidie mwambie bila kusita. Hiki kitu sio kwamba nimekiweka mwisho kwa bahati mbaya ila nimekiweka mwisho maksudi kwa sababu kinaenda hivyo tu. kwa hiyo basi, nikusihi ufuate hizi hatua  ili uweze kufikia hatua kunwa kwenye kile ambacho unafanya.

Hayo ndiyo mambo ya muhimu ammbayo naamini kama kwa siku ya leo utayafanyia kazi basi utaongeza mzunguko wako wa watu ambao unawafahamu. Usisite kuhakikisha kwamba unawasiliana nam ili kunipa mrejesho wa kile kilichotokea. Wasiliana name kwa whatsap tu, 0755848391
Nikuktakie kila la kheri
Ni mimi anayejali mafanikio yako
GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X