Epuka Haya Makosa Matano (05) Wakati Unaanzisha Biashara


kitabu hiki kipo kwa ajili yako. kinapatikana kwa shilingi elfu tano tu
tuwasiliane kwa 0755848391


Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Karibu sana kwenye makala ya leo ambapo ninaenda kukuonesha makosa matano ambayo unapaswa kuepuka kama kweli una mpango wa kuanzisha biashara, yenye mafanikio makubwa. ni vizuri uyafahamu haya makosa mapema, ili usije ukaanzisha biashara huku ukiona kwamba  hakuna mafanikio. Epuka makosa haya matano wakati unaanzisha biashara, ili uweze kuanzisha biashara yenye mafanikio makubwa.
KOSA LA KWANZA; EPUKA KUKOPA ILI UANZISHE BIASHARA
Hili ni kosa kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wanafanya wakati wa kuanzisha biashara, watu wanakopesha pesa ili kuanzisha biashara. Nipende kukwambia ukweli rafiki yangu kwamba haupaswi kukopa ili uanzishe biashara. Badala yake unapaswa kuanza kujijengea utaratibu wa  kuweka akiba kwa kila pesa ambayo inapita mkononi mwako. Ujue pesa ambayo inapita mkononi mwako ni nyingi ila sasa wewe umekuwa hauweki nguvu katika kuhakikisha kwamba unatoa akiba yako na kuiweka pembeni ili akiba hii iweze kukusaidia katika kuja kuanzisha kitu cha tofauti hapo baadae.
Siku hizi imekuwa ni rahisi sana kupata mkopo kutoka kwenye taasisi ambazo zinakopesha. Taasisi nyingine zitakufuata,  na kukuomba wewe uchukue fedha ya mkopo, ili uweze kuanzisha biashara. Usitumie kigezo cha kwamba unakopesheka kuchukua mkopo benki. Hata kama wewe ni mfanyakazi wa benki.
Unapoanza biashara, kuna vitu vingi ambavyo unakuwa hujui mpaka pale utakapoingia kwenye biashara. Na biashara nyingi huwa hazisimami ndani ya siku moja. kwa hiyo utaanza kuhangaika katika kuhakikisha kwamba unaijenga biashara yako mwanzo, mwanzoni kabisa. na pengine utakuta kwamba fedha zaidi itakuwa inahitajika kwa ajili ya kuendesha biashara. Ambayo inakuwa ni fedha zaidi ya ile ya mwanzo.
Sasa katika kipindi hiki hapa, ambapo wewe mwenyewe utakuwa unapigana katika kuhakikisha kwamba biashara yako imekaa vizuri, benki itakuwa inahitaji pesa ambayo walikukopesha. Unaweza kuanza kuona kwamba biashara ni chungu mwanzo, mwanzoni ila kumbe tatizo utakuwa umelisababisha wewe mwenyewe kwa kupuuzia maarifa haya muhimu.
Hivyo kama ambavyo nimekwambia hapo awali. Anza. kuweka akiba sasa hivi ili akiba hiyo ije kukusaidia kuanzisha biashara kubwa.
Au anzisha biashara ndogo kwanza ambayo haihitaji mtaji mkubwa kwanza, ili upate fedha kutoka huko ambayo itakusaidia kuanzisha biashara kubwa
Au anza biashara kubwa kwa kuanza kidogo kidogo.
Hivyo ndivyo unaweza kuepuka kosa la kwanza kabisa ambalo watu wanafanya kwenye biashara rafiki yangu mpendwa.
KOSA LA PILI NI KUKOSA JINA LA BIASHARA
Hili ni kosa jingine ambalo watu wanafanya wanapoanzisha biashara. Yaani, unaanzisha biashara yako bila ya kuipa jina. Kiukweli rafiki yangu naomba usije ukafanya kosa hili hapa. ujue vitu vyote hapa duniani vinapewa majina.
Mtoto akizaliwa tu anapewa jina. Nchi zote zina majina, ndege zina majina, hadi pikipiki zina majina. Sasa kwa nini wewe ukose jina la biashara yako? Tena kibaya zaidi ni pale ambapo unakuta kwamba wewe una mbwa ambaye ana jina, ila biashara yako haina jina. Kwa hiyo nakuomba sana ujitahidi katika kuhakikisha kwamba biashara yako inakuwa na jina kabisa. jina la biashara linapaswa kuendana na aina ya biashara ambayo unafanya. Kwa maelezo zaidi kuhusu jina la biashara, basi usisite kusoma kitabu changu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA  WA KUANZISHA BIASHARA. Kitakufaa sana. Tuwasiliane kwa simu 0755848391
TATU, EPUKA KUANZISHA BIASHARA KWA SABABU KILA MTU AMEANZISHA HIYO BIASHARA
Usianzishe biashara kwa sababu kila mmoja unaona anakimbizana na hiyo biashara. Au kwa sababu kila mtu anasema  kwamba inalipa basi na wewe unakimbia kufanya biashara hiyo hiyo. Ni wazi kwamba hii biashara, haitakuwa biashara yako.
Kitu hiki kitakuepusha wazi wazi na makosa ambayo watu huwa wanafanya kwa kujirundika sehemu moja na aina moja ya biashara. Kiukweli wewe hapo haupaswi kutengeneza ushidani usio wa lazima. Yaani, kama unaona biashara imeanzishwa, na wewe huoni kama unaweza kufanya kitu cha tofauti ambacho kitakupa upenyo basi usitengeneze ushindani usio wa lazima.
Ila kama unaona kwamba unaweza kutengeneza upenyo wako wa kipekee sana, kwa kujitofautisha, basi unaweza kuendelea mbele na kufanya hivyo.
NNE, USIANZISHE BIASHARA NA KUJISHIKIZA KWENYE HIYO BIASHARA
Rafiki yangu, kunapaswa kuwa na utofauti kati yako wewe hapo na biashara. Na hapa ndipo watu wengi wamekuwa wanakosea sana.  Yaani yeye na biashara wanakuwa kitu kimoja. Pesa yake na pesa ya biashara havieleweki. Yeye anatoa pesa  hapa na kutumia kwa kisingizio kwamba biashara ni yake. Na wakati huo huo akitaka kufanya kufanya manunuzi ya biashara anatoa pesa humohumo.
Hili ni kosa kubwa. Kunapaswa kuwepo na mtari kati yako wewe na bishara. Wewe ujue ukomo wako na biashara iwe na sehemu yake ya kujtawala.  Naomba ufahamu kwamba wewe sio biashara. Ndio maana biashara tayari umeipa jina lake la tofauti kabisa. wewe hapo una mahitaji yako ya msingi ambayo kama utayapata basi utaendelea kuishi na ukiyakosa utakufa. Biashara pia ina mahitaji yake ya msingi, ambayo kama itayapata basi itaendelea kukua, na yakikosa basi itakufa.
Biashara ina mzunguko wake kama wewe ulivyo na mzunguko wa damu. Kwa hiyo  wewe ukijitofautisha na biashara itapendeza.
TANO, KUKOSA MAONO MAKUBWA,
Rafiki yangu, biashara inahitaji maono makubwa wakati inaanza. Yaani, unapaswa kujua kwamba unafanya hiyo biashara ukiwa unaelekea wapi. Na unataka kufika wapi. Kitu hiki hapa kitakusaidia sana hata kwa maamuzi unayofanya, maana yatakuwa ni maamuzi ya msingi na ambayo yanajulikana yanaenda wapi. Ila kama unafanya biashara tu kwa sababu unataka upate pesa kesho au kesho kutwa. Basi utajikuta kwamba unafanya makosa makubwa kwenye maamuzi, ambayo kwa muda mrefu yatakugharimu sana.
Rafiki yangu, hayo ndio makosa makubwa matano ambayo leo nilipenda uyafahamu na kuhakikisha kwamba umeyaepuka. Kiukweli kama utaepuka makosa haya utaweza kuanzisha biashara yenye mafanikio makubwa sana. Napenda sana usemi wa Robert Kiyosaki anayesema kwamba, biashara yenye mafikio inaanza kabla ya biashara yenyewe kabisa. hii ndio kusema kwamba kabla biashara haijaanza basi kwenye akili yako tayari unakuwa umetengeneza biashara yenye mafanikio makubwa sana.
Basi, basi rafiki yangu, nenda kaweke katika matendo haya ammbayo umejifunza hapa ili uweze kupata matokeo mazuri sana.
ASANTE SANA, TUKUTANE KWENYE JUKWAA LA WANAMFANIKIO.
NI MIMI ANAYEJALI MAFANIKIO YAKO,
GODIUS RWEYONGEZA
075584839, lakini pia napenda nikwambie kitu kimoja cha mwisho. Ebu jiunge na mfumo wetu wa kupokea makala kwenye barua pepe leo kwa kubonyeza HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X