JIFUNZE MATUMIZI SAHIHI YA NOTEBOOK: Ufanye Mwaka Huu Uwe Wa Mafanikio Kwa kutumia Maajabu Ya Notebook Tu


Habari siku hii njema sana rafiki yangu. Bila shaka siku hii njema sana ya leo umeianza vyema kabisa bila shida yoyote ile. Kama utakuwa makini, utagundua kwamba kuna kitu ambacho tayari kimeshatokea kwenye mwaka huu wa kipekee 2020. Unajua kitu hicho ni kitu gani? Kitu hiki sio kingine, bali ni kuwa, mwezi mmoja wa mwaka huu umeisha kabisa.
Huwezi amini yaani ule uliokuwa unaitwa mwaka mpya 2020, sasa hivi upya wake ushapotea. Na kama bado upya bado upo, basi upo ukingoni kabisa.
Binafsi najua wazi kwamba mwaka huu ulijiwekea malengo. Hivi nikuulize haya malengo uliyaandika au uliweka tu kwenye kichwa, basi.  Mimi sijui wewe umefanyaje, ila kama hujaandika malengo yako sehemu, basi naona wazi kwamba unafeli mapema.
Naomba nikuulize kitu kingine, hivi malengo yako hayo bado unayafanyia kazi? Kama huyafanyii kazi, sasa hapo ndio kabisaa. Mimi nichojua kuna watu ambao tayari wameshaanza kusahau malengo yao ya mwaka huu. Inawezekana sio wewe, ila watu hao wapo. Omba usiwe wewe hapo.
Binafsi siku hii ya leo, kuna kitu kimoja muhimu sana ambacho ningependa nikushirikishe ili kiweze kukuepusha kuupoteza mwaka 2020 hata chembe. Yaani sitaki uupoteze huu mwaka 2020, kwa sababu nakujali. Na kwa kuwa mimi nakujali, hivyo basi jitahidi sana kuepuka vitu hivi ndani ya mwaka huu ili uweze kuwa na mwaka wenye baraka kubwa sana.
Kitu hiki muhimu ambacho ningependa ukiepuke ndani ya mwaka huu ni kupita ndani ya mwaka bila notebook. Ujue hiki ni kitu kidogo sana ila kina maana kubwa. Notebook inakusaidia wewe hapo kujua maendeleo yako binafsi kwa kila siku inayopita. Tena kwa mwaka huu sitaki tu ununue notebook ilimradi umenunua. Nunua kabisa notebook yenye kalenda ya mwaka kuanzia januari mpaka disemba. Na kila siku hakikisha kwamba unarekodi kitu kwenye notebook yako hii mhimu. Yaani kila siku andika kitu kimoja ulichojifunza kwenye hii notebook yako, andika hatua ulizochukua na watu uliokutana nao au kuwasiliana  nao. Hivi ni vitu vidogo sana ila vyenye maana kubwa sana.
Pia kwenye hii notebook hakikisha kwamba unaandika kipato chako ambacho umeingiza kwa siku na matumizi uliyofanya kila siku. Ukiwa na notebook yako na ukawa unafuatilia maendeleo yako kila siku, kila wiki na kila mwezi inakuwa ni rahisi sana kujua ni wapi unakwama ili uweze kujirekebisha na kusongambele zaidi katika kufanya kazi zako za kila siku. Lakini kitu hiki kitaifanya kila siku yako inakuwa ni bora zaidi ya ile ambayo ilitangulia na kitu kingine ni kwamba kitafanya kila mwezi uliotanulia unakuwa ni mwezi wewe kuchukua somo kubwa ulilojifunza ndani huo mwezi hiyo kutorudia kosa ambalo ulifanya kwa mwezi uliopita. Narudia tena. Mwaka huu usikubali kuuishi bila ya kuwa na notebook hata kidogo.
Unaweza kuona kwamba kutoa kiasi cha pesa kizichozizdi elfu kumi kuwa ni kikubwa sana, ila kiuhalisia ni kwamba, kwa kutotoa hiki kiasi unajikuta kwamba unapoteza zaidi ya vile ambavyo wewe mwenyewe unategemea. Hivyo basi, hakikisha kwamba ndani ya mwaka huu 2020 unaamua kwa dhati kuwa na notebook. Hii siisemi kwa ajili ya manufaa yangu. Kama unaona hiki kitu ninachoandika hapa ni propaganda bora usiendelee kusoma, maana unapoteza muda wako. Ila kama unaamua kwa dhati kabisa kuhakikisha kwamba unakifanyia kazi, binafsi nina uhakika kwamba kitu hiki kinaenda kukusaidia sana kupiga hatua kubwa sana ndani ya mwaka huu 2020.
Sasa napenda nimalizie na vitu vya muhimu ambavyo utapaswa kufanya na notebook yako ndani ya mwaka huu
Kwanza kabisa andika jina la kitabu ambacho utasoma au utasikiliza ndani ya siku husika. Mwishoni mwa mwaka watu wengi huwa wanashirikisha ni vitabu vingapi wamesoma. Sasa kuna watu wengi huwa wanapata shida kujua ni vitabu vingapi walisoma kwa mwaka mzima ambao umepita just kwa sababu tu walikuwa hawaweki kumbukumbu. Kwa hiyo wanaanza kubahatisha na kubahatisha. Epuka kitu hiki kwa kuhakikisha kwamba  unaandika jina la kitabu ambacho unasoma kila siku kwenye notebook  yako. Just andika kichwa cha kitabu tu.
Pili, andika kitu kikubwa ambacho umejifunza kwenye siku husika. Kitu hiki unaweza kuwa umekisoma kwenye kitabu,pia kitu hiki unaweza kuwa umekutana nacho kwenye uhalilsia wa kila sikku katika majukumu yako au mambo ambayo unafanyia kazi.  Kiandike kitu hiki ni muhimu sana.
Tatu, andika pia mapato na matumizi yako kwa siku husika.
Nne, andika majina ya watu muhimu unaokutana nao ndani ya siku husika au kuongea nao ndani ya siku husika.kama umekutana na mtu kwa mara ya kwanza, andika jina lake na namba yake ya simu baada ya jina lake.
Tano,fanya tathimini kila unapofikia katikati ya mwezi wako na kila unapofikia mwishoni mwa mwezi. Jiulize hivi ni kweli bado nipo njia kuu ya kuelekea malengo yangu, au ndio kwanza napotea.
Sijui kama umeweza kunielewa kwa hivi vitu ambavyo nimekueleza. Kitu kimoja tu ambacho najua umechanganyikiwa hapa unaweza ukawa unajiuliza hivi vitu vyote nawezaje kuviweka kwenye notebook moja? Mbona nafasi kwenye notebook huwa ni ndotgo na haitoshi kwa ajili ya hivi vitu vyote? Jibu langu hapa ni moja tu, inawezekana. Kama hujui ni namna gani ya kufanya na umesoma mpaka hapa basi nitafute kwenye hii namba 0755848391 kwa kutumia wasapu tu, kisha uniambie tatizo lako, nitakuwa tayari kukusaidia kwa hicho kitu chako ambacho unakwama.
Sitaki uupoteze mwaka huu. Kama umeipoteza januari hakikisha kwamba huo unakuwa mwezi wako wa mwisho kupoteza. Hakuna muda wa kupoteza  tena ndani ya 2020. Jikwamue wewe mwenyewe kuanzia sasa hivi. Kanunue notebook leo, na ufanye yale niliyokushauri. Maajabu yake utakutana nayo huko mbeleni.
Ni mimi anayejali mafanikio yako
Godius Rweyongeza.
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X