Kama Sio Wewe Nani? Kama Sasa Lini? INAWEZEKANA


Rafiki yangu hongera sana kwa nafasi ya siku hii ya kipekee sana. Siku ya leo napenda nikwambie kwamba inawezekana, ndio kama una lengo ambalo unataka kulifanyia kazi katika maisha yako unapaswa kufahamu  kwamba inawezekana kulifanikisha lengo hili hapa.
Kama kuna ndoto ambayo unayo maishani mwako basi fahamu kwamba inawezekana. Watu unawaona sasa hivi wakiwa wamefanya makubwa kwenye hii dunia ni walikuwa ni watu wa kawaida kama wewe hapo. Sasa kuna kitu ambacho kiliwatofautisha watu hawa na kuwafanya watu hawa waweze  kusongambele na kufanya makubwa zaidi maishani.
Kitu hiki ni kuwa na malengo. Walikuwa na malengo ambayo waliyafanyia kazi. Ukiwa na lengo ambalo unalifanyia na kazi na ukaweka nguvu na akili yako hapo, huwezi kushindwa kulifikia. Tatizo la watu walio wengi ni kwamba wanaweka malengo makubwa ila hawayafanyii kazi. Au hawaweki nguvu zao kwenye kufanyia kazi hayo malengo. Hakikisha kwamba unajiepusha na hicho kitu. Jitoe kuhakikisha kwamba unatimiza na kufanikisha lengo lako kwa namna yoyote ile. 
Ujue  Brian Tracy amewahi kusema kwamba, ukiwa na malengo unayafanyia kazi na hayo malengo yanakuwa yanafanya kazi kuhakikisha kwamba yanakuelekea wewe hapo. Mwisho wa siku wewe  pamoja na malengo yako mnafikia hatua ambapo mnakutana.
Sasa swali langu kwako, ni je una malengo gani mwezi huu? Je, una malaengo gani kwa mwaka huu 2020.
Chukua hatua uweke malengo leo hii na uanze kuyafanyia kazi moja kwa moja bila kuchelewa. nakutakia kila la kheri.
Godius Rweyongeza.


One response to “Kama Sio Wewe Nani? Kama Sasa Lini? INAWEZEKANA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X