Moja ya kanuni za fizikia ni hii kanuni inayosema kwamba, to every action there is equal and opposite reaction. Ikimaanisha kwa kila kitu ambacho unafanya kuna kuwa na nguvu ya aina hiyo hiyo ambao inakujwa kwako.
Kwa hiyo ukifanya kazi kwa bidii kubwa ili uweze kupata matokeo makubwa, mwisho wa siku matokeo makubwa yataanza kuja kuelekea kwako na mtakutana katikati.
Hii ndio kusema kwa malengo yako uliyonayo. Matokeo ya malengo ambayo unayapata kwenye maisha yanategemea na kiwango cha juhudi ambacho unaweka. Kama unaweka juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba unatimiza malengo yako. Malengo yako yenywe yatakuja kwako kwa kasi kubwa na mtakutana sehemu.
Lakini kama unayakimbia malengo na unaogopa kuyafanyia kazi, basi badala yake malengo yako hayo yatakukukimbia na wewe na malengo hamtakuja kukutana kamwe. Kwa hiyo basi kuanzia siku hii ya leo, anza kuweka juhudi kuelekea malengo yako kila iitwayo leo. Hakikisha kwamba haulazi damu. Weka juhudi mara nyingi zaidi kiasi kwamba malengo nayo yaanze kukusogelea hapo ulipo. Nikutakie kila la kheri katika kile ambacho unafanya
Ni mimi ninayejali mafanikio yako
Godius Rweyongeza