UNATAKA KULA MEMA YA NCHI, BASI SOMA HAPA


Rafiki yangu, habari ya jioni. Leo nimeona nikwambie aina tatu za ujuzi ambao ukiwa nao wewe hapo utakula mema ya dunia hii.
Nadhani umewahi kusikia watu wanaosemekana kula mema ya nchi. Leo hii kuna vitu vitatu ambavyo ni uhakika ukiwa navyo basi utakuwa njiani kula mema ya nchi.

Kwanza, ni ujuzi wa kuandika andiko lililotukuka.

Hiki ni kitu ambacho nimekuwa nashauri mtu yeyote yule ambaye anaishi hapa duniani aweze kujifunza. Kwa chochote kile ambacho unafanya basi unahitaji kujifunza kuandika. Ila sio tu kuandika. KUANDIKA ANDIKO, LILILOTUKUKA.

Andiko ambalo mtu akisoma, atataka asome tena na tena.
kitu hiki kitakusaidia katika kuuza, katika kushawishi watu wanunue, wawekeze, au katika kazi yako yoyote n.k.

kwahiyo weka utaratibu wa kujifunza ujuzi huu wa kipekee sana.

Pili ni UJUZI WA KUUZA

Huu ni ujuzi mwingine muhimu sana. Ujue kwa namna moja au nyingine katika maisha utalazikika kuuza. ukisimama mbele ya watu kuongea ujue unauza. ukiongea na mtu unakuwa unafanya mauzo, ukitaka mtu akubali falsafa au hoja yako basi ujue kwamba utakuwa unafanya mauzo, ukitaka kumpata mwenza lazima  utatakiwa kufanya mauzo, na hata kama unahubiri bado ni uuzaji.

kwa hiyo jifunze namna bora ya kuuza ambayo itawafanya watu wanunue unachouza. Jua saikolijia ya watu ili ikusaidie katika aina ya mauzo unayofanya.

Soma Zaidi: Usitafute Kiki Kwa Kutengeneza Matatizo

3. Tatu ni KUNENA

Huu ni ujuzi wa tatu muhimu sana. Kunena au kama kunavyofahamika kwa kiingereza ni public speaking.  Hiki ni kitu muhimu pia.
kila siku tunakutana na watu na tukiwa na watu hawa tunaongea, tunawasilisha na kujadili mada, tunacheka na kufurahi.

lakini unahitaji kujifunza kunena. Na kunena ni zaidi ya kuongea. Najua utauliza sasa kunena ni nini? Kwa haraka tu naweza kusema KUNENA ni KUONGEA NA WATU WAKASILIZA.

Sasa kuongea na watu wakusikilize wewe ni kazi. Na sio kazi ndogo.
Nadhani imewahi kukutokea  unaanza kumsikiliza mtu ila unagundua kuwa hana pointi za maana. Yaani amesimama mbele yako na wewe unaona wazi kwamba hakuna kitu cha maana anafanya.

Omba isikutokee wewe. Na namna nzuri ya kuomba ni kuanza kufanya mazoezi leo.
Rafiki, hizo ndizo aina tatu za ujuzi ambazo nimeona wazi nikwambie jioni ya leo.

Nadhani kama utakuwa umefuatilia. Aina hizi tatu zinaendana sana. Yaani zote zinaelekea kuwa na lengo moja tu. Ukiwa na aina tatu za ujuzi, ni wazi kwamba utakuwa mtu anayetafutwa sana kwenye hii dunia. Au kiufupi ni kwamba utakula mema ya nchi.

USHAURI WANGU: Chagua aina moja ya ujuzi ambao unaweza kuanza kufanyia kazi leo.

Usianze na kila ujuzi. Anza na ujuzi mmoja, ufikishe kwenye viwango vikubwa. Kisha kuza ujuzi mwingine. Mwisho wa siku utajikuta umeweza kujenga kila ujuzi.

SOMA ZAIDI: MAMBO MATATU AMBAYO VIJANA WA KITANZANIA WANAKOSEA ILA WANAYAFANYA KUWA HALALI

Rafiki yangu binafsi nakupenda sana na nikutakie usiku mwema.
Kila la Kheri.

Ni mimi anayejali mafanikio yako
GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X