Vitu Saba Vya Kujifunza Na Kuchukua Hatua Kutoka Kwenye Wimbo Wa Ben Paul Wa JIKUBALI


Moja ya wimbo ambao huwa napenda kuusikiliza mara kwa mara ni wa mwanamziki Ben Paul unaoitwa JIKUBALI. Huwa napenda kuusikiliza mara kwa mara kwa sababu kuna mafunzo muhimu ambayo naona na wewe nikushirikishe baadhi ya hayo masomo siku ya leo.
1. UNAWEZA
Ben Paul anaanza kwa kusema kwamba,
unaweza kuwa doctor,
unaweza kuwa star,
 


Ni ukweli usiopingika kwamba chochote kile ambacho utaamua kufikia maishani mwako, unaweza. Kila kitu kinaanza na maamuzi.
kwa kutumia hicho kichwa chako. Kama utaiambia akili yako kwamba huwezi, jua kabisa kwamba hautaweza.Ila ukisema unaweza, utaweza tu.
Napenda sana maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu cha THINK AND GROW RICH sura ya tatu.
mwandishi anasema.
Kama unafikiria umepigwa, umepigwa
Kama unafikiri umeshindwa, umeshindwa
Kama unafikiri huwezi, huwezi
Kama unataka kushinda lakini unafikiri huwezi, karbia huwezi.
Kama unafikiri utapoteza, umepotea
Kwa sababu katika dunia ushindi unaanza na msukumo wa ndani ya mtu,
Hiyo inaitwa hali ya akili.(state of mind).
Kama unafikiri umepitwa na wakati, umepitwa
Inabidi ufikiri mbali
Inabdi ujiamini mwenyewe kabla ya kushinda tuzo.
Vita vya maisha hashindi mtu mweye nguvu au mwenye mbio za haraka
Vita vya maisha anashinda mtu ANAYEFIKIRI ANAWEZA.
kwa hiyo na mimi napenda kukwambia  kwba UNAWEZA.
Sidhani kama mimi nina kitu cha zaidi cha kuongeza hapa tofauti na kusema tu kwamba, badili fikra zako sasa hivi na uanze kujiona kwamba unaweza. Kumbuka kwamba FIKRA ZAKO NDIZO HULETA HISIA UNAZOKUWA NAZONA HISIA NDIZO HUSABABISHA MATENDO AMBAYO UNACHUKUA, HUKU MATENDO YALILETA MATOKEO.

Kwa hiyo ukitaka kubadili matokeo unayopata sasa hivi, basi anza kubadili hicho kitu ambacho unaweka kwenye akili yako sasa hivi. Anza kuona uwezekano. Ujue unapoiweka akili yako katika kutafuta uwezekano ujue kwamba lazima tu itatafuta muda wote kuhakikisha kwamba inatafuta suluhisho.
Soma zaidi; Kitabu Muhimu Unachopaswa Kusoma Kuhusu Ubunifu
2. KIPAJI CHAKO NDIO MTAJI WAKO WA KWANZA
Ben Paul anaendelea kwenye wimbo wake kwa kusema kwamba;
kipaji mali yako,
 


Nadhani moja ya vitu ambavyo vimekuwa havipewi kipaumbele sana shuleni na hata nyumbani ni kipaji.  Lakini ukweli ni kwamba wewe unaweza kunoa kipaji chako kuamzia hapo hapo ulipo.
kwenye kitabu changu cha  JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO nimeshauri kwa mtu yeyote kutenga dakika 30 tu kila siku kufanyia kazi kipaji chake.  ukiangalia kwa jicho la kipekee utaona kwamba dakika 30 kwa siku sio nyingi. Maana kwa siku moja tu una dakika 1440. Ukitoa dakika 30 unabaki na dakika 1440. Sasa unakwama kwa mfano unaweza kushindwa kupata dakika 30 kila siku za kufanyia kazi lengo lako?
3. ELIMU NGAO YAKO, NGAO YAKO

Ben Paul anaendelea kuimba kwa kusema ELIMU NGAO YAKO…
Kama ulikuwa hujui, kamusi ya kiswahili sanifu inasema  NGAO NI KINGA. kwa hiyo ninaweza kusema kwamba elimu yako ndio kinga yako.
Na hapa ninaposema elimu simaanishi tu elimu ya chuoni. Kuna aina nne za elimu
ya kwanza ni ile ya kawaida ya nyumbani ambapo unafundishwa vitu vya hapa na pale.
Ya pili ni ile ya shuleni ambayo unafundiswa kusoma na kuandika na kuhesabu. aina hii ya elimu inapimwa kwa kiwango ufaulu. Yaani A au B unazopata.
Ya tatu ni elimu ya pesa (hii haifundishwi shuleni wala nyumbani) hii unajifunza kitaa. aina hii ya elimu haipimwi kwa kiwango cha elimu ulichonacho.  Na wala haipimwi kwa A au B ulizopata  Aina hii ya elimu inapimwa kwa pesa unazoingiza au pesa unazopoteza.
kwa leo sitaingia ndani zaidi kuhusu aina hizi za elimu, nataka tu uzijue.  Na kamwe usije ukasema kwamba mimi siwezi kufanikiwa maishani kwa sababu tu sina elimu ya shule au chuoni. Wakati hiyo  ni mojawapo kati ya hizo elimu nyingine ambazo unaweza kuwa nazo.
Aina ya nne ni elimu, ni elimu ya maendeleo binafsi. Wakati huleni unafundishwa kusoma na kuandika pamoja na kuhesabu, lakini maisha yanahitaji uandike, usome na kuhesabu. Na hapa ndipo elimu hii inaingilia katikati.
Wakati mwalimu anakufundisha kusoma, lakini mwalimu huyohuyo anapokuja kwenye maisha ya kawaida hakuchagulii kitabu cha kusoma.
Elimu hii ya maendeleo binafsi ndio itakuwezesha wewe kutumia vipaji vyako na uwezo wako ulionao.
inawezekana wewe una kitabu hapo ambacho ningekuwa nasoma sasa hivi ila hujakiandika kwa sababu hupati elimu hii.
Inawezekana wewe una wimbo wa kuniburudisha ila hujafanya hivyo kwa sababu hujiendelezi.
inawezekana wewe una ujuzi mkubwa wa uongozi ila kwa sababu hupati elimu hii basi uongozi wako ndio hivyo hata hauutumii. Kiukweli kama utakufa na vitu hvivi, ujue kwamba utakuwa umefanya kosa kubwa.
Naweza kuandika zaidi hapa. ila kwa leo napenda ukasoma makala yenye kichwa cha Kinachokukwaisha Ni Uoga HAPA
Napenda kumalizia kipengele hiki cha Elimu kwa kusema kwamba mjinga wa karne ya 21 sio yule ambaye hajui kusoma na kuandika, bali mjinga wa karne ya 21 ni yule anayejua kusoma na kuandika ila hasomi. kiufupi kama unajua kusoma ila hujiendelezi kwa kusoma vitabu mbalimbali basi hauna tofauti kabisa na ambaye hajaenda shule.
kumbuka elimu ni ngao yako. Na elimu itakuwa ngao yako kama kile unachojifunza utakiweka katika matendo.

Wasomi wengi wana elimu nzuri na kubwa lakini hawaitumii kama ngao. Wao wenyewe haiwasaidii chochote. Ndio maana wengi wanakimbilia kuajiriwa.  Ila ukiwa na elimu ya kujiendeleza binafsi, basi watu watakutafuta tu kwa sababu utakuwa mtu wa viwango vingine.
Angalia video hii hapa inayozungumzia Maeneo mawili ya kupata shahada mtandaoni bure kabisa HAPA
4. USIISHIE NJIANI
Tuendelee na wimbo wa Ben Paul. Hapa tunaaenda moja kwa moja mpaka kwenye mstari ambao anaimba hivi: “usiache jambo kati kwenye maisha yako
 


Hapa ndipo vijana wengi wa Tanzania wanakwama. Kuna vijana wengi wa kitanzania wana mawazo mengi mazuri ya kujenga kweli kweli. Lakini tatizo lao ni kuishia njiani. Wanagusa gusa tu.  au kwa msemo maarufu ambao unatumika kwamba wanajaribu. Yaani unakuta mtu ana kipaji kizuri cha kuimba, ukiwambia kwamba aiseeh unaweza kuimba. Utasikia anakwambia kwamba najaribu jaribu tu.
Watu wengi ambao huwa wanajaribu jaribu ndio watu ambao huwa wanaishia njiani. Kwa sababu huwa wanaanza kufanya kitu mguu mmoja ukiwa ndani na mwingine ukiwa nje. Yaani wanakuwa wanajua kama wataanza kufanya kitu hiki na kikawa hakijafanikiwa basi watarudi huko huko walipokuwa nyuma.
Vijana wa kitanzania mnahitaji kujitoa. Au kiufupi naweza kusema kwamba KUCHOMA MELI MOTO.  
Soma zaidi: TATIZO HUTAKI KUCHOMA MELI MOTO
Kwa kumalizia kipengele hiki hapa, nipende tu kukwambia kwamba, ukianza kitu kimalize. Usiishie njiani. Kuishia njiani kunafanywa na watu ambao hawana mwelekeo kwenye maisha. Kama kweli unataka kufanya mambo ya kipekee hapa duniani basi hakikisha kwamba kila unachomua kuanya basi unakikamilisha mpaka mwisho hata kama vinatokea vikwazo. Ndio maana Ben Paul anasema kwamba vikwazo lazima nawe usirudi nyuma.
5. WAKATI WAKO NI LEO
Tuendelee na wimbo wa wimbo wa Ben Paul.
Na hapa tumefika kwenye mstari ambapo Ben anasema kwamba,
Mi nakuasa, its your time
Huwezi kuwa chini, you’ve got something special.

 


Ujue kuna watu ambao wana vitu vya kipekee ambao haawajahi kuambiwa kwamba wanaweza. Hawajawahi kuambiwa kwamba una kitu cha kipekee. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwenye mazingira tumezungukwa na watu wengi ambao hi hasi.
Ukijitahidi kufanya kitu chochote kile wanakwambia kwamba huwezi kufanya hicho kitu. Ukijitahidi kusonga mbele kidogo basi unaambia kwamba hicho kitu hakiwezekani. Na maneno mengine mengi.
Kuna siku nilikuwa nasoma hadithi ya A BOY WHO HARNESSED THE WIND. Kwenye kitabu hiki mwandishi ambaye ni Kamkwamba akawa anasema kwamba aliweza kutengeneza umeme nchini kwao ila hakuwahi kushangiliwa wala kupigiwa makofi na mtu yeyote, isipokuwa watu waliokuwa wanataka kumuua kwa sababu eti kwa kutengeneza mtambo wa umeme amezuia mvua. Lakini kijana huyo alikuja kushangiliwa kwa kishindo sana katika nchi ya ugeni.
Na hiki ndicho kinatokea kwa vijana walio wengi na wanaoanza. Kuna watu wengi ambao wanakukatisha tamaa kwenye hicho unachofanya.
Kwa nini watu wanakukatisha tamaa? Watu wanakukatisha tamaa kwa sababu wao walishakujengea mazingira ambayo wanaona kwamba unafaa na hivyo hupaswi kwenda zaidi ya hapo. Yaani ni kama vile watu walishakuweka kwenye kopo. Kwa hiyo sasa unapoanza kufanya vitu vya tofauti na vile watu walivyokuwa wanategemea basi kila mmoja ataanza kusema maneno yake, kila mmoja ataanza kuongea na wengiine wataona kama umekeunga.
Sasa nipende kukwambia kwamba usikubali kuwekwa kwenye kopo.
Wakati ndio leo
Kutimiza malengo
Nakusihi uanze sasa
Jishughulishe utapata.
Kama anavyosema Ben Paul

6. USIWE MCHOYO
Ukitaka kufanya mambo ya tofauti kwenye hii dunia haupaswi kuwa mchoyo hata kidogo. Leo hii najaribu kufikiria kama Steve Jobs anegkuwa mchoyo wa kutengeneza hizi simu janja za kupangusa inawezekana wewe na mimi tusingefahamiana na hata hiki unachokisoma sidhani kama kingekufikia haraka kiasi hiki. Ila aliachana na uchoyo na kutengeneza kitu kizuri.
Ebu fikiria pia kama huyu anayemiliki kiwanda cha nguo unazovaa angeamua kuacha kutengeneza nguo, kwa sababu ya uchoyo, bila shaka lolote lile usingekuwa umevaa hizo nguo. Au kiufupi ungekuwa uchi.
Sasa na wewe uache uchoyo. Badala yake ongonzwa na upendo. Na hapa Ben Paula anasema hivi
Tanzania ni yako, penda watu wako.
Kuwa mfano bora kwenye jamii yako.
Ujue watu wanaopenda jamii ndio wanafanya vitu vya kuisaidia jamii. Ni kwa sababu ya upendo ndio maana unaona watu wanaanzisha biashara. Ni kwa sababu ya upendo ndio maana unaona watanzania wanawekeza (japo wengi hawajui hili somo la kuwekeza)
Ni kwa sababu ndio maana Ben Paul mwenyewe aliimba wimbo huu na kutumia kipaji chake.
Sasa wewe upendo wako  unatumia kufanya nini? ebu na basi na wewe amua kutumia walau kipaji chako.
Ebu na wewe amua basi kutumia uwezo wako wa uongozi. ebu na wewe amua basi kutumia kuchora hiyo michoro ambayo unayo kwenye kichwa chako.
Ebu basi geuza hicho kipaji cha kubishana juu ya mpira ukitumie kwa manufaa zaidi.
Kiukweli una vitu vizuri ila kama hutasukumwa na upendo basi inawezekana hivyo vitu tusivione kwa sababu ya kukosa upendo. Nakusihi uongozwe na upendo ili uweze kutumia kile ulichonacho kufanya makkubwa zaidi.
7. FANYA KAZI KWA BIDII, HAKUNA NJIA RAHISI YA KUFANIKIWA

Ni kweli mpaka hapa nimezungumzia mengi kwenye makala hii hapa. ila siwezi kuacha kuzungumzia suala zima la kufanya kazi kwa bidii. Kuna watu wengi utakuta kwamba wanakwambia wanataka kazi ambayo wataingia ofisini tu na kusaini. Kisha kuondoka. Kweli! Kiukweli kama unataka kufanikiwa basi huna budi kuhakikisha kwamba unafanya kazi kwa bidii sana.
Ndio maana Ben Paula anasema hivi,
 inawezekana if  you work hard in it.
Sio kwa sababu nimesema utumia kipaji chako basi unafanya hivyo mara moja tu.
Au sio kwa sababu nimesema ujifunze na kuongeza maarifa basi unafanya hivyo mara moja tu.
Inawezekana if you work hard on it,
Unahitaji kuchapa kazi haswa, siku zote nyuma ya ushindi huwa kuna kazi kubwa ambazo huwa zinawekwa kabla ya kupata matokeo makubwa .
Kuna mengi sana ya kujifunza ila kwa leo naishia hapahapa.
Mpaka wakati mwingine. KWA HERI ni mimi anayejali mafanikio yako
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA
Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X