Ebu Jionee Jinsi Tone La Wino Linavyoweza Kubadili maisha Yako


Moja kati ya usemi maarufu sana wa Lord Bryon ni ule aliosema kuwa tone la wino, linaweza kuwafnya mamilioni ya watu kufikiri.

Na hii ni kweli kwa asilimia zote. Ukitaka kunielewa kwenye hili napenda nikupe mfano wa karatasi nyeupe ambayo imewekwa nukta moja tu katikati. ukiwaita watu wakuambie wanaona nini kwenye hiyo karatasi wapo watakaokwambia, 
1. naona nukta.
2. huku wengine watakuambia naona karatasi nyeupe na
3. wengine watakuambia naona karatasi nyeupe pamoja na nukta.
Vivyo  sentensi kidogo tu kwenye kitabu inaweza kukufanya ubadili maisha yako moja kwa moja.
Ukisikia mtu anasema kitabu fulani kilibadili maisha yangu, pengine huwa sio kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho huwa kimebadili maisha ya huyo mtu, lakini sentensi au sura fulani kwenye kitabu.
au ukurasa mmoja tu kwenye kitabu.
ndio maana leo nikaona nikwamhie ukweli huu, Tone la wino linaweza kufanya mamilioni ya watu kufikiri.
Tone la wino linaweza kubadili maisha yako.
Tone la wino linaweza kukufanya uanze kuchukua hatua mpya.
tone la wino linaweza kukufanya uanze kutumia kipaji chako
Tone la wino linaweza kuhuisha mahusiano yako.
Je, leo unaenda kusoma kitabu gani?
kama bado hujasoma kitabu cha  KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI nakuona unavyozidi kujinyinyima uhondo wa kubadilisha maisha yako mapema. Kitabu hiki ni elfu 10 tu.
Tuwasiliane leo ili uweze kukipata.
nitumie ujumbe hapa
https://wa.me/255755848391?text=Godius%20Rweyongeza
.
Chukua hatua leo, ili uweze kukipata kitabu hiki hapa kwa elfu 10 tu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X