Hivi Ndivyo Unaweza Kufanya Makubwa Mpaka Kumzidi Mwenye Kipaji


Rafiki yangu kuna vitu sita ambavyo unaweza kuvitumia kumpita mwenye kipaji na wewe ukaweza kufanya makubwa hata zaidi ya yeye.

Kitu cha kwanza ni kuchagua eneo ambalo unaweza kuwekeza nguvu zako.

pili ni kuamua kuwa hapa kufa na kupona mpaka kieleweke. Siachi kufanya hiki kitu mpaka nipate mafanikio.

Tatu, ni kufanya kazi kwa bidii. Ukifanya kazi kwa bidii kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu ni LAZIMA utampita mwenye kipaji ambayebhafanyi kazi kwa bidii.

Nne, Kujifunza na kuongeza maarifa zaidi kila mara. Hakikisha kwamba unakuwa updated kwa kuwa na maarifa mbali mbali kutoka kwenye vitabu.
kama hujui vitabu vinaweza kukusaidia nini maishani bonyeza hapa kupata kitabu hiki bure. Kitakufundisha mengi.
https://blogspot.us14.list-manage.com/subscribe?u=35d404174ee6b730531b8d920&id=7ff0bfcfca

Tano, usikubali kukatishwa tamaa na mtu mmoja. Kuna watu ni wa ajabu kweli! anaweza kuwa amafanya kazi yake vizuri, ila akatokea mtu mmoja akamwambia huwezi akawa ndio amekata tamaa kabisa na kuacha. Yaani hata akasahau watu wengine ambao wamekuwa wanamtia moyo siku zote.

Sita, fanya vitu vinavyoonekana kwa watu (onyesha kazi zako kwa watu). Mtu anaweza kuwa na kipaji ila hafanyi vitu vinavyoonekana kwa watu. Ndio anajua kuimba lakini nyimbo zake hatuzioni, lakiji za kwako  tunaziona, sasa unadhani nani tutampa kipaumbele? Ndio anajua kucheza lakini hachezi, sasa unadhani tutasema anajua? Hivyo weka utaratibu wa kuonesha kazi zako.

Saba, jua nguvu zako ziko wapi zaidi.  Usipoteze muda wako kulisha udhaifu wako badala ya kuwekeza nguvu zako eneo ambalo unaweza vizuri.

Hivyo ndivyo unaweza kumpita mwenye kipaji na kung’aa vizuri kwenye eneo lako.

Rafiki yangu, kuna kitabu cha bure kabisa hapa. Jiandikishe hapa chini kukipata.
http://shorturl.at/qryAN


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X