Hivi Ndivyo Unaweza Kupata Kitu Cha Kuandika




Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Bila shaka siku ya leo imeanza vyema kabisa rafiki yangu. Siku ya leo, nataka nikwambie kitu kimoja muhimu sana  kuhusu uandishi.

Ujue rafiki yangu moja ya  swali ambalo watu huwa wanauliza mara nyingi sana linapokuja suala la unandishi ni swali la je, mimi ninandike kitu gani.
Ukweli ni kwamba kama wewe umeweza kuvuka umri wa miaka 10, ni wazi kwamba huezi kukosa kitu cha kuandika. Na ni wazi kwamba wewe unayesoma hapa lazima tu, utakuwa una miaka zaidi ya 10.
Kwa hiyo kuna mengi ambayo unaweza kuandika. Unaweza kuandika kuhusu, juu ya aina ya chakula mlichokuwa umnakula kipindi  cha utotoni, unaweza kuandika juu ya aina ya likizo za utotoni, jinsi mlivyokuwa mnasherehekea siku kuu. Yule mjomba wako au shangazi ambaye ulikuwa humpendi aje nyumbani kwenu hata siku m oja. Unaweza kuandika juu ya chakula ambacho mlikuwa mnakula, unaaweza kuandika juu ya maisha ya shule ya msingi, mwalimu wako ambaye ulikuwa unampenda kipindi uko shule ya msingi na mambo mengineyo mengi sana.
Rafiki yangu, sio lazima uandike historia ya maisha yako. Bali unaweza kuandika, masomo ambayo umeweza kujifunza kutokana na hivyo vitu ambavyo umepitia wewe kama mtoto.
Rafiki yangu, kama umekuwa unakwamba linapokuja suala zima la kuandika malengo na kuyafanyia kazi, basi rafiki yangu, ndio sasa nimeona nikupe mwanga wa wapi unaweza kuanzia wewe kama mwandishi.
Ni kwa siku sasa nina programu ya uandishi, PROGRAMUHII INAITWA UANDSHI 101. Kwenye programu hii ninafunidisha kila kitu ambacho unahitaji kujua kuhusua kuandika, na programu hii ni kwa ajili ya yule ambaye kabisa angependa kuanza kuandika lakini hajui ni kitu gani ambacho anapaswa kuandika. Au yule ambaye ameanza kuandika lakini akawa amefika eneo fulani akawa amekwama na sasa angependa kupata maarifa ya kumfanya azidi kusongambele.
Unaweza kujiunga na programu hii kwa kubonyeza HAPA



Ni mimi anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X