Hivi Ndivyo Unaweza Kusoma Vitabu Vingi Kwa Muda Mchache


Siku si nyingi sana niliandika makala iliyokuwa inaeleza jinsi ambavyo nimeweza kusoma vitabu tisa kwa kipindi cha wiki moja na nusu.  Moja ya swali ambalo watu waliniuliza ni swali la je, nimewezaje kusoma vitabu vy te hivyo kwa kipindi kifupi hivyo?  Inawezekana wewe pia ukawa unajiuliza swali hili hapa. hivi inawezekanaje kusoma vitabu vingi kwa wakati mmoja  kiasi hicho wakati hata nashindwa kusoma kitabu kimoja kwa wiki? Siku ya leo naenda kukushirikisha njia kuu tatu za kusoma vitabu vingi zaidi.
KWANZA.  Ni kufanya kitu kimoja kwa wakati.
Iko hivi. Muda ule ambao unaamua kuanza kusoma vitabu unapaswa kweli na kuamua kuondoa kila aina ya usumbufu ambao unaweza kujitokeza ili uweke nguvu, akili, muda wako na kila kitu kwenye kusoma kitabu tu. ukigawa nguvu zako utashangaa muda unasogea wakati ukiwa husogei.
Hivyo hatua ya kwanza amua muda wa kusoma ni wa kusoma na wala sio kufanya vitu vinine.
PILI ; KWA VITABU VYA NAKALA NGUMU ( hard copy)

Usomaji wa vitabu vya nakala ngumu ni mzuri sana. unapochukua nakala ngumu soma kwa kupitisha kidole kwenye sentensi unayokuwa unasoma kwa wakati husika. Kitu hiki kitakufanya wewe muda wote uwe unafuata mwendo wa kidole. Kadri unavyooongeza mwendo wa kidole ndivyo na wendo wako wa kusoma unapaswa kuongezeka.  Hii njia inachosha mwanzoni haswa unapokuwa unaongeza mwendo tofauti na vile ulivyozoea, ila inalipa zaidi kwa muda mrefu maana inafikia hatua akili inazoea na kuanza kwenda kwa kasi hiyo.
TATU, UNGANISHA KITABU KILICHOSOMWA (AUDIOBOOK) pamoja na NAKALA  TETE (soft copy) au NAKALA NGUMU.

Kwa njia  hii unaaweza kusikiliza kitabu kilichosomwa wakati ukiwa unafuatilia maandishi kwenye nakala tete au  nakala ngumu. Pale ambapo unakutana na kitu ambacho unapaswa kuandika kwenye kusoma kwako, utapaswa kusimamisha AUDIOBOOK kisha utaandika kitu hicho kisha utaiendeleza audiobook yako.
Vitabu vingi ambavyo vimesomwa vinaanzia saa 1 na vitabu vichache vinazidi saa 10.
Kwa mfano mimi nilisoma kitabu cha The Richest Man In Babylon kwa kutumia mfumo huu. Na nilitumia saa nne tu. lakini jiulize wewe umekuwa unatumia wiki ngapi kusoma kitabu hicho au cha aina hiyo hiyo.
NNE, JIWEKEE LENGO LA KUSOMA UKURASA MMOJA KWA DAKIKA MOJA

Hili ni njia nyingine ambayo nimekuwa nikiitumia kuanzia mwaka jana mwishoni. Nikichukua kitabu naweka lengo la kusoma kurasa 20 ndani ya dakika 20 au zikipungua zaidi zisiwe chini ya 16. Ili kutimiza lengo hili ninapaswa kusoma ukurasa mmoja kwa dakika moja. ni lengo gumu kidog hasa kwa mwanzoni ila kadri akili inavyozoea mambo yanakuwa ni safi kabisa. wewe pia unaweza kufanyia kazi lengo hili hapa. ukiona halikufai unaachana nalo au unaliboresha.
KUPATA AUDIOBOOKS BONYEZA HAPA
TANO, SOMA VITABU VIWILI AU VITATU KWA WAKATI MMOJA

Kuna wakati ambapo unaweza kuunganisha vitabu viwili. Sio kwamba unavisoma muda uleule. Hapana. Kwa siku moja unasoma vitabu viwili au vitatu. Kwa mfano ukiamka asubuhi unasoma kitabu A. machana unasoma kitabu B na usiku unarudia kusoma kitaabu A au unasoma kitabu C.
Kwa mfano sasa hivi nipo nasoma vitabu viwili ila kwa nyakati tofauti. Ninapokuwa nyumbani ninaposoma kitabu cha Bob Proctor kinachoitwa ITS NOT ABOUT THE MONEY. Ila nikiwa safarini, kwenye daladala, au sehemu nimetulia ambapo sio nyumbani nasoma kitabu cha STEVE JOBS ambacho kimeandikwa na Walter Isaacson. Kwa jinsi hii najikuta vitabu viwili vyote vinaenda sambamba. Kwa hiyo hata kwenye kuvimaliza utakuta kwamba vinapishana labda siku moja au mbili tu.
Kuna vitabu vingine huwa vina mada muda fupi lakini zenye nondo zinazoeleweka. Hivyo unaweza kukuta umesoma hata mada mbili mpaka tatu au zaidi kwa muda mfupi. Mfano wa kitabu cha aina hii ni WHO WILL CRY WHEN YOU DIE au THE GREATNESS GUIDE  vyote vimeandikwa na Robin Sharma.
Rafiki yangu nimeona nikujuze hiki kitu. Kwa maoni, maswali na mengineyo tafadhali tuma ujumbe kwenda godiusrweyongeza1@gmail.com

Ni mimi anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X