Kama Huwezi Kuwa Kichaa Wa Ndoto Yako, Basi Isahau


Moja ya kitu kinachowafanya watu wengi washindwe kutimiza ndoto zao ni kwa sababu tu ya hawataki kuonekana vichaa miongoni mwa watu. kwa nini?

Kwa sababu siku zote ndoto huwa ni kubwa kiasi kwamba mtu akianza kuisema mbele za watu basi ataonekana kama kichaa vile. Una ndoto yako kubwa kwa jamii unakuwa kama muasi. Maana jamii yenyewe inakuwa tayari imeshakuamulia aina ya maisha ambayo unapaswa kuishi. Na kwa kuwa mtu anakuwa hapendi kuonekana kichaa basi kwake inakuwa ni bora tu kubaki alivyo sasa hivi. Anachagua #KutoTimizandotoZake. 
Leo nataka nikwambie kwamba kama unataka kutimiza ndoto zako basi unapaswa kuwa KICHAA. Ndio kama wewe hauna ukichaa wa kutosha basi sahau ndoto zako. 
Na historia nzima inaonesha watu waliokuwa vichaa tu ndio walitimiza ndoto zao. Usishangae ukweli ndio huo. Ebu ngoja nikupe orodha ya watu wachache hapa chini na wewe uniambie nani hakuwahi kuitwa kichaa wakati anatimiza ndoto zake.
👉Albert Eintein
👉Bob Dylan
👉Martin Luther King Jr
👉Richard Branson
👉John Lennon
👉R. Buckminster
👉Thomas Edison
👉Mohammad Ali
👉Ted Turner
👉Mahatma Callas
👉Mahatma Gandhi
👉Amelia Earhart
👉Alfred Hitchock
👉Martha Graham
👉Jim Henson
👉Frank Lioyd Wright
👉Pablo Picasso
Umeona nani ambaye hakuwahi kuonekana kama kichaa? Ni nani?
Sasa kama wewe unasubiri kila mtu aanze kuonekana kwamba anakupenda ndio uanze kutimiza ndoto zako. Basi wewe endelea kusubiri. Ila ninachofahamu utasubiri sana tu.
Unachopaswa kufahamu ni kwamba kama watu elfu wamekosea, na kama wewe uko sahihi, uko sahihi tu. wingi wa watu haufanyi kitu chao kuwa sahihi.
Kitu kingine unapaswa kufahamu kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuona ndoto yako kwa ubora kama ambavyo wewe unaona sasa hivi. Kama unasubiri ndoto yako ihakikiwe ndio uanze kuifanyie kazi basi endelea kusubiri wahikiki waipi tie kwanza ili na wewe uweze uanze kuifanyia kazi hiyo ndoto.
Binafsi nakubaliana kwa asilimia zote na Steve Jobs ambaye amewahi kusema kuwa, People who are crazy enough to think they can change the world are the ones who actually do. Akimaanisha hivi, watu ambao wana kichaa kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili dunia ndio huibadili dunia kweli. Sasa wewe kichaa chako kipoje?
Kama una kichaa kweli ukapime usije ukaanza kuwasumbua watu bure. Hahahah!!
Kitu pekee ambacho ni ukweli ni kuwa ukianza kuzifanyia kazi ndoto zako kwa kasi ndipo watu watatokea na kuanza kusema. Wapo ambao watakubaliana na wewe. Wapo ambao watakataa kile ambacho unakifanya kwa nguvu zao zote. Wapo wale ambao watafuata mkumbo wa  rafiki zao. Kama rafiki zao watasema wewe upo vizuri basi nao watafuata huo mkumbo. Kama rafiki zao watasema wewe ni kichaa na wao watasema hivyo hivyo.
Kitu pekee ambacho watu hawawezi kufanya pale utakapoanza kutimiza ndoto zako ni kukupuuza. Hata wale ambao watakupinga wewe watapaswa kufuatilia kazi zako kwanza ili wakupinge vizuri. Wale ambao watakupongeza nao watapaswa kufuatilia kazi zako ili wakupongeze. Kwa hiyo ni hakika hata maadaui zako na wasio maadui zako wote watakufuatilia.
Ninataka nimalizie kipengele hiki kwa kusema,
kuna kipindi ambapo kama mtu angesema ndege inaweza kuruka angani, basi angeonekana kichaa. Lakini vichaa wachache ndio walithubutu kusema tutaweka ndege angani.
Kuna kipindi kama mtu angesema nitamtumia mtu wa mbali picha yangu, basi angeonekana kichaa. Lakini vichaa wachache walimua kufanya hivyo, leo hii ni kitu cha kawaida.
Kuna kipindi kama mtu angesema, unaweza kuongea na mtu wa taifa jingine au kufanya kikao ma watu wa bara moja tena mkiwa mnaonana, basi mtu huyo angeonekana kichaa  lakini vichaa wachache waliwezesha hilo. Leo hii mambo ni safi kabisa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X