Kama Unataka Kuhamisha Mlima Basi Anza Kutoa Jiwe Moja Leo


Rafiki yangu, ni wazi kuwa kila mtu ana ndoto ya kufikia mambo makubwa sana maishani mwake. Kila mtu angependa kile kilicho kwenye akili yake kinatimia. Lakini sasa tatizo la watu wengi ni kutochukua hatua ya kwanza.
Siku ya leo nimeona waziwazi kwamba niongee na wewe moja kwa moja kuwa kama una ndoto ya kuhamisha mlima basi anza kuhamisha jiwe  moja leo. Ndoto ya kuhamisha mlima ni ndoto kubwa sana ambayo huwezi kuifikia kwa siku moja tu. Ila ukianza kutoa jiwe moja leo, kesho ukatoa mawili na kesho kutwa ukatoa manne, ni wazi kwamba utakuwa unaanza kupunguza ukali wa mlima.
Kinachokufanya wewe ushindwe kuzitimiza ndoto zako ni kwa sababu ya kutochukua hatua ndogo ndogo kila siku kuelekea ndoto kubwa. Nimekuwa nakushauri mara kwa mara kwamba ujenge utaratibu wa kufanyia kazi ndoto zako kwa kufanya vitu vidogo vidogo kila kwa siku. Ukiamua kuanzia leo hii kuanza kufanyia kazi ndoto zako, kwa kufanya vitu vitatu mpaka vitano tu kila siku. Ni wazi kwamba baada ya mwaka mmoja tu utakuwa umefanya vitu vidogo vidogo  1,095 mpaka 1825. Sasa nikuulize wewe. Hivi unadhani ukiunganisha vitu 1825 kwa pamoja vitaendelea kuwa vidogo kweli?
SOMA ZAIDI: Ushauri Muhimu Kwa Mtu Anayeanza Biashara Kutoka Kwa Jack Ma
Ni wazi kwamba havitakuwa vidogo tena. Sasa leo sitaki niandike sana, ila nataka ufanye zoezi lifuatalo sasa hivi. Rafiki yangu kaa chini na weka pembeni vitu vingine vyote kwa muda walau wa dakika kumi tu.
Kwanza, andika chini lengo lako kubwa kwa mwaka huu 2020.
Pili, vunja lengo lako kwenye lengo dogo ambalo unaweza kuanza kufanyia kazi mwezi huu.
Tatu, angalia ni kitu gani ambacho kimekuzunguka kwenye mazingira yako ambacho unaweza kuanza kufanyia kazi sasa hivi.
ANGALIA VIDEO HII: Iko Wapi Motisha Ya Januari Mosi?
Nne, anza kuchukua hatua sasa hivi, hata kama ni hatua ndogo tu.
Tano, pima matokeo unayopata kwa hatua ndogondogo unazochukua.
Sita, angalia vitu ambavyo havifanyi kazi kisha angalia namna ya kuviepuka au kuviboresha.
Saba, jifunze.
Nane, rudia nambari moja mpaka nambari saba.
Rafiki yangu nashukuru sana kwa muda wako. Nikutakie kila la kheri.
Ni mimi anayejali mafanikio yako,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X