KANYAGA MAPIGO YOTE YA KUITWA MTU WA KAWAIDA


Moja ya kitu ambacho jamii imekuwa inakutega wewe hapo, ni kukuweka kwenye kundi la WATU WA KAWAIDA. Utasikia watu wanasema, sasa mtuangalie na sisi watu wa kawaida.

mwingine atasema, sasa sisi watu wa kawaida hii itatusaidiaje.

Leo hii nataka nikwambie hivi, kanyaga mapigo yote ya kuwa mtu wa kawaida.

Ukiendelea kujiita mtu wa kawaida maana yake utawaachia kazi watu wengine kazi ya kufikiri. Na wao ndio watakuwa wanahusika kufanya maisha yako yawe bora zaidi. Kiuhalisia kama wewe unasubiri msaada wa mtu aje kukusaidia wewe ukiwa umebweteka. Endelea kusubiri, ila ukweli ni kwamba utasubiri sana.

Najua wanasiasa mara nyingi wakija kwako, watakwambia sisi tupo kwa ajili ya wanananchi wa kawaida kama wewe. Ila wewe usikubali kuendelea kuwa wa kawaida  Acha wengine wanaokubali cheo hicho waendelee kuwa wa kawaida wewe ANZA kutumia uwezo wako huo.
Wewe ni zaidi ya ulivyo sasa. Kuna vitu vikubwa ambavyo bado hujavifanyia kazi. Kanyaga mapigo hayo ya ukawaida anza kutumia uwezo wako. Ndio maana Dr. James akasema hivi, kulinganisha na vile watu tunavyopaswa kuwa, watu wameamka nusu.

Anyway, kwa sasa naishia hapa.
Hakikisha umeangalia
video hii Youtube ili kujifunza zaidi
https://youtu.be/J5qItIVr0M0

Usisahau KUSUBSCRIBE

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
www.songambeleblog.blogspot.com

#weweniulivyosasa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X