Maisha Yangekuwa Rahisi Kama Kungekuwa Na Kitu Hiki


maisha yangekuwa rahisi sana, kama kungekuwa na kibao cha mabadiliko kwenye safari ya maisha. Yaani kwamba ukikifikia kibao hicho unajua kwamba kuna mabadiliko mbele yatatokea baada ya mita mia, hivyo na wewe utapaswa kubadilika.

Lakini ukweli ni kwamba mabadiliko hayatokei kwa kelele kubwa. Ndio maana baadhi ya watu huyapokea na wengine huyapuuza. kama kila mtu angekuwa anajua wazi nini kitamtokea baada ya kuendana na mabadiliko au kuyapuuza, basi mtu angechukua uamuzi sahihi wa kifuata mabadiliko au angeamua kabisa kwa dhati kwamba mimi haya mabadiliko siyataki.

Sasa, katika njia kama hii hapa tunafanyaje? Nashauri sana uwe mtu wa kujifunza zaidi kila kukicha. na hasa linapokuja suala zima la teknolojia na biashara, basi walau mara moja kwa wiki, fuatilia kiundani vitu hivi viwili. Kama wewe unadhani uko bize kiasi hupati muda wa kufuatilia vitu hivi, nipende kukwambia kuwa kuna siku utakuja kushangaa watu wanakimbia kuelekea mashariki baada ya mabadiliko wakati wewe unaelekea kusini. Sasa mpaka uje ubadilike uweze kuendana na kasi ya hawa waliokutangulia, wengine watakuwa wanazidi kupepea.

kama unaona huwezi kulipa gharama kidogo ya mabadiliko sasa, basi niseme wazi kuwa kuna wakati utapaswa kulipa gharama kubwa zaidi ya hii unayobamia sasa hivi.

Kwa kumalizia,
 1. jitahidi kuisoma sekta yako na kuifuatilia mara mara kwa mara. ili yakitokea mabadiliko basi na wewe usiachwe.

2  wekeza walau siku moja kwa wiki kusoma mambo yanayoendana na mabadiliko.

Kwa leo napenda niishie hapa.

hakikisha umepata nakala ya kutoka sifuri mpaka kileleni sasa. nakala hii gharama yake ni 10,000 tu. na inakufikia popote ulipo tanzania

karibu sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X