Salaam Zangu Kwako. Nimekuwa Kimya Kwa Muda Sasa Haya Hapa Ndio Niliyogundua


Unaedeleaje rafiki yangu, ni takribani wiki sasa nikiwa sijakutumia ujumbe wa moja kwa moja  na wala nikiwa sijaandika na kuweka makala kwenye blogu ya SONGA MBELE.
Pole sana rafiki yangu kwa mimi kupotea ghafla bila kutoa taarifa. Ila nipende tu kukwambia kuwa kama wahenga wanavyosema. Kimya kikuu kina mshindo mkuu. Kwa upane wangu mambo yako hivyo hivyo. Nitakuwa hewani ndani ya siku mbili zijazo. Na mambo yote yataendelea kuwa vizuri.
Kwa leo naomba tujadiliane  ungependa kusikia nini kutoka kwangu?
Ipo hivi, ndani ya kipindi hiki cha ukimya nimeweza kusoma vitabu visivyopungua tisa. Ndio huwezi amini vitabu sita na vyote ni konki.
Ngoja niviweke hapa chini ili uvione wewe mwenyewe.
1. The Richecst Man In Babylon
2. Rich Dad Poor Dad
3. The Secret Of The Millionaires Mind
4. Think And Grow Rich
5. As A Man Thinketh
6.  Acres Of Diamond
7. Spacex And Tesla Motors Engineer, Elon Musk
8. Who Moved My Cheese?
9. Jonathan Livingstone Seagull
Je, ungependa kujua nini?
Je, ungependa kujua kuhusu jinsi nilivyosoma vitabu vyote tisa? Nimetumia njia gani kusoma vitabu hivi ndani ya kipindi kidogo?
Je, ungependa kujua ni kitabu gani ningependa na wewe usome sasa hivi?
Je, ungependa kupata uchambuzi wa ktabu gani?
Au wewe unapenda tu kujua nilikuwa wapi. Hahahah
Kwa leo mimi nakutakia kila la kheri. Nategemea kusikia mengi kwako
Ni mimi rafiki yako,
GODIUS RWEYONGEZA
MOROGORO TZ,
0755848391
Mawasiliano yote na mimi kwa sasa, yafanyike kwa barua pepe. godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X