Vikwazo Kama Hiki Hapa Huwa Vinatokea Kukuimarisha Sio Kukuangusha


Moja ya kitu ambacho ambacho kimekuwa gumzo na bado kinaendelea kuwa gumzo ni virusi vya korona. Kila mtu amekuwa kila mtu amekuwa akiongea na kutazama  kwa jicho la tofauti na huku wengi wakifikiri kwamba uwepo wa virusi hivi ndio mwisho wa dunia.
Siku ya leo nataka niokuoneshe jinsi vikwazo kama Corona ambavyo vipo kukuimarisha wewe na wala sio kukuangusha.
Kabla sijaanza kuongelea suala hili kiuandani napenda nikukumbushe usemi ambao aliusema Tony Robins kuwa ni matatizo ambayo yanatufanya tukue. Bila matatizo tusingekua. Hii ndio kusema kwamba tatizo lolote ambalo linatokea kwenye maisha yako. Sio tu kwamba linakuwa linatokea ili kukuangusha. Bali linakuwa linatokea kwa ajili ya kuhakikisha kwamba linakuimarisha.
Kifaranga kinapokuwa kwenye yai huwa kinatakiwa kubomoa ukuta ule wa yai ili kiweze kutoka nje. Ikitokea wewe umekisaidia kifaranga kutoka nje. Basi huo huwa ndio mwisho wa kifaranga hicho. kwa nini? kwa sababu umekisaidia kutatua tatizo ambalo lilipaswa kutatuliwa na kifaranga chenyewe. Hivyo hivyo kwa kipindi hiki hapa.
1. Kitu kikubwa ambacho unaweza kufanya ndani ya kipindi hiki hapa ni kuangalia namna ambavyo unaweza kutoa huduma bora zaidi kwa watu.
2. Hakikisha kwamba umefuata kanunia na taratibu zote ambazo zinatambulika kujikinga na ugonjwa huu. Zifuate wewe mwenyewe. Lakini pia wateja wako na wafanyakazi. Ukiumwa awewe au mfanyakazi wako huduma zitakwama. Akiumwa mteja wako utakosa fedha ya  kuendesha biashara. Hivyo hakikisha hauumwi wewe wala mfanyakazi wako.
3. Wapokee na wahudumie vyema wateja wapya. Katika kipindi hiki hapa unaenda kupata wateja wapya ambao hujawahi kuwapata hapo awali. Hakikisha kwamba huu unakuwa mwanzo mzuri wa wewe kujenga mahusiano ambayo yataendelea kudumua hata baada ya virusi hivi kutoweka.
Rafiki yangu kwa leo mimi naishia hapo nichukue nafasi hii kukutakia jumapili njema sana.
Ni mimi rafiki yako wa ukweli GODIUS RWEYONGEZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X