Hii Ndiyo Idadi Ya Kurasa Za Kitabu Ambazo Unaweza Kuandika Kwa Siku Za Mwaka Zilizobaki


Rafiki yangu, bila shaka siku ya leo unaendelea vyema kabisa. siku ya leo nimeandaa makala kwa ajili ya wale ambao kazi zao zinawabana sana kiasi kwamba hawapati muda wa kukaa chini na kuandika japo wangependa kuandika na wanajisikia kwamba wana kitu cha kuandika.

 

Kwanza nipende kusema kwamba hicho kitu ambacho unaona kwamba unacho, hakikisha haufi nacho. Na mimi siwezi tu kukwambia kwamba uandike, bila kukupa mwongozo utakaoutumia ili uweze kuwa wenye manufaa kwako.

 

Siku ya leo ningependa nikwambie namna ambavyo utawez kuandika kitabu kimoja chenye kurasa zaidi ya 250 kwa siku za mwaka zilizobaki. Ebu fikiria kwa miaka yote ambayo tayari umeishi hapa duniani kama ungekuwa unaandika kitabu cha kurasa 250 kila mwaka sasa  hivi ungekuwa umeandika vitabu vingapi?

 

Ni jambo la kushukukru kuwa wewe unapata maarifa haya, maana kuna watu ambao wangetamani kupata maarifa haya ila hawayapati kabisa. Hivyo siku ya leo nimeona nikuwekee hii njia ya kipekee itakayokuwezesha kuandika kitabu chenye kurasa zaidi ya 250.

 

Na njia hii ni rahisi sana. kila siku kwa siku zilizobaki, andika ukurasa mmoja tu. mpaka sasa hvi zimabaki siku 260. Ukijiwekea lengo la kuandika ukurasa mmoja tu kila siku. Ni wazi kwamba kufikia mwishoni mwa mwaka huu utakuwa umeandika kitabu kikubwa sana. na watu wengi watabaki kukushangaa na wengine watakuja kwako kuomba ushauri.

 

Ila kumbe siri yako ya mafanikio itakuwa ni hii hapa. huu ndio ukweli wenyewe na siku zote ukweli huwa unakuwa rahisi lakini ukiufanyia kazi, basi ni wazi kuwa  mwaka huu kwa mara yako ya kwanza utaandika kitabu.

Ukizembea, na usipofanyia kazi hiki ambacho umejifunza hapa, utashangaa mwaka huu umeisha ukiwa hujafanya kitu chochote cha maana.

 

Sasa ni juu yako, kuweka katika matendo hiki ambacho umejifunza hapa. au kukiweka kapuni. Kila la kheri

 

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X