Huyu Ni Mtu Ambaye Unapaswa Kushindana Naye Kila Siku


Rafiki yangu bila shaka siku ya leo imekuwa ni siku bora sana kwako. Karibu sana katika makala ya siku hii ambapo ninaenda kukwambia mtu ambaye unapaswa kushindana naye kila siku.

Kama kwenye maisha yako utapaswa kuanzisha mashindano ya kuona ni mtu gani ni bora, mtu gani anafanya vizuri zaidi ya mwingine, mtu gani anaingiza kipato kikubwa zaidi ya mwingine. Kama kweli utapaswa kushindana na mtu mwingine basi utapaswa kushindana na wewe mwenyewe.

 

Unapaswa kushindana na wewe wa mwaka jana au wewe wa siku ya jana. Hakikisha kwamba wewe wa leo anakuwa ni bora zaidi ya wewe wa jana. Kama jana ulizembea kwenye utendaji wako wa kazi. kama wewe wa jana hukutimiza majukumu yako kadri ilivyokuwa inatakiwa, basi wewe wa leo unapawa kuwa bora zaidi unapaswa kujituma. Unapaswa kuepukana na kuhairisha.

 

Iko hivi kila siku kwako inapaswa kuwa ni siku bora zaidi ya vile ilivyokuwa jana. Ukiona leo hii unasema kwamba bora ya jana basi ujue kwamba kuna sehemu umekosea. Ujue kwamba wewe wa leo amekuwa dhaifu kuliko wewe wa jana.

 

Kwa asili yetu sisi binadamu ni viumbe wa kukua. Na kitu chochote kile ambacho hakikui basi kinakufa. Kuanzia leo jiwekee utaratibu wa kuhakikisha kwamba unakua kila siku. Maeneo muhimu ambayo wewe unapaswa kukua ni kwenye masuala ya kifedha, kiroho, kiakili na kimwili. Kila siku hakikisha kuwa umekuwa bora zaidi kwenye maeneo haya.

 

Rafiki yangu, kwa upande wangu sina la ziada, isipokuwa ntu ningependa nikutakie siku njema sana. ninaamini siku hii hapa unaenda kuitumia vyema kabisa.

 

Nipende tu kukumbusha kuwa kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu, basi fanya hivyo sasa hivi kwa kubonyeza HAPA.

 SOMA ZAIDI: Kheri Ya Mwaka Mpya Na Mambo 12 Ambayo Unaweza Kufanya Kuanzia Leo

 

Ni mimi anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X