Kama Umeajiriwa, Upo Kwenye Biashara. Na Mteja Wako Ni Mtu Mmoja Tu Ambaye Ni Mwajiri Wako. Haya Hapa Ni Mambo Matano Ambayo Unaweza Kufanya Ili Kuuteka Moyo Wake


 

Ujue kila mtu hapa duniani yupo kwenye biashara, tofauti ya watu waliofanikiwa zaidi kwenye biashara ni wale ambao wanakuwa tayari kuwasaidia watu wengi zaidi na huku wengine wakichaguwa kuwahudumia wateja wachache.

 

Mtu anapoingia kwenye ajira anakuwa amechagua kumhudumia mteja mmoja ambaye ni mwajiri wake. Kwa hiyo kipato chake chcote anakuwa anakitegemea kutoka kwa huyo tu. wakati mtu ambaye yupo kwenye biashara anakuwa amechagua kuwahudumia maelfu mpaka mamilioni ya watu. na kipato chake kinatokana na hao maelfu au mamilioni. Ni wazi kwamba kadri unavyohudumia watu wengi zaidi utalipwa zaidi kuliko yule ambaye anamhudumia mtu mmoja.

 

Hata hivyo ni ukweli kwamba ajira inaweza kuwa ni nafasi yako wewe hapo kuanzia, kwa sababu utapata mtaji na utapata  watu wa kushirikiana nao ambao hapo awali hawakuwa kwenye mzunguko wako wa biashara. Hivyo kwa kuona umuhimu kama huo hapo nimeona leo hii nikuletee mambo matano ambayo unapaswa kuyafanya ili uweze kuishi vizuri na mwajiri wako pamoja na wafanyakazi wenzako

1. Anza kufanya kazi zaidi ya mtu yeyote ambavyo anategemea kutoka kwako.

2. Ipende kazi yako, wahamasishe wengine kufanya kazi zaidi na wasilisha kazi zako kwa wakati

3.Kama kuna shughuli mpya na watu wengine wanaiogopa, kwako hii inaweza kuwa ni nafasi yako kuonesha ujuzi wako wa kipekee

4. Usilalamike, ukiona ulalamikaji umekunyemelea basi unyamazishe. Kama huwezi bora tu ukaacha kazi maana hiyo kazi haikufai. Utaharibu mwenendo wa kazi kwa kuwaharibia hata wale wanaopenda kufanya kazi kwa bosi wako.

5.Usifanye maisha ya mwajiri wako magumu kwa sababu ya vitu ambavyo unafanya. Siku zote jitahidi kurahisisha maisha.

6. Usifanye kosa ukitegemea kwamba kuna mtu atakutetea.

 

Rafiki yangu, hayo ndiyo mambo ya muhimu ambayo unaweza kufanya ili kuuteka moyo wa mwajiri wako paoja na kuishi vyema na wafanyakazi wenzako. Nakutakia kila la kheri katika kuyaweka katika matendo.

 MAKALA NYINGINE ZINAZOENDANA NA HII: Mfanyie Kitu Hiki Myu Huyu Hata Kama Humpendi

Ni mimi anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X