Mambo Kumi Na Moja (11) Ambayo Watu Waliofanikiwa Hawachoki Kufanya


Rafiki yangu karibu sana kwenye makala ya siku ya leo. Na leo, nimeona nikushirikishe mambo ambayo watu waliofanikiwa hawachoki kufanya;

1. hawachoki kujifunza na kusoma vitabu.

2. hawachoki kufanyia kazi kile ambacho wamejifunza.

3. hawachoki kutafuta ushauri wa kitaalamu au ushauri wa watu waliofanikiwa.

4. hawachoki kuuliza maswali sahihi.

5. hawachoki kujituma.

6. hawachoki kulipa gharama. Maana wanajua ili ufanikiwe lazima ulipe gharama.

7. hawachoki kutoa huduma zaidi kwa jamii. Maana, wanajua kadri unavyoihudumia jamii, ndivyo jamii yenyewe inakuwa tayari kukulipa.

8. hawachoki kufanya kazi kwa viwango vikubwa sana.

9. hawachoki kutimiza majukumu yao.

10 . hawachoki kutangaza bidhaa zao. Maana wanajua ukikitangaza walau mara saba, ndipo mtu anachukua hatu ya kwanza kununua.

11. hawachoki kubeba majukumu ya maisha  yao na wala hawamsubiri mtu yeyote ili aje kuwasaidia kufanya kile ambacho wao wanapaswa kufanya

 

Je, wewe umekuwa unachoka kufanya kitu kimojawapo kati ya hivi. Kuanzia leo, azimia kuwa sitachoka kufanya kazi ambazo ninapaswa kufanya. Kila la kheri

 

JIUNGE NA MFUMO WETU WA KUPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUM Kwa kubonyeza HAPA

KUPATA NAKALA YA BURE YA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, basi bonyeza hapa. zimebaki siku mbili tu kabla ya zawadi hii kuisha
umekuwa nami rafiki yako wa ukweli,
Godius Rweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X