SIMAMA KWA MIGUU YAKO MIWILI


 

Leo rafiki yangu nimeamua kuongea na vijana wa kitanzania.  Makala ya leo inawalenga zaidi hasa wanachuo, wahitimu wa chuo na vijana wengine ambao bado wanakaa nyumbani.

Sasa labda tujiulize kusimama kwa miguu miwili ndio nini?

KUSIMAMA kwa miguu miwili maana yake kuamua kutimiza malengo yako wewe kama wewe bila kusubiri wazazi, walezi au serikali.

kama una malengo ambayo umjiwekea basi unapaswa kusimama kwa miguu miwili na kuyafanyia kazi.
kadri unavyokua unapaswa kujijengea hali ya kujitegemea katika utendakazi wako. unapaswa kusimama wewe kama wewe.
usikae nyumbani ukabweteka kwa sababu kuna baba au mama ambaye anakupa chakula na kitu cha kunywa. unapaswa kufikia hatua ambapo wewe unaweza kujitegemea kwa chakula, kunywa na uendeshaji wa maisha yako kiujumla. usiendelee kukaa nyumbani kwa sababu unaona wazazi wanaleta kila kitu. na wewe ukasahau kujenga maisha yako. anza sasa hivi, SIMAMA KWA MIGUU YAKO MIWILI.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X