Tofauti 15 Kati Ya Matajiri Na Masikini Ambazo Zitakuacha Mdomo Wazi


Unaendeleaje rafiki yangu, bila shaka siku ya leo imekuwa ni siku bora sana. 

Leo nimeona nikuletee tofauti 12 zilizopo kati ya matajiri na masikini. Hizi tofauti zitakuacha mdomo wazi kabisa.  kuna vitu ambavyo pengine umezoea vinafanywa wengi na hivyo vinaonekana ni sahihi. Ila ukweli ni kwamba wingi wa watu haumaanishi usahihi wa kitu. Hivyo watu wanaaweza kuwa wengi wanafanya kitu hicho, ila sasa kumbe ni cha kimasikini kama ambavyo unaenda kuona hapa,

 

TOFAUTI YA KWANZA;  MATAJIRI WAKIPATA FEDHA WANAWEKA AKIBA KWANZA KISHA NDIO WANATUMIA, MASIKINI ANATUMIA KWANZA NDIO ANAKUJA KUWEKA AKIBA

Iko hivi masikini ni watu wa ajabu kweli. Wao wakipata fedha, wanakimbia kufanya matumizi na kisha wanasubiri kiasi ambacho kitabaki baada ya matumizi ili waweke akiba. Sasa unajua nini, mwisho wa siku hakuna fedha ambayo huwa inabaki, maana hakuna siku hata moja ambapo fedha imewahi kukosa matumizi. Hivyo masikini huwa hawaweki akiba wala kuwekeza.

 

Sasa turudi kwa matajiri, kitu cha kwanza kabisa wanachofanya baada kuingiza kiasi cha fedha sio kutumia, bali ni kuweka akiba na kuwekeza. Kisha kiasi kinachobaki ndicho wanatumia. Kwa sababu matajiri wapo vizuri kwenye kupangilia vitu, basi huwa hawaishiwi kabisa. huwa wanabaki na kiasi cha kutumia hukuwa wakiwa wamejizuia kufanya matumizi ambayo sio ya lazima. Kwa kufanya hivi maisha yao huendelea kuwa bora zaidi.

 

TOFAUTI YA PILI; NI KUTULIZA FEDHA

Maskini akipata fedha ile mipango yake mizuri yote huwa inapotea kwanza. Anakuwa kama amepagawa kwa kuiona fedha. Anakimbia kuitumia fedha, ikiisha ndio anaanza kukumbuka mipango yake.

Matajiri wenyewe wana fikra tofauti kabisa. wao wakipata fedha wanaituliza kwanza, na kukaa nayo. Kama kuna mipango ya haraka inakuja kwao basi wataiandika chini na kisha kuangalia kama ni ya lazima. Hawakurupuki kutumia fedha kwa sababu ipo. Ila wanatumia kuendana na mipango.

 

TOFAUTI YA TATU; MASIKINI HUAMINI KWAMBA FEDHA YOTE WANAYOPOKEA NI YA KWAO, MATAJIRI HUTOA FEDHA YAO KWANZA KISHA HUWAPA WATU WENGINE FEDHA ZAO

Masikini akipokea fedha, basi anadhani kwamba hiyo fedha yoote inakuwa ni ya kwake. Hivyo, anatumia anavyotaka. Ananunua nguo, anaunua gari, ananunua nyumba, chakula n.k.

 

Matajiri wao hali ni tofauti. Wanajua fedha ipo ili kuzunguka. Na kitu hiki kinawafanya wawekeze. Wanajua fedha yote sio ya kwako. wanajua kwa mfano ukipokea elfu kumi. Unaweza kununua unga elfu tano, mafuta elfu nne na ukatumia elfu moja usafiri. Hivyo mpaka hapo elfu kumi, inakuwa imeisha na wao  wanakuwa wamewalipa wengine bila kujilipa wenyewe. Hivyo kwa msingi huo wanajua wazi kwamba mtu anakuwa hajashika fedha zake, badala yake anakuwa na fedha za watu.

 

Kwa hiyo wanachofanya matajiri, ni kutoa fedha yao kwanza kabla ya kutoa fedha za watu wengine.

 

TOFAUTI YA NNE; MATAJIRI NA MASIKINI HUTUMIA KAULI MOJA HUKU WAKIMAANISHA VITU TOAFUTI

Kuna kauli kwamba fedha inapaswa kutumiwa. Tena wengine huiweka kauli hii vizuri zaidi kwa kusema kwamba, ukiitumia fedha lazima itakuja nyingine zaidi. Unaweza kuona hii ni kauli moja  ila sasa ngoja tuone utofauti kwenye matumizi ya kauli hii hapa

 

Masikini wakipokea fedha wanakimbia kunywa pombe, kununua sigara na kuwaridhisha rafiki zao ili waonekane ni watu wazuri. Hivyo wanakuwa wanatumia fedha kwa kufuata kanuni hiyo kwamba kadri unavyoitumia fedha, lazima itakuja zaidi.

 

Matajiri wao wakiipokea fedha, wanaitumia kwa kufanya uwekezaji, kununua hisa, kununua hatifungani na kuwekeza kwenye vitu ambavyo havishuki thamani au vitu ambavyo vinawaongezea fedha zaidi.

Kinachotokea ni kwamba, kweli zile fedha zinawatengenezea matajiri fedha zaidi, huku masikini wakizidi kuwa masikini.

 

TOFAUTI YA TANO; WOTE WANAAMINI KWENYE BAHATI, ILA UTENDAJI KAZI UNATOFAUTIANA

Masikini wanaamini kwamba, ili uweze kutengeneza utajiri basi unapaswa kuwa na bahati. Wanaamini kwamba kuna watu wana nyota zao zinag’aa huku wengine nyota zikiwa zimefifia. Wanaamini huwezi kutengeneza utajiri labda ikitokea mjomba, shangazi au ndugu akakupa fedha zake au ukarithi basi hapo ndipo unatengeneza utajiri.

 

Matajiri wao pia wanaamini kwenye bahati. Ila sasa matajiri wanaamini kwamba, bahati inatengenezwa. Wanajua kabisa  ili ujikwae lazima uwe njiani unatembea. Na bahati siku zote haiji kwa watu ambao wamefunga milango.

TOFAUTI YA SITA; Matajiri wanaamini kwenye kufanya kazi kwa bidii, kujituma, kwenda kinyume na mazoea na kufikiri kwa kutumia akili zao.

Masikini wanaamini kwamba kuna mtu sehemu fulani ambaye anahusika kuwatengenezea maisha wanayotaka. Hivyo wanakaa wakisubiri.  Wanachosahau ni kwamba maisha mazuri unayatengeneza wewe mwenyewe.

 

TOFAUTI YA SABA; MASIKINI WANAAMIMI KWENYE UNYONGE, MATAJIRI WANAAMINI KWENYE UKUU

Masikini wao wanajiita wanyonge. Tena wakiambiwa kwamba nyie ni watu wanyonge, basi wanajisikia faraja kweli kweli.

Ila hali kwa matajiri ni tofauti. Wanaamini kwenye ukuu. Hata inapotokea matajiri wakayumba kidogo, sio kwamba huo ndio unakuwa ni mwanzo na mwisho. Au sio kwamba kitendo hicho kinawafanya wanyonge. Bali wao tayari wanakuwa wameona fursa ya kurekebisha hicho kitu na kusonga mbele.

 

UNYONGE KWA MATAJIRI HAUNA NAFASI, siku zote wanaamini wanaweza. Na muda wanasongambele kuhakikisha kwamba wanaweza.

 

TOFAUTI YA NANE; WOTE WANAKUTANA NA VIKWAZO NA MATATIZO ILA FIKRA ZAO ZINATOFAUTIANA

Matajri na masikini wote wanakutana na vikwazo pamoja na matatizo. Ila sasa fikra za hawa watu wawili hutofautiana. Masikini hufikiri kwamba vikwazo ni laana, masikini huona vikwazo kama mwisho. Vikwazo humkwamisha masikini na kumfanya atulie..

 

Hali huwa ni ya tofauti kwa matajiri. Wao wakikutana na vikwazo wanajua kuna fursa kubwa ambayo inakuwa mbele yao inakuja. Hivyo wanahakikisha kwamba wanatafuta suluhisho la tatizo hilo na kusonga mbele.

Matajiri sio wadogo kulinganisha na matatizo wanayokutana nayo.  Hata wakikutana na tatizo kubwa lazima wao wajiinue juu zaidi ya tatizo kisha kuanza kulifanyia kazi. matajiri wanajua wazi kwamba huwezi kutatua tatizo ambalo limekuzidi uwezo. Hivyo kuna mawili, au tatizo wewe ulishushe chini  tatizo ili uweze kulitatua au tatizo libaki juu na ushindwe  kulitatua.

 

Ukitaka kunielewe kwenye hili hapa ngoja tu nikupe mfano mdogo wa simu yako. Hivi, hiyo simu ikiharibika sasa hivi unafanyaje? Bila shaka utaniambia kwamba mbona jibu linajulikana, si unaenda kwa fundi? Vizuri sana. sasa wewe ukifanya hivyo maana yake unakuwa umekuwa mkubwa kuliko  tatizo lenyewe ambalo limetokea. Hivyo unakuwa tayari kulitatua.

 

Lakini ukikwama na kuona kwamba huo ndio mwisho, basi kweli hapo unakuwa umeshindwa. Sasa masikini wengi wapo hapa. Kila wakikutana na vikwazo basi wananyoosha mikono juu na wanashindwa kuendelea mbele.

 

TOFAUTI YA TISA; MATAJIRI NA MASIKINI WOTE WANAKUWA UPDATED MUDA WOTE ILA SASA KINACHOWATOAFUTISHA NI HIKI

Huwezi amini masikini na matajiri wote wanaamini kwenye huu usemi wa kuwa updated. Ila masikini wanakuwa updated kwenye vitu ambavyo havina maana. Wanakuwa updated kwenye taarifa za habari, wanakuwa updatedkwenye status za whatsap na facebook na wanatumia muda mwingi mtandaoni wakizurura.

Masikini hawasomi vitabu. Na asilimia kubwa ukiwauiza mara yako ya mwisho kusoma kitabu ni lini wanakwambia kwamba ilikuwa baada ya shule, miaka kumi au ishirini iliyopita

 

Ila sasa matajiri wanakuwa updated kwenye mambo ya maana.  Wanajifunza kuhusu biashara, wanajifunza kuhusu fedha, wanajifunza kuhusu mahusiano na mambo mengine.

 

Matajiri  ni wasomaji wazuri lakini pia ni wahudhuriaji wazuri wa semina. Matajiri wapo tayari kulipia kitabu au semina hata kama ni ya gharama kubwa. Wanaamini kwamba, kama kwenye hiki kitabu nitaweza kujifunza kitu kimoja cha kufanyia kazi, basi fedha yangu itakuwa imetumika ipasavyo.

 

TOFAUTI YA KUMI; MASIKINI WAO WANAJUA KILA KITU. Hawana cha kujifunza cha ziada. Yaani walishahitimu. Ila matajiri wanaamini kwamba hakuna kuhitimu kama bado unapumua. Matajiri wanaamini unahitimu pale watu wanapokuwa wanasema pumzika kwa amani.

 

TOFAUTI YA KUMI NA MOJA; WOTE WANAAMINI KWENYE MAHUSIANO, ila sasa sasa masikini hawana muda wa kujenga mahusiano mazuri na kuyaimarisha kila siku. Wanakosa fedha na mahusiano mazuri wanakosa pia.

Kwa matajiri hali ni tofauti. Kitu nambari moja kwao ni familia. Wanatenga muda wa kuwa na familia kila siku. Wanawasaidia watoto wao kufanya kazi za shuleni.

Kama ni kusoma vitabu basi wanasoma kwa pamoja na watoto wao.

 

Lakini pia matajiri wanaamini kwamba unaweza kuwa  na vitu vyote ambavyo utaka kuwa navyo. Masikini wenyewe wanaamini kwamba huwezi kuwa tajiri huku ukiwa na mahusiano, fedha, afya na busara. Matajiri wanavyo vyote hivyo.

 

TOFAUTI YA KUMI NA MBILI; WOTE WANATUMIA MITANDAO YA KIJAMII ILA LENGO LINATOFAUTINA

Masikini wanaingia mitandaoni ili kuwakejeli wengine, wanaingia ili kuwasema watu wengine na kufuatilia maisha ya watu wengine. Lengo lao wajue ni mtu gani anatoka na nani . hali ya mahusiano yao sasa hivi ikoje. Wanakaa kujadili mtu fulani ana kipaji na mwingine hana.

 

Wakiona mtu anafanya kazi basi wanaanza kuzungumza kila kitu kuhusiana na huyo mtu (habari za kweli na uongo).

 

Matajiri wao wanaingia mtandaoni au kujifunza, au kutangaza kazi zao au biarasha zao, au wanaingia mtandaoni ili kutafuta taarifa muhimu tu. matajiri hawana muda na mtu. Wana muda na wao tu.

 

TOFAUTI YA KUMI NA TATU; MATUMIZI YA MUDA

Masikini hawana ratiba maalumu. Yaani wao ni bendera hufuata upepo. Hivyo likitokea jambo ambalo wao wanaona wanaweza kushiriki wanaenda.  Wakiwa bado wanaendele na hilo jambo likatokea jingine wanaacha hili la awali na kwenda kufanya jingine. Kwa hiyo wao hawana ratiba  maalumu. Yaani, ni bora liende. Wakikwambia  tukutane saa saba, basi wanakuja saa nane au saa tisa, kisha wanaendelea kukwambia kwamba hakuna haraka barani Afrika.

Ila sasa matajiri ni tofauti. Wanapangilia muda wao. Wanajua muda gani wanapaswa kuwawapi na muda mwingine wanapaswa kuwa wapi. Hawaruhusu ratiba zao kuingiliwa bila mpangilio maalumu. Wakikwambia tukutane muda fulani wanamaanisha kweli. MATAJIRI WANA MUDA WA KUTAFAKARI MAISHA YAO, KUBADILI MAKOSA NA KUSONGA MBELE

 

TOFAUTI YA KUMI NA NNE; KULALAMIKA.

Masikini wanalalamikia kila kitu ambacho kinatokea maishani mwao. Wanalalamikia serikali, wanalalamikia wazazi, ndugu n.k. yaani masiki hajawahi kukosa mtu wa kulalamikia kwa kitu chochote maishani mwake. Akikosa fedha atapata mtu wa kulalamikia. Akichelewa basi siku hiyo bodaboda au konda atatupiwa lawama.

 

Ila sasa matajiri wao wanabeba jukumu la maisha yao. Wanajua wazi kwamba,  maisha ni wajibu wao. Wanajua kushinda au kushindwa ni juu yao.

 

TOFAUTI YA KUMI NA TANO; KUWARIDHISHA WENGINE; masikini wao wanataka waonekane kwa watu kwamba na wao wana uwezo au wanajua. Hivyo hata wanaponunua nguo wanakuwa wanatanguliza watu wengine kwanza. Wanafikiri fulani atanionaje.

Unakuta kwamba masikini wanaingia gharama kubwa, kufanya vitu kwa kuwaridhisha watu. huku matajiri wao wakiwa wananunua vitu kwa sababu wanavihitaji ila sio kuwaridhisha watu

 

Rafiki yangu, hongera sana kwa kusoma makala hii ya kipekee mpaka mwisho. Hii ni ishara tosha kwamba wewe ungependa kujitoa kwenye kundi la watu masikini na kujiweka kwenye kundi la watu matajiri. Hongera sana.

 

Sasa kazi ambayo imebaki kwako ni kuanza kufanyia kazi haya yote ambyo umejifunza,.

Mwisho kabisa nakukaribisha uwe miongoni mwa wanasongambele kwa kubonyeza HAPA

Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X