Aina Mbili Za Hamasa Na Jinsi Ya Kuzitumia Kwa Manufaa


Hivi unaposikia watu wanazugumzia juu ya hamasa unaelewa nini? je, ni kitu gani ambacho kinakuja kwenye akili yako?

Leo ningependa nikwambie aina mbili za hamasa na jinsi ambavyo unaweza kuzitumia zote. Aina ya kwanza ni HAMASA YA KUEPUKA KITU. Hii ni ile nguvu ambayo inamuskuma mtu kufanya kitu ili aepukane na kitu fulani. Mfano mwajiriwa anakimbizana kutimiza majukumu yake ili asipewe adhabu kazini au asifukuzwe kazi.

 

AINA YA PILI ni HAMASA YA KUPATA KITU FULANI Aina hii ya hamasa huwa inamskuma mtu kutimiza majukumu yake kwa sababu anajua kuna zawadi ambazo zinakuja mbeleni.

Kwa mfano mfanyakazi anatimiza majukumu yake akijua kwamba anaweza kupandishwa cheo, kuongezwa mshahara au zawadi nyingine nyingine

 

Kiuhalisia aina ya pili ya hamasa ndiyo huwa inazalisha mawazo ya kibunifu zaidi. Hata hivyo aina ya kwanza pia huwa inatumika pia. Maana kuna watu asipojua kwamba kuna adhabu, basi utakuta kwamba hatimizi wajibu wake vizuri majukumu yake

 

Hivyo kuanzia leo hakikisha kwamba unazitumia aina hizi mbili za hamasa kwa manufaa yako. Unaweza kuanza kuzitumia wewe mwenyewe au ukawazitumia pia kwa watu ambao unafanya nao kazi au sehemu zote mbili.

NAMMNA YA KUZITUMIA KWAKO MWENYEWE

Aina hizi za hamasa unaweza kuzitumia kwako kwa  kujipa majumumu na kujipongeza pale ambapo unakuwa umefanya kazi yako yako vizuri au kujipa adhabu. kwa mfano unaweza kuweka lengo kuwa usipofanya kitu fulani kila siku utapaswa kulipa elfu moja kama adhabu. na unaweza kumtafuta rafiki yako ukamwambia lengo ambalo utakuwa unalifanya. Labda tuseme kuandika kila siku.

 

Ssa unamwambia huyo rafiki yako kuwa “kuanzia leo nitakuwa naandika kila siku, endapo itatokea siku ambapo sitaandika basi nitakulipa elfu moja”. kwa namna hiyo adhabu hiyo ya kulipa inakufanya ujisukume zaidi.

 

Au kama huwa unapendelea kitu fulani, mfano kunywa kinywaji fulani. Basi unaweza ukaamua kufanya kinywaji hicho kuwa ni zawadi ambayo unapata baada ya kukamilisha kazi fulani.

Kama unapendeea kuingia mtandaoni, basi anza kuingia ktandaoni kama zawadi ambayo unapata baada ya kukamilisha majukumu fulani. Kama hutakamilisha hilo jukumu basi hakuna kuingia.

 

Rafiki yangu hizo ndizo aina mbili za hamasa na jinsi ambavyo unaweza kuzitumia kwenye maisha yako ya kila siku.

Kila la kheri

SOMA ZAIDI; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-108, tatizo  hujajua kuwa huzuiliki


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X