Hiki Kitu Ndicho Kinafanya Biashara Yako Ishindwe Kukua


Habari ya siku ya leo rafiki yangu. Karibu sana kwenye makala ya siku ya leo ambapo ninaenda kukueleza, kitu kimoja ambacho kinafanya biashara yako ishindwe kukua. Kitu hiki sio kingine bali ni kwa sababu ya kukosa maono. Unaweza kuwa unashangaa kuwa biashara yangu inakosaje maonio.

 

Pengine ulianzisha biashara yako ukiwa na mtazamo fulani wa kutaka kufika katika hatua fulani. Ni kweli ila kuna kitu kimoja ambacho nigependa ukifahamu kiundani. Unaweza kuwa na maono mazuri kichwani mwako. Ila kama hauwezi kuwashirikisha watu wengine unaoshirikiana nao kwenye biashara yako  hayo maono yako. Basi ni wazi kuwa utabaki nayo wewe mwenyewe. Na hiki ndicho kitu ambacho kinakukwamisha. Maana wewe utabaki KUDHANI watu wanayajua maono yako, ila utashangaa utendaji kazi wao hauendani na hayo maono.

 

Hivyo kuanzia leo unapaswa kubadili mwelelekeo wako. Badala yake anza kuwaonesha watu maono yako ya biashara na sehemu ambapo unataka kuipeleka. Je, unataka kuipeleka wapi baada ya miaka 10. Je, ndani ya miaka mitatu ijayo biashara yako inapaswa kuwa imefikia wapi? Je, mna mpango gani mkubwa wa kufanyia kazi ndani ya siku 90 zijazo? Vipi kuhusu mwezi  mmoja ujao.

 

Maono yako yanapaswa kujengwa kwenye msingi huo. Kisha kazi na shughuli zote ambazo zitafanyika ndani ya bishara yako zinapaswa kujikita kwenye hayo maeneo.

 

Hiki ni kitu kidogo ila usipokifanyia kazi kitakukwamisha.

 

Rafiki yangu, asante sana kwa wakati wako. Nikutakie kila la kheri

BONYEZA HAPA KUPATA CHA BURE

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X