Hivi Ndivyo Unaweza Kumiliki Kampuni Kubwa Kama CRDB, VODACOM, TBL Na Nyinginezo Kwa Mtaji Wa Elfu Kumi Tu


 

Pata nakala ya kitabu hiki kwa shilingi elfu 10 tu popote ulipo nchini. tuwasiliane kwa 0755848391

Hivi umewahi kujiuliza kuwa kwa mtaji wangu huu mdogo naweza kutoboa kweli na kufanya mambo makubwa. au umekuwa unakwama katika kukuza mtaji wako kwa siku sasa na unapenda kukuza mtaji wako. Au kwa mfano umewahi kuwa na wazo tu la kumiliki kampuni kubwa ili na wewe uweze kutengeneza faida kama ambavyo makampuni mengine yanafanya?

 

Siku ya leo nilipenda nikupe mbinu zitakazokuwezesha wewe kumiliki kampuni kubwa huku ukiwa na mtaji mdogo. Na mbinu hii ni kupitia kununua hisa za kampuni husika. Hisa za kampuni huwa zinauzwa kupitia soko la hisa. Na kwa Tanzania soko la hisa lipo Daresalaam (DSE).

 

Labda unaweza ukawa unajiuliza kuwa hisa nini? hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni ambayo unaipata kwa kuchangia mtaji wa uendeshaji. Mfano tuseme kwamba wewe unahitaji kuanzisha bishara ya laki moja. ila kwenye mfuko wako una elfu sabini. Sasa unaenda kwa rafiki yako ambaye unamweleza mpango wako wa biasahra na kumwomba awekeze mtaji kwenye biadhara yako. Na huyo rafiki yako anawekeza efu 30, ambayo inakamilisha laki moja. kwa hiyo kwenye umiliki wa biashara hiyo ni kuwa wewe utakuwa na umiliki wa asilimia 70 wa biashara, wakati rafiki yako atakuwa na umiliki wa asilimia 30. Huu ni mfano ambao nimeutoa kwenye ngazi ya kawaida kabisa ya chini, lakini unafanya kazi kwenye ngazi kubwa ya biashara kama makampuni makubwa.

Makampuni makubwa pia huwa yanauza sehemu ya hisa zake kwa ajili ya kuongea mtaji kwenye biashara. Na hisa hizi zinaweza kununuliwa na mtu yeyote na hata wale ambao huwa wananunua baadae huwa wana uwezo kuuza pia

 

Mpaka sasa hivi soko la hisa la Daresalaam lina makampuni 27 ambayo yamejiandikisha. Kwenye haya makampuni unaweza kuchagua kampuni moja ambayo unaweza kununua hisa zake kwa kuanza na mtaji mdogo. Kitu muhimu unachopaswa kufahamu ni kuwa  ukianza na fedha kidogo utapaswa kuendelea kununua mara kwa mara ili uongeze kiwango chako cha hisa.

 

KIWANGO CHA CHINI CHA HISA UNAZOWEZA KUNUNUA

Kiwango cha chini cha hisa unazoweza kununua kwa kuanzia ni hisa 10. Kwa hiyo unaweza kuingia kwenye tovuti ya soko la hisa la Daresaam ukachagua aina ya kampuni ambayo utanunua hisa zake. Kisha ukaangallia bei zake kwa sasa hivi. Bei ya hisa za sasa hivi utazidisha mara kumi. Hicho ndicho kiwango cha fedha ambacho unahtaji kuwa nacho kununua hisa za kampuni hiyo.

Kuna baadhi ya kampuni ambazo hisa zake ziko chini ya 200. Hii ndio kusema kwamba kwa shilingi elfu mbili tu unaweza kununua hisa za kampuni na wewe kuwa mmiliki wa kampuni kubwa.

 

Rafiki yangu usikwame, endelea kufuatilia masomo haya muhimu kwenye blogu hii hapa. siku nyingine niitaeleza vigezo vya kuzingatia kwenye kuchagua aina ya hisa za kununua.

MUHIMU ZAIDI; jiunge na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu kwa KUBONYEZA HAPA


4 responses to “Hivi Ndivyo Unaweza Kumiliki Kampuni Kubwa Kama CRDB, VODACOM, TBL Na Nyinginezo Kwa Mtaji Wa Elfu Kumi Tu”

  1. Habari, ukitaka kununua fuata hatua zifuatazo.

    1. Chagua broker wako Kisha nenda kwake kajiandikishe.

    Baada ya hapo hapo utakuwa unanunua hisa kupitia kwa huyo broker (dalali)

  2. Utakua ukiangalia soko linaendaje la hisa lakini pia kunakua na viwango kwa mfano kuna amount unawekewa labda ili uwe na hisa laki 2 ndo utaruhusiwa kuuza faida nyingine inapatikana baada ya kampuni kuingiza faida na wewe unakua kwenye mgao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X