Hivi Ndivyo Unaweza Kutumia Muda Wako Na Fedha Kwa Manufaa


Moja ya kitu muhimu kwenye maisha ya kila siku ni muda na fedha. Ipo misemo kadha wa kadha ambayo imesemwa ikiwa ni pamoja na watu kusema kuwa muda ni mali. Muda haumsubiri mtu. Na misemo mingine kama vile poteza fedha utaipata ila ukipoteza muda hautaupata.

 Kwenye makala ya leo sitaki nikuelekeze jinsi kupoteza fedha na kuupata muda. Badala yake ningependa vitu hivi viwili ujifunze namna ya kuvitumia kwa manufaa yako. 

na hasa jinsi ambavyo unaweza kuutumia muda wakoz vizuri. maana ukiweza kuutumia vizuri, utaweza kupata fedha zaidi na muda zaidi.

1. wekeza muda wako  kwenye vitu ambavyo vinaleta asilimia 80 ya kipato chako na kuachana na vile ambavyo vinaingiza asilimia 20 ya kipato chako

 

2. kama ni kipaji unapaswa kuchagua kimoja ambacho utaweka asilimia 80 ya muda wako na huku asilimia 20 ya muda wako ukiutumia kufanya vitu vingine.

 3.  Punguza muda wako kuzurura mitandaoni, badala yake wekeza nguvu zako kwenye kazi za muhimu ambazo inakuingizia kipato.

Hivi ndivyo unapaswa kutumia muda wako. Kuna sheria hii ya pareto ambayo inafahamika kama sheria ya 20/80. Yaani, asilimia 20 ya zile kazi ambazo unafanya ndizo zinakuingizia kipato ambacho ni asilimia 80. Sasa wewe kazi yako iwe ni kuzijua hizi kazi chache ambazo ni asilimia 20 na hakikisha kuwa unawekeza nguvu zako kwenye hizi kazi.

SOMA ZAIDI: Maeneo Sita (06) Ambapo Kila Kijana Mwenye Miaka 20-29 Anapaswa Kuwekeza
umekuwa namo, rafiki yako
Godius Rweyongeza
wasiliana nami kupitia; godiusrweyongeza1@gmail.com
au whastsap au simu; 0755848391
USISAHAU KUSUBSCRIBE KWENYE YOUTUBE CHANNEL YANGU KUPITIA HAPA


One response to “Hivi Ndivyo Unaweza Kutumia Muda Wako Na Fedha Kwa Manufaa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X