Tangu enzi na enzi, asilimia kidogo ya watu wamekuwa wanaiongoza dunia. Watu hawa wamekuwa wanaiongoza dunia kwenye masuala ya uchumi, siasa, biashara, vipaji n.k. na watu ninaowaongelea hapa ni wale ambao wanaonekana kula mema ya nchi. Ukipita mtaani utasikia mtu anasema, aiseeh fulani ana nyota, wewe acha tu.
Watu hawa wamekuwa wakionekana kama wamebarikiwa na Mungu, na wengine wamelaaniwa. Ila kumbe kiuhalisia watu wote wamebarikiwa ila tofauti kwenye matumizi ya Baraka. Wapo ambao wanatumia vizuri baraka hizi hapa na wengine wanazitumia vibaya. Wanazitumia vizuri Baraka ndio wamefanikiwa sana na ndio wanaiongoza dunia, huku ambao wanazitumia vibaya Baraka hizi wakiishia tu kulalamika
Sasa unaweza ukawa unajiuliza ni kitu gani kinaifanya hii asilimia moja kumiliki kila kitu kizuri na wengine kuwa na uhaba wa kila kitu.
Hapa kuna vitu vitano ambavyo wao wanafanya tofauti na wewe unaweza kufanya hivyo pia ili ujiunge nao
1. wanasoma vitabu. Hii ni asilimia moja ambayo ipo tayari kujifunza kitu na kukifanyia kazi. sio tu wanasoma, ila wanafanyia kazi kile wanachosoma. Lengo la kufanyia kazi kile ambacho amesoma ni kupata matokeo ambayo mwandishi anakuwa ameandika. Kwa mfano akisoma kwenye kitabu cha Tajiri mkubwa mjini babiloni kuwa mtu anapaswa kujilipa mwenyewe. Basi anahakikisha amefanya hivyo bila kujali kitu gani kinatokea kwenye maisha yake.
Sasa kama unataka kujiungana kundi hili hapa. basi soma na ufanyie kazi kile ambacho unasoma. Kiweke kwenye matendo mpaka pale utakapopata matokeo ambayo mwandishi wa kitabu husika amesema. Kama hutapata matokeo unaruhusiwa kuachana nacho ili kuendelea na maisha mengine.
2. wanafanya kazi kwa bidii. Watu hawa sio tu kwamba wanafanya kazi. bali wanaenda hatua ya ziada kwenye kufanya kazi. na kitu hiki ndicho kinaitwa kufanya kazi kwa bidii.
3. wanafikiri chanya. Hawa ni watu ambao wanaona chanya kwenye kila kitu. Wanaona fursa ambapo watu wengine wanaona majanga au mabaya. Ni wazi kwamba watu hawa wanakutana na changamoto na matatizo, ila wao hawayaoni hivyo. Wanayaona kama fursa za wao kuzidi kusonga mbele na kufanya makubwa zaidi.
4. wanaungana na watu wengine ambao ni chanya. Watu wa aina hii hawaruhusuu watu hasi na wanaokatisha tamaa waingie kwenye maisha yao. Hata inapotokea ametokea mtu wa kuwakatisha tamaa na kuwarudisha nyuma basi wanawahi kuondoa hiyo hali kwa kusoma vitabu, kusikiliza mafunzo chanya na kusikiliza vitabu vilivyosomwa
5. hawana visingizio. Kama kuna kitu ambacho wanakieupuka ni kuwa na visingizio. Zile stori za sijui sijaweza kufanya hivi kwa sababu nilikosa konekisheni wanazidondoa. Wanajua wazi kwamba konekisheni kwenye maisha unazitengeneza wewe mwenyewe.
Wanajua wazi kwamba kama hutafanyia kazi wazo lako, basi kuna mtu sehemu ambaye atajitokeza na kulifanyia kazi wazo lako. Hivyo wewe utaishia kusikia tu kwenye vyombo vya habari kuwa kijana machachari ambaye amefanya hivyo. Sasa ili kuondokana na hali hiyo, wanafanayia kazi mawazo yao bila kurudi nyuma.
Pia wanajua wazi kwamba kama hufanyii kazi wazo lako, basi ni wazi kuwa utakuwa unasamidia mtu mwingine kufanikisha lengo lake na wazo lake.
6. wanafanya na kutimiza majukumu yao kwa wakati bila kuhairisha
Kama kuna kitu hawa watu wanahairisha,basi ni majumu ambayo hayana umuhimu tu. ila majukumu yote yenye umuhimu wanayafanyia kazi tena kwa wakati na bila kukosa au kisingizio.
Rafiki yangu bila shaka utakuwa umeona jinsi ambavyo kundi la watu wachache wanaweza kuiongoza dunia na kupata mema ya nchi kwa kufanya vitu ambavyo wewe unaweza kufanya. Kinachokutufofautisha wewe na hao wengine ni utendaji kazi. hivyo haya ambayo umejifunza hapa unapaswa kuyaweka kwenye vitendo moja kwa moja bila kuchelewa.