Kama Unataka Kuongeza Kiwango Chako Cha Fedha Zinazoingia Fanya Hivi


Rafiki yangu hongera kwa nafasi ya siku hii ya kipekee. Karibu sana kwenye makala ya leo ambapo tunaenda kuona jinsi ambavyo unaweza kuongeza kiwango chako ch fedha. Na njia hii ni KUWA MAKINI NA KIWANGO KIDOGO AMBACHO UNAPATA SASA HIVI.

Yaani, hiki kiwango kidogo ambacho unakipokea sasa hivi unaweza kukitumia kwa manufaa makubwa ili kuongeza kipato zaidi. Inashangaza kuona kwamba watu wengi huwa wanataka kupata fedha zaidi ila wanadharau kiasi kidogo ambacho wanacho. Kamwe, usifanye hivi. Kadri unavyokuwa na nidhamu kwenye matumizi ya kiasi kidogo ndivyo unazidi kupata kikubwa zaidi. Hivyo, hakikisha kwamba unajijengea nidhamu ya kutumia kiasi kidogo vizuri.

Kama unapaswa kuweka akiba na wewe una kiasi kidogo. usisite kuweka akiba kwa sababu una kiasi kidogo. hakikisha kwamba kuweka akiba unakuwa ni utaratibu wako, bila kujali kuwa upo kwenye hali gani kwa wakti husika.  Kumbuka kadiri unavyokuwa mwaminifu kwenye mambo madogo, hata mambo makubwa yanakuja kwako pia. Hivyo, kuanzia leo hii hakikisha kuwa unakiheshimu kiasi kidogo cha fedha ambacho kinaingia mfukoni mwako. Kitumie vizuri kwa ajili ya manufaa ya sas ahvi na baadae

SOMA ZAIDI; Fedha zako zimelala hapa; Fanya haraka uzichukue kabla hazijachukuliwa

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli,

GODIUS RWEYONGEZA
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X