KULIPA DENI NI LAZIMA SIO OMBI: Njia Zilizothibitishwa Zitakazokusaidia Kulipa Madeni Yako


Habari ya siku ya leo rafki yangu. Hongera sana kwa nafasi ya siku hii ya kipekee. Leo nilipenda nikwambie kuwa kama umejikuta kwenye madeni na kuna watu ambao wanakudai, usiyakimbie hayo madeni. Badala yake jipange kuyalipa. Kulipa madeni ni lazima sio ombi.

Ni wewe ulichukua hatua ya kukopa, unapaswa pia kuchukua hatua ya kulipa hayo madeni. Kama ambavyo mtu huwa unajilipa kwanza kiasi cha asilimia 10 kwa kila kipato ambacho kinaingia. Kuanzia leo anza kujenga utaratibu wa kulipap madeni kwa kufufuata utaratibu huu hapa.

1. kwa kila kiasi unachoingiza jilipe wewe kwanza asilimia 10. Hii ni ile fedha ambayo ni ya kwako na wala hakuna mtu mwingine mwenye umiliki wa hii fedha. Fedha hii sio ya matumizi ya kila siku. Fedha hii sio ya chakula. Fedha hii ni ya kuja kuwekeza hapo mbeleni.

2. waorodhese wadeni wako wote na kiasi ambacho wanakudai. Kisha panga njia ambayo unaenda kutumia ili kuwalipa watu. unaweza kupanga kulipa madeni makubwa kwanza, kisha ukamalizia na madogo. Au unaweza kuanz na madeni madogo na kisha kumalizia na madeni makubwa.

Au unaweza kuanza na wadeni wasumbufu kisha ukamalizia na wale ambao sio wasumbufu

 

4. Tenga asilimia 70 ya kiasi ambacho kinaingia kwa ajili ya matumizi yako ya kila siku. Na usitumie zaidi ya hapo hata kama unakufa.

4. waambie wadeni wako kwamba unaenda kuwalipa kwa mpango ambao umeuweka na utaufuata huo. Waombe wakuvumilie ili uweze kuwalipa taratibu.

5. usikope TENA. Katika kipindi hiki ambacho unalipa madeni, usijiingize kwenye shida za kukopa tena.

KUMBUKA; isitokee siku ambapo utasema kwamba sijilipi mwenyewe kwanza. Hapana. Endelea kujilipa wewe mwenyewe kwanza bila kuacha na hiyo akiba yako usiitume kwa kitu chochote, kile ambacho sio uwekezaji. Ni vizuri unapoanza kuweka akiba kuhakikisha kwamba unakuwa na lengo ambalo linakusukuma kuweka akiba. Kisha kila mara unahakikisha kwamba unafuatilia hilo lengo kuona umefikia wapi.

 

Moja ya kitu ambacho kinawafanya watu wengi wakwame na kuitumia akba yao ni KUKOSA MALENGNO LINAPOKUJA SUALA LA KUWEKA AKIBA. Hivyo kuwa na lengo mahsusi ambalo utalifanyia kazi.

Mfano lengo linaweza uwa ni kuweka akiba ya milioni kumi ndani ya mwaka mmoja. Kisha lifanyie kazi hilo lengo kila siku na usiitoe hiyo fedha yako mpaka pale ambapo utakuwa umeweza kufikish hilo lengo.

TEMBELEA YOUTUBE CHANNEL KWA KUBONYEZA HAPA NA UHAKIKISHE UMESUBSCRIBE

Umekuwa nami rafiki yako, GODIUS RWEYONGEZA

Tuwasiliane kupitia 0755848391.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X