Tafadhal Usifanye Kosa Hili Kwenye Biashara Yako Pale Watu Wanapokuja Kununua (mbinu zilizothibishwa za kumvuta mteja kwako bila kuficha chenji yake)


kitabu hiki ni nakala tete (soft copy) na gharama yake ni 5,000/- tu. tuwasiliane kwa 0755848391 ili uweze kupata nakala yako.

Rafiki yangu karibu sana kwenye makala ya siku hii ya leo. Siku ya leo napenda nikwambie uepuke kosa hili hapa. kosa hili hapa ni pale kukataa kutoa chenji kwa mteja huku ukimwambia aondoke, wakati lengo likiwa ni kuwa baadae arudi aitumie hiyo fedha na fedha yote iishie kwako.

 

Kuna njia nyingi za kumfanya mteja aendelee kuja kwako, ila sio kwa kushikilia chenji yake ili aitumie yote kwako. kwanza nipende tu kukwambia kuwa ni jukumu lako kuwa na chenji kwa ajili ya wateja wako. Sio mteja anakuja na elfu kumi na wewe unaanza kumwambia “elfu kumi yote hiii asubuhi hii”! hivyo, hakikisha muda wote unakuwa na chenji ya kutosha. Na pale inapotokea hauna, hakikisha mteja anaporudi basi unampa chenji yake ila sio unaendelea kumsumbua kwa kumpiga tarehe eti hauna chenji kumbe ipo, ila wewe unataka aitumie yote kwako. baada ya kuwa nimesema hayo sasa, naomba nikupe mbinu za kumfanya mteja aje kwako zaidi bila ya kuficha chenjia ya mteja

1. kwanza kabisa mpe huduma ambayo anapenda, na ini vizuri umpe huduma bora zaidi.

2. mpokee na muage mteja wako kwa uzuri

3. kama kuna kitu anahitaji ila wewe hauna basi mwelekeze kwa uzuri.

4. usilete shida za kifamilia yako kwenye biashara yako. Unapokuwa kwenye biashara hakikisha kuwa unakuwa na sura ya bishara. Sio unanuna kama vile una ugomvi na mtu,

5. hakikisha unapata mawasiliano ya mteja wako kwa ajili ya kuwasiliana naye baadae na siku zijazo.

 

 

Rafiki hayo ni machache kati ya mengi ambayo unaweza kufanya ili kumteka mteja wako. Nikusihi ujitahidi kupata kitabu hiki hapa cha MAMBO 55 YA KUINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA ili uweze kujifunza mengi zaidi kutoka kwenye kurasa za kitabu hiki. Gharama ya kitabu ni 5,000/- tu na  ni softcopy. Tuma fedha kwa 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA,  kisha utanitumia ujumbe wenye neno BIASHARA ili nikutumie kitabu mara moja.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X