Hatua Sita (06)Za Kuufikia Ukuu Kwenye Kazi Yako


 Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii ya kipekee sana.

Watu wengi huwa wanaanza kufanya kitu mwanzoni kwa juhudi kubwa sana. Kuna ambao huwa wanaweza kuendelea kufanya kile kitu kwa muda na baadae kuacha hasa baada ya kukutana na changamoto za hapa na pale. Na kuna wale ambao huwa wanaendelea kwa kusuasua na kufikia hatua ambapo wanaacha kabisa. Rafiki yangu leo hii ningependa nikwambie kwamba kuweza kufikia ukuu kwenye jambo lolote lile ambalo unafanya kwenye maisha sio jambo rahisi. Bali ni jambo ambalo linachukua muda kidogo. Leo hii nitakushirikisha hatua za kuchukua ili kuweza kuufikia ukuu kwenye eneo husika.

Ukuu unaweza kufikia kwenye eneo au sekta yoyote ile ambayo unachagua kwenya maisha. Inaweza kuwa kwenye kazi au kisomo ambacho unacho, unaweza kuwa ni ukuu kwenye kipaji chako, unaweza kuwa ukuu kwenye kitu kipya ambacho unapenda kujifunza kama lugha au kuandika.  Kwa vyovyote vile kitu chochote kile ambacho utachagua kufanya, unapaswa kufahamu kuwa kuna nafasi ya kufikia ukuu.

 

Kama wewe umewahi kufuatilia baadhi ya tamthilia za kichina au kikolea. Basi huwa unakuta kuna mtu ambaye wanamwita MASTER kwenye hizo tamthiliya. Sasa huyu MASTER ndiye tunamzungumzia hapa kwenye andiko letu la leo. Na mwisho tunaenda kuona ni kwa jinsi gani na wewe unaweza kuufikia huo UMASTER

 

1. Kwanza kabisa, unapaswa kuchagua eneo ambalo utaufikia ukuu. Ni wazi kuwa kuna maeneo mengi ambapo unaweza kuufikia ukuu lakini wewe sasa unapaswa kuchagua eneo moja ambalo ungependa kuufikia ukuu.

Kuchagua eneo moja kunakusaidia kuwekeza nguvu zako na muda wako kwenye eneo hilo badala ya kutawanya nguvu na muda wako kwenye maeneo mengi kwa wakati mmoja.

 

2. Pili unapaswa kuanza kujifunza kuhusu hilo eneo. Baada ya kujua eneno ambalo umechagua, kinachofuata ni wewe kuanza kujifunza kiundani kuhusu hilo eneo bila ya kuchoka. Na kwenye zama za ssa hivi kuna taarifa na maarifa mengi ambayo mengi pia yanapatikana bure mtandaoni. Hivyo jifunze kuhusu hili eneo kiundani. Zijue sifa za hili eneo ambalo umechagua.kiufupi lijue hili eneo nje ndani.

 

3. Tatu unapasawa kuchagua mwalimu wako ambaye atakufundisha. Mwanzoni nilikwambia kuhusu tamthililya za kikolea au za kichina ambapo huwa kuna MASTER. Huyu  master huwa unakuta kwamba anafundisha watu wengine ujuzi ambao yeye ameupata kwa miaka mingi kupitia kujaribu kuanguka na kusimama. Wewe unamhitaji mtu wa aina hii kwa sababu hakuna haja ya wewe kuanza kurudia makosa ambayo yeye alishafanya. Badala yake unapaswa kuyaepuka hayo makosa kwa kujifunza kutoka kwake. Mtu wa aina hii hapa anapaswa kuwa mtu ambaye tayari amefikia ukuu kwenye eneo ambalo na wewe ungependa kufikia ukuu.

Mtu wa aina hii pia anapaswa kuwa mtu ambaye atakusukuma kwenda hatua ya ziada. Kuna nyakati ambapo utalazimika kuwa na watu wa aina hii wawili au zaidi kama mmoja ambaye umempata hajakidhi au hana vitu vyote ambavyo wewe ungependa kuwa navyo.

Ukishapata mtu wa aina hii hakikisha kwamba unajifunza kila kitu ambacho anakufundisha na kukifanyia kazi huku na wewe ukiangalia ni namna gani unaweza kuongeza kitu cha ziada au kuboresha kile cha kwake na kukifanya kuwa bora zaidi.

 

4. Nne, toa muda. Kuna muda ambao unapaswa kuwepo kabla ya wewe kuufikia ukuu. Na hapa unapaswa kufahamu kuwa hili sio suala la kulala na kuamka. Kwamba utalala usiku wa leo na kesho kuamka ukiwa tayari umeweza kuufikia  ukuu kwenye eneo hilo. Hapana. Badala yake utahitaji muda wa kutosha kufanya hivyo.

5. Tano, utapasawa kufanya mazoezi. Ya kutosha. Kwa chochote kile ambacho utapenda kuupata ukuu hakikisha kwamba unatoa muda wa kutosha kwenye mazoezi. Fanya mazoezi mengi kadri uwezavyo.  Wataalamu wamefuatilia mara kwa mara na kugundua kuwa ukuu ni jambo ambalo linachukua muda kufikiwa. Na linachukua masaa yasiyopungua elfu kumi. Ambayo ni sawa na miaka saba mpaka kumi. Kwa hiyo utahitaji hiyo miaka ya kuweka kazi na kujifuma zaidi kabla ya kuufikia ukuu kwenye eneo husika

 

6. Sita, unapaswa sasa kutafuta sauti yako. Baada ya kuwa umejifunza kwa huyu MASTER. Na umekuwa chini yake kwa kipindi sasa, kinachofuata ni wewe kutafuta sauti yako wewe hii ndio kusema kwamba, unapaswa kusimama kwa miguu yako yote miwili huku ukitumia ujuzi uliojifunza kwa huyo master na kuongezea vitu vingine vya ziada.

Rafiki yangu, hivyo ndivyo unaweza kuufikia ukuu kwenye eneo husika. Bila shaka lolote utachukua hatua mara moja kuanza kuuendea ukuu kwenye eneo lako ambalo umechagua. Inaweza kuwa ni ukuu kwenye kazi, ukuu kwenya kipaji, ukuu kwenye kazi n.k.

 

Nikutakie kila la kheri

Umekuwa nami, Godius Rweyongeza

Tuwasiliane kupitia 0755848391

Au songambele.smb@gmail.com

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X