Hii Ndiyo Sifa Ya Biashara Ambayo Watu Wengi Hawajui


 

Rafiki yangu bila shaka umekuwa na siku bora kabisa. karibu kwenye makala ya leo ili tuzungumzie sifa ya biashara ambayo ulikuwa hujui. Na sifa hii hapa inakuangusha kwenye biashara yako. Sifa hii ni kwamba biashara huwa inachukua tabia za mwanzislihi au mmiliki wa biashara hiyo.

Unaweza kushangaa kuwa biashara na yenyewe inachukuaje tabia za mtu. Ngoja sasa nikueleze kiundani.

Kwanza ili uweze kunielewa vizuri unapaswa kufahamu kuwa biashara ni kama kiumbe hai. Maana, ina damu yake (ambayo ni mzunguko wa fedha au chashflow kama ambavyo inafahamika. ) biashara pia ina mifumo yake (kama ambavyo mimi na wewe hapo tuna mifumo ya kupumua, mifumo ya damu n.k)

Moja ya mfumo maarufu kwenye biashara ni mfumo wa uongozi. Ambapo kunakuwa na uongozi unaoleweka kuanzia kwa wamiliki wa biashara mpaka kwa mfanyakazi wa chini kabisa. Sasa hawa wafanyakazi, wanapokuja kwenye biashara siku za kwanza wanakuwa hawajui kitu chochote kuhusu taratibu na mwenendo wa biashara yako, wewe ndiwe utakayehusika na kuwaelekeza kila kitu kuhusu biashara hiyo. Unapaswa kukitumia vizuri kipindi hiki mfanyakazi anapokuwa mgeni kuhakikisha kwamba unamwelekeza kwa kina kuhusu utendakazi wa biashara na miiko yote ya biashra yako. Na hili hupaswi kulifanya tu kwa maneno, bali kwa vitendo pia.

 

Baada ya kipindi hicho cha ugeni kuisha huwa kinafuata kipindi ambacho mfanyakazi anakuwa tayari ana uzoefu wa kazi. Kama kwenye kipindi cha kwanza ulimwelekeza vizuri, basi kwenye kipindi hiki hapa atachapa kazi na kukuletea matokeo mazuri. Kama hukumwelekeza vizuri, basi hii itapelekea kwa kipindi cha tatu ambapo kwenye kipindi hiki anaanza kuiga na kutendea kazi zlie tabia zako na hivyo kuifanya biashara yako idolole.

 

Hivyo basi, wewe kama mwanzilishi au mmiliki wa biashara unapaswa kuwa na mfumo fulani wa maisha ambao unaufuata kwenye biashara yako. Na taratibu zote za biashara unapaswa kuwa mtu wa kwanza kuhakikisha kwamba unazifuata bila kisingizio chochote kile. Ukiweza kufuata taratibu na kununi zote ambazo ungependa kuona wengine wanazifanyia kazi basi ni wazi kuwa na wao watazifuata.

Kwa hiyo kama unataka watu wawahi kwenye kazi, wewe kuwa mfano.

Kama ungependa kuona watu wakifanya kazi kwa uaminifu, basi wewe anza kuonesha huo uaminifu.

Kama ungependa kuona watu ni wabunifu, basi wewe anza kujenea mazingira ya kibunifu.

Kama ungependa kuona watu wanachukua hatua za tofauti, wewe kuwa chanzo

Kama ungependa kuona wanatatua changamoto kwa weredi, wewe kuwa chanzo cha kufanya hivyo.

 

Rafiki yangu, biashara huwa inabeba tabia za mwanzilishi wake au mmiliki wa biashara hiyo. Nikusihi sana, kuanzia leo hii kuhakikisha kwamba unaonesha tabia ambazo ungependa kuziona kwenye biashara yako.

 

Umekuwa name rafiki yako wa kweli,Godius Rweyongeza

Tuwasiliane kupitia 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X