Rafiki yangu kuna vitu ambavyo vinalipa ukvifanya kwenye hiii dunia. Moja ya kitu ambacho kinalipa kufanya ni kukumbuka majina ya watu.
Majina ya watu usiyachukulie poa hata kidogo. watu wanapenda kukumbukwa kwa majina yao. Nadhani wewe ni shahidi wa hil hapa. kila mara unapokutana na mtu ambaye ulishamwambia jina lako ila sasa anaonesha dalili kuwa halikikumbuki, kitu cha kwanza ambacho utafanya ni kumwuliza. Umesahau jina langu. Hakuna mtu ambaye huwa anapenda jina lake lisahaulike. Na pale mtu napokuwa amesahau jina lako basi hata kama hutamwabia basi ni wazi kuwa unaenda kusitika ndani kwa ndani.
Ila hali huwa ni tofauti pale ambapo utafika sehemu na kuita jina la mhusika moja kwa moja hata kama hamjawahi kukutana. Huyu mtu ataanza kujenga hali ya udadisi kutaka kujua nani amekwambia jina lake. Na hapo ndipo maongezi yenu yanaanzia.
Watu huwa wapo makini sana jina lao linapotajwa. Hii huwa inaonesha yule ambaye anataja jina lake anajali. Hivyo muda mwingine unapoongea na watu jitahidi kutaja jina la mtu na hasa pale anapokuwa amejitambulisha kwako mara ya kwanza.
Kuna kitu nataka nikuelekeze hapa kuonesha kwamba watu wapo makini na majina yao. Mnaweza kuwa kwenye kundi kubwa la watu ambao wanapiga kelele mfano kwenye sherehe. Sasa kwenye sherehe hiyo kukawa na vikundi mbalimbali vya watu ambapo kila kikundi kinashughulika na kuongea mambo yake. Lakini pale inapotoke kwenye kikundi kimoja likatajwa jina la mtu ambaye yuko sehemu nyingine ila alikuwa hasikilizi yale maongezi atastuka. Yaani, kutajwa jina lake tu inakuwa kama ndio ametolewa usingizini. Maongezi ambayo hapo awali yalikuwa chini, sasa anaanza kuyasikia na kuyafuatilia vizuri kwa sababu tu lilitajwa jina lake. Hiii ni dalili tosha kuonesha kwamba watu wapo makini na majina yao, hivyo na wewe usiyachukulie poa majina ya watu.
Mambo yamuhimu ya kufanya ili uweze kukumbuka majina ya watu.
1. kila mara unapokutna na mtu hakikisha kwamba unamwuliza jina lake.
2. akishakwambia jina lake hakikisha kuwa unalitumia mara nyingi kwenye mazungumzo yako.
3. pale unapoaga mtu ambaye amejitambulisha kwako mara ya kwanza hakikisha unamuaga kwa jina lake.
4. kama mtu amejitambulisha kwako na jina hujalisika vizuri muombe alitamke vizuri ili ulisikie. Usiogope kufanya hivyo.
5. siku zote hakikisha unamwuliza mtu jina lake siku ya kwanza mnapokutana badala ya kusubiri pale mnapokuwa mmekutana zaidi ya mara tano.
6. Mtu akikwambia jina ambalo linakushinda kuliandika basi omba akwambie jinsi ambavyo linaandikwa.
7. ukifika nyumbani kila siku jioni jikumbushe majina ya watu wapya ambaoumekutana nao ndani ya siku
husika. Kisha yaandike majina hayo kwenye diary yako.
8. kuwa makini sana watu wanapotaja majina yao kwako. umakini wako unaweza kukufanya ukumbuke majina ya watu kwa asilimia 50.
9. Kama mtu ana cheo mwite kwa cheo hicho ambacho anacho
10. HAKIKISHA unasikia jina la mtu linapotajwa kwako mara ya kwanza. Watu wengi husahau majina kwa sababu hawakuyasikia pale yalipotajwa kwao mara ya kwanza kabisa. na unakuta kuwa aliyekuwa anafanya utambulisho mwenyewe alikuwa hakummbuki hilo jina. Hivyo analitaja kijanja, kijanja bila kusikika na wewe unaitikia tu kuwa umefurahi kukutana na huyo mtu, kumbe jina lake hujalisikia. Hiki ndio huwa kinawafanya watu wengi waseme kwamba wanakumbuka sura ya mtu ila sio jina lake. Sijawahi kuona mtu anasema eti jina lako nalikumbuka ila sura yako siikumbuki.
11. kamwe usije ukachukulia poa kuwa huyo mtu anayetambulishwa kwako hutakuja kukutana naye tena maishani mwako. Utashangaa siku nyingine unakutana na huyo mtu na wewe ndio huelewi kabisa kitu cha kufanya. Jitahidi mara zote kuhakikisha unakumbuka majina ya watu. maana siku na muda ambao hutegemei ndio utakutana na mtu huyo.
*JINSI YA KUULIZA JINA LA MTU KAMA UMESAHAU*
Unaposahau jina la mtu inakuwa inaonesha kuwa hujali. Hata hivyo inaweza kutokea kwamba umesahau jina la mtu. Sasa hapa ninapenda nikuelekeze
Kama umeshau jina la mtu njia bora ambayo unaweza kutumia ili akwambie jina lake ni kumwambia kuwa unaomba akukumbushe jina lake, sasa mtu atakapotaja jina la kwanza, mwambie hapana, siwezi kusahau hilo, nilitaka unikumbushe jina lako la la pili au akitaja la pili unamwabia hapana nilikuwa nataka kusikia hilo la kwanza.
Kwa mfano ukishau jina langu. Utaniomba nilitaje jina langu. Mimi nitakwambia naitwa GODIUS. Utasema hapana nilitaka kusikia la pili. Nitasema tena RWEYONGEZA. Huwa inaonesha kuwa
ulisahau jina moja tu, walau inafunika ile ya kutojali kabisa.
Hata hivyo njia hii huwa haifanyi kazi muda wote. Kuna mtu mwingine unaweza kumwomba akutajie jina lake akataja yote bila kuacha hata moja. hapho sasa sijui utasemaje?
Kuna watu ambao huwa wanatumbia mbinu hii ili watu wawakumbushe majina yao, ‘ utasikia mtu anasema, afu wewe jina lako ni gumu kweli, ebu nikumbushe. Afu mtu ndio anaanza kutiririka na wewe unaweza kutumia tena njia ya hapo juu kujisafisha.
Rafiki yangu, kwa vyovyote vile uanapaswa kufahamu kuwa inalipa sana kuyajua majina ya watu. ujiondoe kwenye orodha ya watu ambao wnalalamika kuhusu kukumbuka sura za watu ila sio majina.
Nakutakia siku njema.