Jinsi Ya Kujiimarisha Kifedha Katika Hali Zote Unazopitia


ni haki yako kuwa na fedha kwa kiwango
chochote unachotaka

Kuna mchezaji mmoja ambaye alikuwa anajifunza vizuri sana kuhusu mbinu za mchezo wa masumbwi ila alipokuwa anaingia uwanjani na kupigwa ngumi moja, alikuwa anapteza ule uwezo wake wote na hivyo kuanza kucheza kwa hisia kama vile hajawahi kujifunza mpira maishani mwake.

 

Kitu kama hiki hapa kimekuwa kinawakumba watu kwenye mchezo wa maisha na hasa kwenye mchezo wa fedha. Yaaani, watu wanajifunza kuhusu fedha na hasa kuweka akiba. Ila unakuta kwamba mtu baada ya kuweka akiba mara mbili au tatu, basi anasahau mbinu za kutunza na kutumia feha na badala yake anaanza kutumia fedha kama ambavyo alikuwa amezoea.

 

Au mwingine anaanza vizuri kuweka akiba ila inatokea siku moja ambapo anauwa njaa, basi anaitumie ile fedha yote bila kuacha. Leo hii hapa ningependa ujifunze jinsi ambavyo unaweza kuepuka hali kama hizi hapa ili uweze kutunza akiba yako bila shida yoyote ile.

 

Moja, hakikisha unajifunza kuhusu fedha kila siku. Na kuendelea kufanyia kazi kile ambacho unajifunza kila siku. Unaposoma kuhusu fedha unapata hamasa ya kuchukua hatua, lakini hiyo hamasa inaweza isidumu. Hivyo ili kuifanya hiyo hamasa iweze kudumu unapaswa kujifunza kila siku kuhusu masuala ya fedha bila kuchoka.

Kitu muhimu unachopaswa kufahamu ni kwamba hakuna shule ambayo inafundisha kuhusu fedha. Hivyo ni jukumu lako kujiendeleza kuhusu fedha na kuhakikisha unaijua kiundani zaidi na jinsi ambavyo inafanya kazi.

 

Pili, Epuka kutumia fedha ambayo tayari umeweka akiba. Na utaweza kuepuka hili kama fedha hiyo utaiweka kwenye gereza ambalo huwezi kuifikia kwa haraka. Kwa mfano, kuweka fedha kwenye akaunti ya mpesa ambayo wewe mwenyewe hauna namba za siri za kuitolea. Na unaweza kufanikisha hili hapa kwa kumpa rafiki yako au mtu wako wa karibu nafasi ya kukuwekea namba ya siri ila wewe ukabaki na laini. Kwenye laini hiyo utaendelea kuweka fedha bila kuchoka mpaka pale utakapokuwa umeweza kufikia lengo lako, ndipo hapo unaweza kumwomba rafiki yako akupe namba ya siri ili utoe hiyo fedha ili uweze kuitumia hiyo fedha kwenye uwekezaji.

 

Rafiki yangu hizo ndizo mbinu ambazo zinakuwezesha wewe kutunza na kuitumia vizuri kwenye nayakati zozote zile. Nakutakia siku njema sana. endelea kutembelea blogu hii hapa kila siku ili uweze kujifunza kila siku  mambo muhimu kama haya

 

Umekuwa name rafiki yako wa ukweli, GODIUS RWEYONGEZA

Tuwasiliane kupitia 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X