Kitu kingine ambacho kinawafanya watu wawe masikini ni kukosa jicho la kuziangalia fursa. Yaani, kila fursa zinapojitokeza basi wao wanazipita na hata kutoziangalia kwa jicho la fursa. Hata hivyo, halil ni tofauti kwa matajiri. Kila inapojitokekza fursa wao wanahakikisha kwamba wanaitumia vizuri. Na fursa huwa zinakuja katika namna tofautitoauti. Fursa kuptIia matatizo ambayo unakumbana nayo au ambayo jamii inakumbana nayo. Fursa inaweza kuja kupitia watu ambao unakutana nao (iwe ni ana kwa ana au kupitia mitandaoni.
Unachopaswa kufahamu ni kuwa
1. fursa hazina muhuri wowote ule.
2. fursa hazipigi kelele sana. wapo wanaosema kwamba fursa huwa haigongi mlango mara mbili. ila uhalisia ni kuwa fursa huwa haigongi mlango kabisa.
3. vitu ambavyo vinaonekana sana kwa watu kama fursa mara ngingi huwa sio fursa. Kama kila mtu anaona hicho kitu kama fursa wewe achana nenda katafute sehemu nyingine.
4. fursa huwa hazipigiwi kelele sana. ukiona watu wanapiga kelele na kukushawishi kuwa hiyo ni fursa epukana na hicho kitu.