Siku zote ni matendo yana nguvu kubwa kuliko maneno. unaweza kuwa na elimu na unajua vitu vingi lakini kama hutumii hiyo elilmu katika kuhakikisha kwamba unasonga mbele, basi ni wazi kuwa hiyo elimu haitakuwa na msaada wowote kwako. hivyo moja ya kosa ambalo watu wanafanya ni kujifunza kuhusu fedha na kutoafnyia kazi kile ambacho wao wanajifunza,
Mtu anajifunza kwamba anapaswa kuweka akiba ila bado haweki akiba. Na bado mtu huyu anaendelea kuhangaika linapokuja suala la fedha. Kumbuka kwamba kitendo kimoja ni bora kuliko maelfu ya maneno. haitoshi tu wewe kujifunza kuhusu fedha. Badala yake unapaswa kuweka katika vitendo kile ambacho umejifunza.
Linapokuja suala la kuchukua hatua huwa napenda kutolea mfano wa kitabu cha TAJIRI MKUBWA MJINI BABILONI. Kwenye kurasa za kitabu hiki mwandishi ameeleza kwamba unapaswa kujilipa wewe mwenyewe. Na kiwango cha kujilipa wewe mwenyewe ni asilimia 10. Sasa wewe unapaswa kufanya hivi kila unapopokea fedha bila kujali ni jumatatu, au jumapili. Bila kujali kwamba inanyesha siku hiyo au ni baridi. Kitu pekee unachopaswa kuwa nacho kwenye akili yako ni kwamba kila unapopokea fedha basi unapaswa kutoa asilimia 10 na kujilipa wewe mwenyewe. Hiyo ndiyo nguvu ya vitendo. Usiipuziie, maarifa bila vitendo hayatakufaa.