MAKOSA 50 AMBAYO WATU HUFANYA KUHUSU FEDHA: KOSA LA #3 KUDHARAU UTARATIBU WA KUWEKA AKIBA


 

 

Asilimia kubwa ya watu wamekuwa wanaamini kwamba ukipokea fedha inakuwa ni ya kwako yote. Hivyo wanatumia kadiri watakavyo. Hata hivyo ukweli ni kuwa fedha unayopokea leo sio ya kwako yote. Wewe unakuwa kama umeshikilia fedha ya watu wengine kwa muda. Maana baada ya hapo utaenda kununua chakula, nguo, vinywaji, na matumizi mengine.

Kwa kufanya hivyo utakuwa unawakabidhi hao watu wengiine fedha zao na mwisho wa siku utakuta kuwa umebaki bila kitu chochote kile.

 

Kama unataka kutengeneza utajiri, basi utapaswa kuweka utaratibu wa kuweka akiba. Na kiwango cha kuweka akiba ni kidogo sana. yaani, asilimia 10 ya kile kipato chako ambacho kinaingia mfukoni.  Ni wazi kuwa itafikia hatua ambapo  kiwango chako cha fedha kitaongezeka na wewe kuanza kuingia kwenye ulingo wa matajiri.

 

Ukishatoa akiba yako ambayo ni asilimia 10 ya kile pesa unayopokea, kinachofuata ni wewe kuhakikisha kuwa matumizi yako yote hayawi makubwa kuliko hicho kiasi ambacho kimebaki. Kumbuka akiba sio kwa ajili ya kununua chakula, akiba sio kwa ajili ya nguo za mtoko, akiba sio kwa ajili ya kusherehekea. Akiba inapaswa kutumika kuwekeza au kuanzisha chanzo cha ziada cha kipato.

Kama mpaka sasa hivi umekuwa hupati msukumo wa kuweka akiba hizi hapa zinaweza kuwa sababu za kuanzia kwako wewe kuweka akiba.

1. weka akiba kwa ajili ya lengo lako au ndoto yako ya sasa hivi.

2. weka akiba ya fedha ya ambayo unaweza  kutumia kwa miezi 6 mfululizo kama itatokea vyanzo vyako vya sasa hivi vimekwama. Unapaswa kuwa na fedha ya aina hii hapa. yaani, fedha ambayo kwa miezi sita unaweza kutumia hata kama hufanyi kazi.

Je, wewe unaweka akiba?

Nikutakie siku njema sana

BONYEZA HAKA KUSOMA KOSA LA PILI

PATA KITABU CHA MAAJABU YA KUWEKA AKIBA ili uweze kujifunza kuhusu jinsi kuweka akiba kunavyoweza kubadili maisha yako kiujumla. Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu 4 tu. tuma fedha kwenda 0755848391.baaada ya hapo utanitumia ujumbe ili nikutumie kitabu.

Kitabu hiki ni nakala laini.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X