MAKOSA 50 AMBAYO WATU HUFANYA KUHUSU FEDHA : KOSA LA KWANZA; Kutokuwa na kipaumbele cha kujifunza kuhusu fedha


Inashangaza kuona kwamba watu wanaamka kila siku kwenda kutafuta kufanya kazi kwa siku tano au sita za wiki. Na kurudia ratiba hiyo mwaka hadi hadi mwaka. Lengo lao kufanya kazi ni kutafuta fedha ila hawachukui muda wa kujifunza kuhusu kile ambacho wanakitafuta, ambacho ni FEDHA.

Kitu hiki ndicho kinawafanya watu wengi wazidi kuhangaika kwenye masuala ya kiefdha mwaka hadi mwaka. Hivyo basi ni juu yako kuhakikisha kuwa unawekeza zaidi kwenye kuzijua fedha na jinsi zinavyofanya kazi kila siku ya maisha yako. Kamwe usihititmu.

Nimekuwa nikiwaambia watu kwamba walau kila mwezi unapaswa kusoma kitabu kimoja kinachohusu fedha. Na hivyo kwa mwaka tunatarajia kwamba uwe umesoma vitabu 12. Kwa miaka ambayo unayo sasa hivi, basi ni wazi kuwa inategemewa uwe umsoma vitabu 12 kuzidisha miaka uliyo nayo. Hivyo ni vitabu kuhusu fedha tu wala sio kitu kingne.

Je, wewe umesoma vingapi?

 

PATA KITABU CHA MAAJABU YA KUWEKA AKIBA ili uweze kujifunza kuhusu jinsi kuweka akiba kunavyoweza kubadili maisha yako kiujumla. Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu 4 tu. tuma fedha kwenda 0755848391.baaada ya hapo utanitumia ujumbe ili nikutumie kitabu.

Kitabu hiki ni nakala laini.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X