Kuna vitu katika maisha ya kila siku ambavyo watu huwa wanachukulia poa, ila japo vina uzito mkubwa sana. wapo wanaofanya hivi kwa kujua. Eubu chukulia vitu kama kuvuta hewa ya oksijeni. Ni kitu cha kawaida ambacho pengine unaweza kupitisha wiki bila kuona umuhimu wake au hata kujua kama unapumua, ila pale ambapo mtu anaumwa na kupelekwa hospitali na kutakiwa kulipia gharama kubwa kwa ajili ya kitu ambacho siku zote amekuwa anachukulia poa, hapo ndipo mtu anatambua wazi kwamba OKSIJENI sio kitu cha kawaida.
Vipo vitu vingi ambavyo watu huchukulia poa ila vina maana kubwa kwenye maisha. Labda zamu hii niseme kitu kama mswaki na dawa ya meno. Inawezekana ni kitu ambacho hujawahi kuona umuhimu wake maishani mwako. Hata hivyo ni vitu vyenye umuhimu mkubwa usisubiri upoteze vitu hivi vidogo ili uanze kuvithamini. Anza leo hii kuvithamini.
Inashangaza kuona kwamba watu huwa hawaoni thamani ya kitu mpaka pale ambapo wanakuwa wamekipoteza. Olumide Emmanuel kwenye kitabu cha chake 50 THINGS YOU SHOULD NEVER TAKE FOR A GRANTED. Ametueleza hivi vitu 50 ambavyo hupaswi kuchukulia poa kwenye maisha. Kwenye uchambuzi huu hapa tunaenda kuona kitu kimoja baada ya kingine. Kwa ufupi. Ukitaka kusoma zaidi tafadhali jipatie kitabu chenyewe na maelezo na kukipakua bure nimeyaweka mwishoni mwa andiko hili hapa. wakati unaendelea kusoma uchamabuzi utagundua kwamba kuna baadhi ya vitu nimeviruka. Hivyo vichache vilivyorukwa utavikuta kwenye kitabu.
Kwa wale ambao wapo kwenye mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu basi tayari wameshatumiwa kitabu hiki hapa cha OLUMIDE EMMANUEL, hivyo utaratibu ulio mwishoni mwa andiko hili hapa hauwahusu, badala yake wanapaswa kuingia kwenye barua pepe zao ili kuchukua kitabu chenyewe. Sasa baada ya maelezo hayo hapo, hivi hapa ni vitu 50 ambavyo watu huchukulia poa.
1. WATU
Hakuna mtu ambaye ni kisiwa. Yaani, anajitegemea yeye mwenyewe kwa asilimia 100. Tunaishi katika ulimwengu ambapo tunashirikiana na watu wengine. Ukitaka kusafiri ni wazi kuwa utampigia bodaboda au mtu wa taxi simu, kabla ya kupiga simu utahitaji vocha ambayo inauzwa dukani, na anayeuza humo ni mtu. Vocha hiyo imetengezwa sehemu na watu, simu pia imetengewa sehemu nyingine na watu. Hivyo, usichukulie watu ambao unakutana nao poa hata kidogo. hata wale ambao hujakutana nao usiwachukulie poa.
Kiufupi hawa watu ndio wanakuweka mtaani na kukufanya ufurahie mema ya dunia. Unavaa nguo kwa sababu zimetengenezwa na watu wengine. Umekalia kiti ambacho kimetengenezwa na watu wengine. Unaandikia kalamu ambazo wamtengeneza watu wengine…orodha ni defu.
Usiwachukulie poa watu wengine.
2. MAENEO/SEHEMU
Siku za hivi karibuni kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, ni wazi kuwa kuna maeneno ulikuwa unaenda sasa huwezi kwenda kama ambavyo ulikuwa ukienda hapo zamani. Inawezekana haya maeneo ulikuwa unayachukulia poa, ila baada ya kukosa kwenda maeneo haya kwa kipindi hiki basi hutaendelea kuyachukulia poa.
3. MAJUKWAA
Majukwaa ambayo unapata kwenye maisha yako usiyachukulie poa. Yana nguvu ya kukuletea fursa ambazo hukutegemea maishani mwako. Tena kwa sasa hivi tupo kwenye zama ambapo unaweza kupata nafasi ya jukwaa ukiwa nyumbani kwako. majukwaa kama facebook, instagram, twitter n.k. sio ya kuchukulia poa hata kidogo.
Na yale majukwaa ambayo watu wengine wameandaa na kukualika, usiyachukulie poa. Kwa mfano semina ambayo umealikwa kutoa neno. Hakikisha kwamba unayatumia vizuri kwa kutoa kitu cha thamani ambacho kitawanufaisha wale watu
4. UWEZO
Usichukulie uwezo ulio nao sasa hivi poa. Utumie vizuri kwa manufaa yako na wengine bila kumuumiza mtu kwa sababu ya uwezo wako.
Nadhani walau umewahi kusikia hadithi ya watu waliokuwa wakiwatesa wengine. Na ikaja kutokea baadae maishani wale watesaji wakawa waombaji msaada kwa wale waliokuwa wanateswa. Utumie uwezo wako wa sasa hivi vizuri.
Kama umemwajiri mfanyakazi wa ndani sasa hivi na una uwezo, usimchukulie poa hata kidogo.
5. namba tano imeunganishwa na namba 32.
6. SERA
Sera ambazo umeweka kwenye biashara yako au kampuni yako, hakikisha kwamba unazifuata. Kuzikiuka hizi sera kunaweza kuwa na madhara makubwa ambayo yatakuletea shida.
Kama una sera za kuajiri, basi zifuate hizo hapo. uzichukulie poa
7. UWEPO
Usichukulie uwepo wa watu poa. Kuna baadhi ya watu ambao uwepo wao ni wa muhimu sana kwako katika kufanikisha malengo yako. Usiwachukulie poa.
8. POLISI
Katika jamii nyingi polisi hawapendwi. Ukitaja polisi picha inayokuja kwenye akili za watu ambao wanapiga, kukanyaga na kuweka watu jela, kunyanyasa n.k. hata hivyo picha hiyo inapaswa kukukumbusha kuwa wewe haupaswi kuwa mtu wa maovu kwenye maisha yako. Hivyo usiwachukulie poa.
Lakini pia usiwachukulie poa maana wao ndio wanalinda usalama wako hata pale ambapo wewe unaenda kulala. Au unapotembea unakuwa hauna hofu ya kitu chochote kibaya kitokee kwako. hivyo usiwachukulie poa.
9. KUSUDI
Kusudi la maisha yako usilichulie poa. Kuna watu ambao huwa wanaishia kuumia baada ya kughairisha kile ambacho walipaswa kuwa wamefanya kwenye maisha yao. Hivyo wanafikia mwisho wa maisha yao wakiwa na majuto mengi. Maisha yako yanapaswa kuwa na kusudi ambalo linakusukuma wewe muda wote kufanya kitu kikubwa zaidi. Kukosa kusudi tu kunaweza kukufanya ufe kabla ya wakati wako. Ndio maana kuna wastaafu wengi wanaaga dunia siku chache baada ya kustaafu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi hicho wanakuwa hawana kusudi lolote lile la kuishi. Hivyo usichukulie poa kusudi la maishayako.
10. WATEJA
Usiwachukulie wateja wako poa maana wana nafasi ya kukutangaza zaidi wewe kwa mtu mwingine na hivyo kukuongezea idadi zaidi ya watu ambao wanakuja kwako. lakini pia wana nafasi ya kuharibu jina lako na kuwafanya watu wengine wasije kwako.
Pia usidharau mtu ambaye unakutana naye kwa kumwangalia. Kila mtu ana mzunguko wake wa watu ambao unaweza kuwa wenye manufaa kwako pia.
11. SALA
Usichukulie poa sala. Unaweza kupata kile ambacho unataka maishani mwako kupitia sala. Hivyo uzischukulie poa. Kuna watu ambao wanakosea kuhusisha sala na dini. Sala inaweza kusaliwa na mtu yeyote bila kujali dini yake ni ipi. Kujua zaidi kuhusu masuala ya sala. Na kusali kisanyansi katika namna ambayo itakupa majibu basi nakushauri usome kitabu cha THE POWER OF THESUBCONSIOUS MIND
13. UWEZO NA UWEZEKANO
Usichukulie poa uwezo na uwezekano maishani mwako.
Kila mimba ina uwezo wa kutoa mtoto pale ambapo itatunzwa vizuri. Lakini pia ina uwezekano wa kutolewa endapo haitatunzwa vizuri.
Kila mwanafunzi ana uwezo wa kufanya vizuri endapo atasoma kwa bidii na kila mwanafunzi ana uwezekano wa kupoteza nafasi yake ya masomo endapo hatasoma kwa bidii.
Kila mahusiano yana uwezo wa kutoa ndoa nzuri endapo ytatahaminiwa, na wakati huo huo kila mahusiano yana uwezo wakuharibika na kuumiza wahusika endpo hayathaminiwa.
14. MATATIZO
Moja ya kitu ambacho unapaswa kukithamini ni matatizo ambayo unakutana nayo. Ni matatizo ambayo yanatufanya tukue maana bila matatizo tusingekua. Matatizo ndiyo yamesababisha uwepo wa bishara. Matatizo ndiyo yameleta uvumbuzi na ugunduzi. Matatizo ndiyo yamefanya watu wabadili maish yao na kuanza kufanya vitu vya kusonga mbele. Hivyo usichukulie poa matatizo hata siku moja.
15. USAFI
Kukosa usafi kumewafanya viongozi wa siasa, dini na wale waliokuwa wakiheshimika kuhaibika, kuburuzwa kortini, kuhukumiwa na wengine kufilisiwa. Usichukulie poa suala la kuwa msafi. Kumbuka hapa sizungumzii unadhifu bali usafi. Unahitaji kuwa safi kiwmili, kiroho n.k
Achana na utapeli, ufisadi, rushwa, uzinzi….
Kama utapata mafanikio ambayo hayajajengwa kwenye misingi ya usafi. Unaweza siku moja ukaangushwa kwa sababu ya kitendo kimoja kichafu ulichofanya.
16. KANUNI
MAISHA yanaongozwa na kanuni. Ukizifahamu kanuni ambazo zinaogoza eneo lako basi utafanikiwa sana. tukuchulie mfano wa kanuni ya utavuna ulichopanda. Kanuni hii ipo hivi. Na usitegemee kwamba itabadilika hata siku moja.
kanuni hizi zimekuwepo tangu mwanzo wa uwepo wa dunia
zina umri kuliko wewe hapo
zinafanya kazi ulimwenguni kote, iwe ni mashariki au magharibi.
Zinafanya maisha yatabilike
Usizichukulie poa. Jifunze kanuni kwenye eneo lako la kazi
17. MZUNGUKO WAKO
Mzunguko wako unaweza kukuinua au kukuangusha. Hivyo usichukulie poa mzunguko wako.
Mzunguko wako unaweza kukusaidia katika kutimiza ndoto zako. Unaweza kukusaidia kukushikilia pale ambapo hujatimiza mipangoyako, unaweza kukusaidia kukuonesha fursa ambayo inaendana na mipango yako, unaweza kukusaidia kwenda mbali zaidi.
Lakini pia mzunguko wako unaweza kukufanya ujione kwamba hauwezi, unastahili kuishi maisha ya kawaida, mafanikio ni ya watu wachache n.k.
Mzunguko wako usiuchukulie poa.
21. BIDHAA
Usichukulie bidhaa unazoziona poa. Kitu kama sanitizer au barakoa kilikuwa kinachukuliwa poa kabla ya virusi vya corona. Ila sasa kinachukuliwa kwa umuhimu mkubwa sana. baadhi ya bidhaa zilikuwa hazinunuliwi kwawingi ila ilipoingia hofu ya corona miongoni mwa watu wakawa wanakimbizana kuzinunua kwa wingi. Usichukulie bidhaa poa.
22. GHARAMA
Usichukulie poa gharama. Kuna wakati utapaswa kulipa gharama kubwa ili kuonesha kuwa hicho kitu unakithamini sana. mafanikio makubwa na utajiri vinahitaji gharama kubwa pia. Hivyo utapaswa kuilipa.
Siku zote gharama ambayo upo tayari kukipa huonesha thamani ambayo unakuwa tayari kuipata. Ukilipa kidogo, utapata thamani kidogo, ila ukilipa gharama kubwa utapata thamani kubwa.
Ukichukulia gharama poa itakuletea shida kwenye biashara na maisha yako.
23. MATANGAZO
Bila shaka leo sio mara yako kwanza kusikia kwamba bishara ni matangazo. Hata hivyo watu wemekuwa wanachukulia poa kitu hiki. Haijalishi utatengeza bidhaa nzuri kiasi gani kama hutaitangaza utaishia kupata mauzo hafifu. Ila bidhaa mbovu ikitangazwa itapata mauzo makubwa na bidhaa bora ikitangazwa itapata mauzo mengi zaidi. Ni wewe tu, kuchagua kusuka au kunyoa.
Pia watu wanapokutangaza, usichukulie hiyo nafasi poa. ITHAMINI.
24. KUWASILISHA
Unapopata nafasi ya kuwasilisha kitu kwa watu, basi hiyo nafasi usiichukulie poa hata kidogo. ukipata nafasi ya kuongea mbele ya watu, itumie vizuri usiichukulie poa
Ukipata nafasi ya kuimba, usiichukulie po.
Ukipata nafasi ya kuandika au kuongea kwenye redio usiichukulie poa
25. KIFUNGASHIO
Nadhani umewahi kusikia watu wakisema usihukumu kitabu kwa mwonekano wake. Hata hivyo katika zama za sasa hivi mwonekano una maana kubwa. Mwonekano mbaya unawez akufanya upate mauzo kidogo na mwonekano mzuri unaweza kukufanya upayte mauzo mauzuri.
Katika zama za sasa hivi hata bidhaa feki zinapewa vifungashio vizuri ili ziuzwe, sasa wewe ni nani mpaka usifungashe bidhaa zako kwa umaridadi?
Ni kitu kidogo ila usikichukulie poa.
26. FAIDA
Hiki ni kitu kingine ambacho unapaswa kukifuatilia kwenye kile ambacho unafanya. Biashara nyingi huwa zinakufa ndani ya miaka mitano baada ya kufunguliwa kwa sababu ya kukosa mauzo mazur. Hivyo usikukbali kuacha kitu hiki kipite tu.
Hakikisha kila mara unafuatilia faida kwenye biashara, mahusiano,uwekezaj n.k. popote pale ambapo unaona uwekezaji ni mkubwa kuliko matokeo, basi ujue hiyo SIO HABARI NJEMA
28. MAENDELEO BINAFSI
Kuna vitu ambavyo unaweza kuwa unavifanya sasa hivi ila watu wanachukulia poa, ila siku vikianza kukulipa basi watabaki wanashangaa tu. vitu kama kusoma vitabu, kuhudhuria semina na kulipia baadhi ya kozi. Huwa napenda kuwatolea watu mfano wa kujenga msonge na ghorofa. Mjenziwa msonge anaweza kumaliza ujenzi wa wake ndani ya siku moja na kuanza kuishi maisha yake kwenye makazi mapya. Ila wa ghorofa ndio kwanza anakuwa ameanza hiyo safari yake. Lakini anapomaliza baada ya siku nyingi, basi utofauti unakuwa unaonekana kwa macho tu.
Hivyo usichukulie poa maendelea binafsi . fanya maendelea binafsi kuwa kitu ambacho utakifanya maisha yako yote.
30. AFYA YAKO
Kuna watu ambao huwa wanachukulia afya poa. WANAFANYA VITU AMBAVYO VINAPOTEZA AFYA Kiasi kwamba wakishaipoteza afya yao ndio wanakumbuka kuitunza, tena kwa gharama. Usiichukulie poa afya yako, hakikisha unaitunza muda wote. Siku ukiipoteza utakuja kuitafuta kwa gharama kubwa na pengine usiipate
32. NAFASI/FURSA
Hivi ni vile vitu ambavyo katika maisha unapata nafasi ya kuwa navyo au kushikilia. Inashangaza kuona kwamba mtu mmoja anahangaika kutafuta kitu fulani katika wakati fulani kwenye maisha wakati huohuo mtu mwingine anakipoteza kitu hcho.
Mtu ambaye hana ajira anahangaika kutafuta nafasi ya kuajiriwa ili aweze walau kupata sehemu ya kuanzia na kutoka kimaisha. Wakati yule ambaye yuko kwenye ajira haitumii nafasi hiyo vizuri. Badala yake anakwepa kazi kwa visingizio visivyo na maana na hata kufanya kazi chini ya viwango.
Ambaye hajaoa au kuolewa anategemea kuoa au kuolewa na kuwa na nyumba yake wakati ambao wameoa na kuolewa wanachulia nafasi hiyo poa na kwa mazoea.
Mwenye mimba ana matumaini makubwa ya kuitwa mama siku sio nyingi na mme wake kuitwa baba. Wakati wenye wenye watoto wanawatesa bila huruma.
Tafadhali sana, usichukulie nafasi ambazo unazopata poa.
Kama wewe ni kiongozi fahamu kwamba hiyo nafasi hupaswi kuichukulia poa. Kuna watu wamepoteza nafasi hizo na kuja kuzijutia baada ya kuzipoteza.
33. MALI
Mali na vitu vyote ambavyo unamiliki usivichukulie poa. Pale ambapo unakuwa navyo vitumie vizuri ila usijishikize kwenye hivyo vitu kiasi kwamba vikipotea basi ndio na unakuwa kama umepoteza maisha yako.
Kitu kingine ni kwamba weka juhudi katika kutafuta mali na vitu vizuri ambavyo unaweza kununua hapa duniani, ila pia hakikisha unawekeza kufuatilia mwenendo wa hivyo vitu.
34. ADHABU
Kuna nyakati katika maisha ambapo wazazi au watu wanaweza kukupa adhabu kulingana na kosa ambalo umefanya. Uzichukulie poa hizi adhabu. kuna watu ambao leo hii wanakiri kwamba adhabu fulani walizopewa kipindi fulani kwenye maisha ndizo zimewafanya jinsi walivyo.
35.SUMU
Usichulie sumu poa. Kuna watu ambao wamepoteza maisha yao kwa sababu ya sumu ambazo wamekuwa wanaingiza kwenye mwili wao kama chakula au kinywaji cu chochote.
Kunywa sigara ni sumu
Kunywa pombe ni sumu
Kula vyakula ambavyo sio vizuri ni sumu
Vinywaji baridi ni sumu
Kukubali umbea na habari nyepesinyepesi ni sumu
Kuwa na marafiki ambao sio sahihi ni sumu
Wakati baadhi ya sumu huathiri mwili, nyingine kabisa huathiri roho na kuwafanya wengine waishie kuwa mateja. Hata hivyo bado kuna watu wanachukulia hivi vitu poa.
35 UCHAFUZI WA MAIZNGIRA
Kuna kipindi uharibifu wa mazingira ulikuwa unaonekana kama kitu cha maana kufanyika. Ni mpaka pale ambapo maeneo yalianza kuonekana yanaathirika, watu walipoanza kuwa makini na utunzaji wa mazingira. Hivyo walichukulia poa mazingira mazuri ila sasa baada ya kupotea ndio jumuiya za kimataifa zikaanzisha kampeni za kuyatunza.
Kuna kipindi wavuta sigara walikuwa wanavuta sigara kile sehemu. Lakini ilikuja kugundulikwa kuwa ule moshi wa sigara unawaathiri zaidi wale ambao hawavuti kuliko hata wale ambao wanavuta, ndipo watu wakaanza kuambiwa wasivute sigara maeneo ya wazi na yenye mikusanyiko ya watu
Kuna aina nyingi za uchafuzi wa mazingira ambao unaendelea na pengine wewe umekuwa mwathirika wa hii hali. Tafadhali usichukulie poa uharibifu wa mazingira.
37.UFAHARI
Ukipata nafasi ya kuishi kwenye nyumba ya kifahari, au maeneo ya kifahari basi uisyachukulie poa. Maana siku ukiyapoteza unaweza kujuta sana. badala yake itumie hiyo nafasi kwa viwango ambavyo vinasitahili. Ili hata ikitokea umeyapoteza hutakuwa na cha kujutia.
38. MCHAKATO
Ni wazi kwamba kila kitu kizuri huwa kinapitia mchakato wake.
Huwezi kuwa mzee kabla ya kuwa kijana kisha mtu mzima.
Huwezi kukimbia kabla ya kutembea. Ukidharau mchakato na mwendelezo wa vitu vya kawaida, utaumia sana kwenye maisha.
Kula tunda kabla halijaiva ni kuruka mchakato na ina madhara yake
Kutoa mimba badala ya kusubiri miezi tisa ifike mtoto azaliwe ni kuruka mchakato na ina madhara yake.
Kumbuka ukiruka ngazi kwenda hatua ya ziada kwa sababu ya kukwepa mchakato, itafikia hatua ambapo utaanguka na kurudi chini. ila ukikua kwa kufuata mchakato utajenga mafanikio ya kudumu.
39. MAONI
Mara nyingi kila mtu huwa anapenda kuona vitu kama ambavyo anataka yeye, ila sio kuona vitu kwa uhalisia wake. Hli hii huwa ina madhara yake kutokana na ukweli kwamba kila mtu ana vitu ambavyo anaweza kuona kwa uzuri na kuna vitu ambavyo hawezi kuona kwa uzuri.
Hivyo ni wazi kutambua kwamba kwenye maisha kuna pembe tofauti zakuona kitu. Ndio maana unashauriwa kusikiliza na kuwaelewa wengine kwanza kabla ya kutaka kueleweka wewe zaidi.
Unapofanya kazi na watu waachie uhuru wa kutoa maoni yao kuhusu kitu fulani na usiwathibiti kwenye kuoa maoni. Maoni ya mtu mmoja yanaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye kubadili mwenendo wa maisha yako. Tafadhali usichukulie haya maoni poa.
40. MWENDELEZO
Ni matarajio ya kila mtu kupata mwendelezo kwenye kile ambacho anafanya. Jifunze kushukur kwa vile vitu vyako ambavyo vinaendelea vizuri. Kila mara fuatilia maendeleo yako kwenye yale maeneo ambayo unahusika.
Kama maisha yako ya kiroho yanaendelea vizuri basi ENDELEA KUYATHAMINI
Kama ndoa yako inaendelea vizuri, ITHAMINI
Kama kazi yako inaendelea vizuri basi, ITHAMINI
Kama biashara yako inaendelea vizuri, ITHAMINI
Kama afya yako inaendelea vizuri, ITHAMINI
Kama mwenendo wako wa masomo uko vizur, UTHAMINI
Kama maisha yako kiujumla yanaendelea vizuri, YATHAMINI.
1. VITU UNAVYOPATA
Usichukulie poa vitu ambavyo unapata kwenye maisha yako. Iwe ni elimu ambayo unapata, au masuala ya kiroho, kiafya, kimwili, kifedha au vitu ambavyo vinashikika. Usivichukulie poa.
Kama una mme wako anakuletea vitu, MTHAMINI na VIPE THAMANI vile anavyokupa
Kama una mwanamke pia anakuletea vitu, MTHAMINI na VIPE THAMANI vile anavyokupa
Kama una wazazi ambao wanakusaidia, THAMINI kile wanachokusaidia na wao pia.
Kama una bosi wako ambaye anakusaidia, THAMINI msaada wake na uwepo wake.
Kama una familia ambayo inakujali na kukupa vitu, ITHAMINI pamoja na kile wanachokupa
Kama taifa lako linakujali, lithamini pamoja na kile ambacho wanakupa
Kama kanisani kwako au msikitini kwako wanakusaidia, WATHAMINI pamoja na kile wanachokusaidia.
Jifunze pia kutoa kwa watu wengine.
42. MAANDALIZI
Ni wazi kuwa tunaishi katika maeneo ambapo maandalizi yanapewa thamani kidogo. Ndio maana, unaweza kuona kwamba watu walikuwa na miaka minne ya kujiandaa na michezo ya kimataifa ila wanakuja kujiandaa miezi mwili ya mwisho tu.
Au watu wanakuja kukumbuka kutafuta fedha za kwenda hospitali kujifungua wiki za mwisho wakati kulikuwa na miezi tisa ya kujiandaa.
Tafhadhali usichukulie poa maandalizi. Iwe unajiandaa kwa ajili ya mitihani, mahojiano, au chochote kile. Yape thamani maandalizi na hakikisha una
43. UTABIRI
Usichukulie poa utabiri hasa ule unaohusiana na hali ya hewa, mvua na magonjwa. Kama utabiri umefanywa na kuna vielelezo ambavyo vinaonesha kutokea kwa huo utabiri, basi usichukulie poa.
44.KUPANDA
Sheria ya kupanda ni muhimu sana uifuate. Wahenga wetu wamekuwa wakisema kwamba utavuna ulichpanda. Hii sio kwamba ni habati mbaya. Hata siku moja usitegemee kuvuna pale ambapo unakuwa hujapanda. Na unapopanda hakikisha kwamba unafuatilia kile ulichopanda kukiwamgilia, kukilinda, kukiza mpaka pale utakapovuna.
45.USHIRIKIANO
Kuwa makini na yule ambaye unashirikiana naye kwenye majukumu yako. Ukishirikiana na wambea ni wazi kuwa unaenda kuwa mbea.
Ukishirikiana wezi, utaiba. Ukishirikiana na watu wanaofikiri chanya utafikiri chanya,
Kuwa makini na wale watu ambao unashirikiana nao.
46. MSUKUMO
Usichukulie msukumo poa.
Kuna aina mbili za msukumo. Msukumo chanya na msukumo hasi.
Msukumo hasi ukiruhusiwa kwenye maisha yako unaweza kukupelekea wewe kujjutia vitu ambavyo utafanya, kuumia n.k.
Hata hivyo msukumo chanya ukiutumia vizuri utakusaidia kuongeza ubora na uwezo wako.
Ukifuatilia kwa umakini kwenye maisha yako utagundua kwamba vile vitu ulivyofikia ni kwa sababu kulikuwa na msukumo nyuma yake ambao ulikusukuma wewe kwenda hatua ya ziada
47. UVUMILIVU
Uvumilivu sio kitu ch akuchukulia poa. Martin Luther King Jr amewahi kusema, “kama huwezi kupaa basi kimbia, kama huwezi kukimbia tembea, kama huwezi kutembea basi tambaa. Bila kujali ni kitu gani ambacho kinatokea kwenye maisha yako wewe endelea kusonga mbele.
Kuna awatu wengi ambao wanashindwa kufikia kile ambacho wanata kwenye maisha kwa sababu ya kuacha kufanya kitu hicho mapema na kukosa uvumilivu. Ukijaribu kitu mara ya kwanza kikawa hakijfanya kazi, basi tafuta njia nyingine ya kukifanya kifanye kazi
Uvumilivu ni moja ya siri kubwa za mafanikio na inatofautisha wanaofanikiwa na wale ambao hawafanikiwi. Usiuchukulie poa.
48. KUPANGA.
Ukosefu wa kupanga ni chanzo cha kushindwa kwa watu, jumuiya, familia, mashirikana hata makampuni. Kuna mtu mmoja ambaye amewahi kusema kwamba ukishindwa kupanga basi unapanga kushindwa. Hivyo usichukulie kupanga poa.
Kumbuka kwamba unapaswa kuwa na mipango ya muda mfupi, muda wa kati na mipango ya muda mrefu. NASHAURI UPATE KITABU CHANGU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI ILI UJIFUNZE ZAIDI KUHUSU KUPANGA NA KUWEKA MALENGO. Sura ya pili ya kitabu hicho imeandaliwa maalumu kwa ajili hili suala la mipango. Tuwasiliane kwa namba 0755848391 ili kukipata.
49. MAPUMZIKO
Ni wazi kuwa utapaswa kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuweza kufanikisha kazi zako, hata hivyo usisahau muda wa mapumziko. Na unapopanga muda huu usiuchukulie poa.
Unapopata mapumziko na familia usichukulie poa nafasi hiyo. Usiutumie muda huo kukaa kwenye mitandao ya kijamii na kuwasahau wale watu ambao unao hapo karibu. ni nafasi ya kipekee ya wewe kuwa na hao watu wako wa karibu, hivo usiichukulie poa.
50. AHADI
Ukiweka ahadi, basi hakikisha hiyo ahadi unaitimiza. Usichukulie poa ahadi ambazo unatoa kwa watu na kisha kuzivunja kama vile hakuna kitu ambacho kimetokea.
Ninaamini baada ya kuwa umesoma hapa umejifunza mengi na hivyo yale mambo ambayo umekuwa unachukulia poa, sasa hutaendelea kuyachukulia poa.
Kitabu hiki hapa ni mwongozo wa vile ambavyo hupaswi kuchukulia poa. Bila shaka kimekuwa jicho la vile vitu vyote ambavyo kwako hupawi kuchukulia poa. Hivi ni vitu gani umekuwa unachulia poa? Ni vitu gani ambavyo hutaendelea kuchukulia poa tena maishani mwako? Unaweza kuniandikia ujumbe kupitia songambele.smb@gmail.com
Baada ya kumaliza uchambuzi huu kuna watu watatu ambao siwezi kuwachukulia poa.
Kwanza siwezi kuchukulia poa mtu aliyenitumia kitabu hiki hapa, Edius Katamugora. Hivyo nipende kumshukuru sana kwa kujali na kunitumia kitu kzuri kama hiki hapa.
Pili, siwezi kuchukulia poa mtu ambaye amekutumia ujumbe huu mpaka ukakufikia wewe. Hivyo nipende pia kumshuru. Bila shaka na wewe utaufikisha kwa mwingine. usichukulie poa, kuna mtu mmoja anaweza kubadilika kwa sababu yako, ebu tuma kwa wale ambao wanajali ili nao waache kuchukulia vitu hivi poa.
Mwisho siwezi kukuchukulia poa wewe hapo kwa kuweza kusoma andiko hili mwanzo mpaka mwisho. Tuendelee kuwasiliana kupitia 0755848391
Jiunge na kundi la THINK BIG FOR AFRCA ambapo utapata kitabu kimoja cha Kiswahili kila mwezi. Kujiunga tuma ujumbe kwenda 0755848391
Kupata kitabu ambacho kimefanyiwa uchambuzi bonyeza hapa na ujaze taarifa zako. Kitabu kitatumwa mara baada ya wewe kujaa taarifa zako. Kila la kheri
https://blogspot.us14.list-manage.com/subscribe?u=35d404174ee6b730531b8d920&id=7ff0bfcfca
makala hii imeandaliwa na Godius Rweyongeza
unaweza kuwasiliana naye kupitia 0755848391
barua pepe; songambele.smb@gmail.com
MOROGORO-Tz