Rafiki yangu hongera tena kwa siku nyingine tena. Leo hii nimeona niongee kitu muhimu ambacho kinaweza kukufanya ufikie utajiri wako wa kifedha, kiroho na KIAFYA. Kama utakitumia vyema au kama utakitumia vibaya, kitakuzuia kuufikia huu utajiri. Na kitu hiki ni kusamehe.
Unaweza kushangaa hivi kusamehe kuna uhusiano gani na utajiri wangu wa kifedha, kiroho na kiafya? Unapotoa msamaha unakuwa unatuma mawimbi ya upendo, furaha, afya njema na vitu vingine vizuri kwa yule mtu ambaye umemsamehe. Na kwa vyovyote vile kama wewe unaweza kumtakia mtu mema, basi na wewe mema lazima yatakufuata. Maana hii ni sheria ya ya asili ambayo inaitwa sheria ya KICHOCHEO NA MATOKEO (law of course and effect).
Kwa sheria hii ni kwamba unavuna kile kitu ambacho umepanda. Ukipanda wema na wewe unavua wema. Ukipanda ubaya na wewe utavuna ubaya. Sasa kama wewe unamtakia mwenzako mabaya maana yake wewe mwenyewe yatakayokupata ni mabaya. Ila kama mwenzako unamtakia mema, basi na wewe mema yatakufuata.
Sasa msamaha unakuhitaji wewe uweze kumsamehe mtu kiasi cha kumbariki na kumtakia mema na mafanikio kwenye kazi. ukiona umefikia kiwango hicho hapo ujue ndio umemsamehe mtu kabisa.
Ila kama kwa nje unasema umemsamehe mtu wakati kimoyo moyo unalaani, ujue UNAJILAANI wewe mwenyewe. Maana, kwa sheria ya kichocheo na matokeo ni kwamba unavuna ulichopanda. Ukilaani, mtu unakuwa unajiilaani wewe mwenyewe.
Ukimtakia mtu mabaya yatakurudia wewe mwenyewe.
Hivyo badala ya kujihusisha na haya mambo mabaya. Badala ya kuwalaani watu na kuwatakia mabaya, chukua muda wa kuwatakia watu mema hata wale ambao wamekukosea.
Fanya hivyo mpaka pale utakapokuwa unawabariki kwa moyo wako kutoka ndani wala sio kwa kuigiza. Nakuhakikishia ukiweza kumtakia mtu mwingine mema, lazima mema yatakurudia.
Fanya hivyo hata kama mtu huyo atakuwa anaonekana kukutakia mabaya wewe
Kitu kingine kuhusu mshama ni kwamba, hautoi msamaha ili kumfurahisha mtu, hautoi msamaha ili uonekane unajifurahisha. Unasamehe kwa sababu yako wewe mwenyewe. Usiposamehe utajiumiza kwa kubaki na hasira, visasi na vinyongo ambavyo unakuwa umebeba kwenye mwili wako.
Na vitu hivi vinaweza kuanza kujionesha nje katika mifumo ya magonjwa. Kwa hiyo kuwa mtu wa kusambaza upendo. Hata kwenye familia, Hakikisha hamwendi kulala mkiwa na hasira na chuki kati yenu wanafamilia. Hata kama kumetokea kitu ambacho unaona kimekuudhi.
Siku njema