Hiki Ni Kitu Ambacho Kinapaswa Kukusukuma Wewe Kuitafuta Fedha Zaidi


 Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana, karibu sana kwenye makala ya siku ya leo ambapo ninaenda kukushirikisha kitu ambacho kinapaswa kukusukuma wewe kutafuta fedha zaidi.

  

Rafiki yangu kumekuwepo na watu ambao wana imani mbalimbali kuhusiana na fedha kiasi kwamba wengine wamekuwa wanaona aibu kuitafuta fedha. Wengine wamekuwa wanafikiri kwamba fedha ina nguvu kubwa sana kiasi kwamba wakiitafuta fedha basi, nguvu yake itawafanya washindwe kuishi maisha ambayo wao wanataka.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba fedha haina nguvu yoyote ile. Unaweza kushangaa kuisikia kauli hii. Na pengine unaweza kudhani kuwa ni kauli ambayo imekosewa, hata hivyo ukweli ni kwamba FEDHA HAINA NGUVU YOYOTE ILE.

 

KWANI NGUVU NI NINI?


usemi wa kwamba fedha ina nguvu unatokana na methali ya  la kiingereza inayosema kuwa money is power. Hivyo tunaweza kusema, kinachozungumziwa hapa ni UWEZO. Kitu kinakuwa na uwezo pale ambapo kinaweza kujizalisha chenyewe. Au pale ambapo kitu hicho kinaweza kufanya maamuzi yake. Au pale ambapo kitu hicho kinaweza kuongezeka kwa ukubwa, urefu au hata kubadili umbo lake bila kutegemea kitu kingine. Au pale ambapo ambapo kitu hicho kinaweza kutumia nguvu ya ndani kufanya mambo ya kipekee kwa kutumia rasilimali zilizo nje. Hapo ndipo tunasema kwamba kitu hiki hapa kina uwezo. Saasa je, fedha ina uwezo gani kati ya huo hapo niliouleza.

 

NI LINI TUNASEMA KWAMBA KITU KINA NGUVU NA NI LINI TUNASEMA KWAMBA KITU HAKINA NGUVU?

Ukitaka kuelewa kwamba fedha haina nguvu, ila wewe hapo ndiye mwenye nguvu napenda tu kutolea mfano wa vitu vitatu. Ukichukua noti ya elfu kumi pamoja na sarafu za shilingi miatano na mia mbili ukaviweka pamoja, kisha ukachukua mbegu ya mhindi, baadae ukachukua kuku, halafu ukachukua mtu mmoja. Ukiweka vitu hivi vyote kwenye eneo ambalo ni tambarare, na linapata mvua na kila kitu kikawa huru bila kutegemea kingine kisha ukaondoka, ukija kurudi baada ya miezi sita unaweza kukuta yafuatayo.

Fedha yako itakuwa bado iko vilevile.

Mbegu ya mhindi itakuwa imeota na kutoa mahindi mengine mengi.

Kuku atakuwa au ameondoka kwenye hilo eneo na kutafuta eneo jingine la kuishi. Au kama amebaki hapo basi atakuwa ametaga mayai na pengine kutoa vifaranga vingine.

Mwanadamu atakuwa ameondoka kwenye hilo eneo. Kama atakuwa yeye kwa hiari yake ameamua kukaa kwenye hilo eneo, basi ni wazi kuwa atakuwa amejenga na pengine atakuwa ameashaanzisha shughuli fulani za kijamii ambazo atakuwa anazifanya kila siku.

 

Ila fedha yako itakuwa haijafanya chochote kile. Sasa swali langu kwako kipi chenye nguvu kati ya hivyo vitu? Nadhani unaweza kuona wazi kuwa fedha kama fedha, yenyewe haina nguvu, wewe ndiwe mwenye nguvu na wewe ndiwe unapaswa kuipa amri fedha infanye nini au isifanye nini.

 

SASA KWA NINI WATU WANASEMA KWAMBA FEDHA INA NGUVU?

Kinachowafanya watu waseme kwamba fedha ina nguvu, ni kwa sababu  wanapokuwa na fedha wanashindwa kutuliza hisia zao. Na hivyo kushindwa kufanya maamuzi kama watu, badala yake, wanafanya maamuzi kwa kufuata hisia ambazo zinatokana na fedha. Yaani, inakuwa kama wamepatwa na pepo fulani ambalo linawasukuma kutumia fedha mpaka pale fedha inapokuwa imeisha, ndipo sasa wanarudi kwenye hali yao ya kawaida.

 

NAWEZAJE KUEPUKA HALI HII?

Hali hii hapa inaepukika. Kwanza unapaswa kuhakikisha kwamba unapopokea fedha unakuwa na uwezo wa kuituliza hata wiki kabla hujaitumia.

Pili, unapopokea fedha kuwa na bajeti ambayo unaisimamia kwenye kufanya manunuzi yako, badala ya kwenda kununua vitu tu bila mpangilio.

Tatu, hakikisha kwamba unapopokea fedha haununui kitu kwa sababu kimeonekana mbele yako. Badala yake kinapaswa kuwa kwenye mpango wako. Kama umeona kitu ni kizuri, na ukaona kama unapaswa kukilipia, basi kitafakari hicho kitu kwa wiki nzima kwanza, ukiona kwamba kuna umuhimu wa kukinunua basi hapo ndipo unaweza kuchukua hatua ya kukinunua.

Nne, igawe fedha yako kwenye mafungu muhimu. Na mafungu haya yanapaswa kuwa hivi, asilimia kumi kwa ajili ya kuweka akiba. Asilimia tano kwa ajili ya maendelea binafsi. Asilimia 10 kwa ajili ya fungu la kumi ambalo utatoa kulingana na imani yako. Asilimia 5 kwa ajili ya  maendeleo binafsi. Asilimia 60 kwa ajili ya matumizi yako ya kawaida. Asilimia kumi kwa ajili ya dharura au uhuru. Kw maelezo zaidi kuhusu hili hapa nakushauri usome kitabu changu cha MAAJABU YA  KUWEKA AKIBA. Ambacho kinapatikana kwa shilingi elfu tano (softcopy). Tuwasiliane kwa 0755848391.

 

SASA JE, NI KITU GANI KINAPASWA KUNISUKUMA KUITAFUTA FEDHA ZAIDI?


kuna watu ambao wanaona kama ni dhambi vile kuwa na fedha. Kama wewe ni mmoja wao, nakushauri uitafute fedha ili walau uweze kuwasidia wale ambao wanaihitaji. Ni wazi kuwa utakuwa msaaada mkubwa kwa kuwasaidia watu wa aina hii ukiwa na fedha kuliko pale ambapo wewe mwenyewe unakuwa unatafuta mtu wa kukusaidia fedha.

 

Rafiki yangu hili hapa ndilo nimekuandala kwa siku hii ya leo. Bila shaka umejifunza kitu kikubwa hapa.  nakutakia kila la kheri.

 

Hakikisha kuwa umejipatia nakala ya kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Kitabu hiki hapa kinapatikana kwa nakala tete, na unaweza kukipata kwa kuwasiliana name kupitia 0755848391.

 

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli

GODUS RWEYONGEZA.

Tuwasiliane kwa 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X