Jinsi Ya Kuwafanya Watu Uliowapa Kazi Wapende Kazi Uliyowapa


 

Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Siku ya leo hakikisha unaitumia vizuri kwenye safari yako ya mafanikio. Leo ningependa tujadili jinsi ya kuwafanya wale watu ambao umeaajiri waipende kazi yao na kuifanya kwa ufanisi, bila kukukimbia.

Nimeona niandike hili hapa maana kwa wiki kadhaa zilizopita nimeshuhudia watu wawili wa karibu wakihangaika na kushughulika na watu ili wamalizie kazi walizokuwa wamewapa. Mmoja alikasirika mpaka akafikia hatua ya kwenda kwenye uongozi wa kiserikali baada ya kumpa mtu kazi ili aifanye kisha akaikimbia.

 

Mwingine ameendelea kuhangaika bila mafanikio akiwa na matumaini kuwa kazi zitafanyika na kumalizika. Kitu kilichonifanya mimi niweze kushirikishwa kwenye visa vya hawa watu wawili ni kwamba nilikuwa na uhusika kwenye hizo kazi zenyewe, japo nilikuwa sisimamii kazi moja kwa moja.ila hao watu wote wawili tofauti walikuwa wanatoa ripoti kwangu juu ya maendeleo ya kazi.  hivyo nimeona ushauri niliowapa kuhusu jinsi ya kushughulika na watu linapokuja suala la kazi nikupe na wewe.

 

KITU GANI KINAWASUKUMA WATU KUFANYA KAZI

Asilimia kubwa ya watu wapo tayari kufanya kazi, sio kwa sababu wanazipenda, ila wanafanya tu kwa ajili ya kupata fedha ya kujikimu na kutimiza mahitaji yao ya kila siku. Kwa hiyo unaweza kuona hapo kuwa kinachowasukuma watu kwanza kabisa kwenye kazi sio UPENDO WA KAZI, bali ni UPENDO WA FEDHA. Sasa unapokuwa una mtu ambaye anatanguliza fedha mbele kabla ya kazi unapaswa kuwa makini sana unapompa kazi. na ikiwezekana usimpe kazi kabisa. kazi inapaswa kutangulia kwanza kabla ya fedha.

 

Ila kwa vyovyote vile iwe msukummo wa mtu kupata kazi ni wa fedha au upendo wa kazi, pale unapompa kazi, hakikisha;

 

1.Umempa vigezo kamili vya kazi yako. Huu uwe ni mkataba wa kazi yako unayotaka aifanye. Mwelekeze hiyo kazi inabidi ifanyikeje, lakini kuwa makini kumwelekeza mwisho wa kazi yako unapaaswa kuwa lini.  Maandishi yanakuwa ni bora zaidi kuliko kumwambia mtu kwa maneno. Maandishi yatakusaidia hata pale unapotaka kumkumbusha mtu kazi inavyopaswa kufanyika na kumalizika. Kama hakuna uwezekano wa kuandika basi maelewano yam domo uyasisitize kwake ili ajue anachopaswa kufanya. Maana kuna watu wanaweza kujidai wamekusikia ila kumbe wanapoenda kufanya kazi wanafanya kinyume chake. Baadae wanakuja kukwambia si tuliongea hivi na mimi nimefanya kama tulivyoelewana. Wakati wewe ulikuwa umewapa maelekezo mengine. Sasa ili kuepuka hili hapa, yasisitize sana mambo ya muhimu unayopenda yafanyike kwenye kazi yako au la, ANDIKA MKATABA.

 

2.Tarehe ya kuhitimisha kazi iwe mbele kidogo ya ile tarehe ambayo wewe mwenyewe ungependa kazi iwe imekamilika. Yaani, mfano kama wewe ungependa kazi iwe tayari mwishoni mwa mwezi kumi mwaka huu. Basi unaweza kuwambia mtu huyo kuwa anapaswa kumaliza kazi hiyo mwanzoni mwa mwezi huo wa kumi au katikati. Ili ikitokea kuwa hajamaliza kwa wakati unakuwa na muda wa kumsukuma zaidi ili aimalize bila ya kuwa nje ya malengo yako binafsi.

3. USIMLIPE mtu kama bado hajamaliza kufanya kazi. Kama yatahitajika malipo, basi mlipe kiasi cha fedha ambacho ni kidogo kulinganisha na kazi ambayo tayari amefanya. Ila sio zaidi ya ile kazi ambayo amefanya. Ukimlipa kiasi kikubwa ataikimbia kazi. hii ni kutokana na ukweli huo ambao tumauona hapo juu kuwa watu wengi hawasukumwi na UPENDO WA KAZI bali UPENDO WA FEDHA kwenye kazi. hivyo, unapokuwa umempa mtu fedha na wakati huo mtu huyo anasukumwa na upendo wa fedha kufanya kazi. ujue kuwa mtu huyo umempoteza kabisa. akiangalia kuwa kazi iliyobaki ni kubwa kulinganisha na fedha iliyobaki, ataondoka na kuiacha kazi, kitu ambacho kitakuwa ni usumbufu mkubwa sana kwako.

 

Hakikisha kwamba muda wote, ile nguvu ya fedha ipo kwako. kiasi mtu akiangalia kazi aliyoifanya na fedha ambayo amepokea, basi anaona tu aendelee na kazi asije kuikimbia.

 

 

Rafiki yangu hayo ndiyo mambo muhimu sana ambayo unapaswa kuyazigatia katika kazi na katika kuajiri ili watu wasije wakakukimmbia na kuiacha kazi yako.

SOMA ZAIDI: jinsi ya kujiimarisha kifedha katika hali zote unazopitia
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA
Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X